Wapi "This week In perspective" na Babu Simbeye!

swagazetu

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
4,250
1,467
Wadau napenda kuuliza juu ya kilipoishia na kiliishaje kipindi hiki bora kilichokuwa kikiendeshwa na Mzee Simbeye cha This week in Perspective kilichkuwa TBC kila alhamisi kama sikosei.

Je ndiyo kilikufa au Babu Simbeye hatuna?

Hivi Mzee Simbeye alikuwa mtumishi wa serikali katika kitengo gani na mbona kwenye siasa na kokote hasikiki kabisa?
 
Umenikumbusha mbali aisee. Nina zaidi ya mwaka sijaiona TBC wanaofahamu kilipoishia watatueleza
 
Kwani wewe si miongoni mwa wale waliokuwa wanalilia Bunge kuoneshwa live na TBC? Au umesahau?
 
Wadau napenda kuuliza juu ya kilipoishia na kiliishaje kipindi hiki bora kilichokuwa kikiendeshwa na Mzee Simbeye cha This week in Perspective kilichkuwa TBC kila alhamisi kama sikosei.

Je ndiyo kilikufa au Babu Simbeye hatuna?

Hivi Mzee Simbeye alikuwa mtumishi wa serikali katika kitengo gani na mbona kwenye siasa na kokote hasikiki kabisa?
Kipindi cha "This week in perspective" kilichokuwa kinaendeshwa na Adam Simbeye na kuoneshwa kila ijumaa saa 2.30 usiku kilikuwa na changamoto kubwa kwenye uendeshaji wake. Kwa kuwa kilikuwa kinaendeshwa kwa lugha ya kiingereza, kuwapata washiriki ilikuwa kazi kubwa mno.Simbeye akipeleka mwaliko kwa mtu kushiriki mara nyingi mtu aliyealikwa hutoa visingizio kibao kukwepa kuhudhuria.Hali hii ilimfanya Simbeye kushindwa kuendesha kipindi hivyo akakifutilia mbali.
 
Welcome to this week in perspective with Adam Simbeye. Ninakumbuka mzee alikuwa anaanza hivyo.
 
Kipindi cha "This week in perspective" kilichokuwa kinaendeshwa na Adam Simbeye na kuoneshwa kila ijumaa saa 2.30 usiku kilikuwa na changamoto kubwa kwenye uendeshaji wake. Kwa kuwa kilikuwa kinaendeshwa kwa lugha ya kiingereza, kuwapata washiriki ilikuwa kazi kubwa mno.Simbeye akipeleka mwaliko kwa mtu kushiriki mara nyingi mtu aliyealikwa hutoa visingizio kibao kukwepa kuhudhuria.Hali hii ilimfanya Simbeye kushindwa kuendesha kipindi hivyo akakifutilia mbali.
wale wazee wanaosemaga watu wa zamani wanajua kiingereza wamefariki wote?

hawana lolote,wamehamishia nguvu Alhamisi kwa Mzee Mengi
 
Au kwa kuwa Simbeye hakuwa mtu wa itikadi za vyama tbc wakaona hatawasaidia kuwapa promo!
 
Back
Top Bottom