sisalimii maana maneno yatakuwa mengi! lol
wapenzi wa mmu, leo naomba tujadili ni wapi tunakosea katika mahusiano. watu wengi wamekuwa hawafurahii mahusiano, wakati wanaume wanatuona wanawake tupo kama mafisi tunajali maslahi zaidi na sie tunawaona wao kama manyani kudandia kila mwanamke. tunakosea wapi? binafsi naona kuna mambo tunakosea katika kuanzisha na kuendeleza mahusiano.
Hapa ni kweli na kwa kuwafahamisha tu ni kwamba tatizo lingine liko hapa
Tabia ya kumtafuta wa kumlaumu tatizo linapotokea bila kujitazama kwa nza wewe ni hasara kuu
Kila mmoja anajiona hana hatia hapo ndipo anashindwa kujifunza ili kuboresha mahusiano yajayo
1. tunakosea katika kuchagua mpenzi sahihi.
ni ukweli ulio wazi kuwa kila mtu ana vigezo vya mpenzi anaependa awe nae. inapotokea mtu amekuwa single muda mrefu hujikuta ameanzisha mahusiano na mtu hata kama hana vigezo alivyokuwa anaviwaza awali. wakati upo kwenye mahusiano sasa antokea mtu mwenye vigezo vyote ulivyovitaka na hapo ndipo usaliti huanza. a nashauri utulie na utampata yule umfikiriae hata kama itakuwa muda mrefu kiasi gani, jitulize na epuka kufanya hili kosa.
Hapa nina mtazamo tofauti na wako
Tatizo kuu hapa ni hivyo "vigezo"
Unakuaje na vigezo kwenye kuchagua mume/mke?
Ninavyojua mimi kuna kazi ambazo zinakuwa na vigezo ili uweze kuipata kwa sababu inahitaji utaalam na uzoefu,mfano udaktari wa binadam ni lazima uwe umeusomea,huwezi kutibu bila kuwa na mafunzo ya udaktari
Sasa kwenye suala la mapenzi unaweka vigezo ili nini?
Nijuavyo mimi ili mtu awe na sifa ya kuwa mume/mke ni vyema[sio lazima] awe anajitambua BASI
Unapoweka vigezo jua kwamba hivyo vigezo unaviweka wewe na huenda hakuna mtu wa namna hiyo
Kwanza vigezo ni nini?
2.kosa katika hatua ya awali kabisa. wengi huwa hatujadili aina gani ya uhusiano tunaoutaka. wakati mwingine anafikiria mambo ya "mpaka kifo kitutenganishe" kumbe mwenza wake anafikiria kula bata tu. ni vizuri kujadili mapema kuhusu aina ya mahusiano yenu.
Haya nayo ni matatizo mengine
Unajua tatizo linalotukabili wengi ni maradhi ya kutamani kupendwa
Wengi hatukupewa upendo tangu utoutoni na hatujafundishwa upendo ni nini,hivyo tunajikuta tuna njaa ya kupendwa sana
Sasa tunapokuwa tunakuwa tunasaka sana watu wa kutupenda ili wazibe pengo lililoachwa na wazazi wetu
Hapa ndipo tunapoingia mkenge
Unakutana na mtu unamuona kabisa hana muda na kujadili ndoa na wewe achilia mbali kuoana,kwa hofu ya kupoteza kupendwa unaogopa kumuuliza,unajikuta muda umeenda bila kuwa na "fyucha" yoyote
Hovyo sana sisi!
3. tunakosea tunapotaka wenzi ambao wapo perfect katika kila kitu wakati tunajua hakuna mkamilfu. unapokuwa katika mahusiano ni vizuri kuyakubali na kuyavumilia mapungufu ya mwenzi wako badala ya kufikiria kumbadilisha kuendana na unavyotaka awe maana ni ngumu mno..
Safi sana hii
Hii ningependa wanawake waizingatie sana maana wanamatatizo sana eneo hili!
4.tunaposhindwa kuwa na muda na wapenzi wetu pia tunakosea.si ajabu kuona mtu anaspend muda mwingi na marafiki kuliko mpenzi wake ambae ni mtu wake wa karibu zaidi. waweza kuona ni kawaida lakini kadri tunavyojiweka mbali na wenzi wetu tunazidi kuchujisha penzi.
Hapa kuna makundi mawili ya matatizo yanayohusiana na hili
Kundi la kwanza ni lile la mahusiano kabla ya ndoa
Hapa tatizo hili huwa sio kubwa sana
Hapa huwa muda mwingi wapenzi huwa wanakuwa pamoja kwa kuwa hapa ndipo wakati wa upofu wa "mapenzi"
Hapa watu hushindwa kabisa kukaguana!
Kundi la pili ni lile la wanandoa
Hap ndipo tatizo hili lipo kwa kiasi kikubwa sana hasa watoto wanapozaliwa
Mama anakuwa bize na watoto kuwaosha,kunyonyesha n.k
Baba nae majukumu yanaongezeka hivyo anakuwa anafanya kazi kwa kiwango kikubwa sana
Matokeo yake ni kuchokana na kulalamikiana kuwa mmoja hamjali mwenzake
Nyumba ndogo hutafutwa sana kipindi hiki!
hayo ni baadhi ya tunayoyakosea, nakaribisha wana mmu tujadili wapi pengine tunakosea kwa pande zote mbili ke na me.
Usijali umefanya kazi nzuri
ushauri wa bure:
ruhusu moyo wako kupenda bila kujali umetendwa mara ngapi maana katika kila mahusiano unayoumizwa ni changamoto ya kukufanya uwe imara katika mahusiano yako yajayo.
Hapa siongezi neno!!!!!!!!!