Wapi nitapata nguo za mitumba za watoto zenye ubora?

minatouch

Member
Sep 23, 2021
13
24
Okay naswali kwa wakazi wa Dar ni wapi wanauza mitumba grade one au two mizuri ya nguo za watoto mana mmi hununua zile za jero Ilala za wakubwa lakini biashara inaenda taratibu nataka nianze za watoto nipo Dar nipeni chimbo na mda sahihi niende.
 
Binafsi sijawahi kujishughulisha na biashara hiyo, ila Cha kukusaidia humu Kuna nyuzi nyingi zilizojadiliwa kwa kina kuhusiana na Hilo hitaji lako mkuu...
 
Hello guys naomba kujuzwa mtaa wa ashanti ilala wanauza nguo za mtumba bei gani je wanauza mabalo ya nguo ama amna wenye connection na wafanyabiashara pale nawaomba wanisms pm maisha ni kusaidiana only serious people
 
Ilala hakuna mtaa wa Ashanti kama unazungumzia pale sokoni linapoonekana bango lao ule ni mtaa wa Morogoro japo ulibadilishwa jina na kuitwa mtaa wa Ramadhani Mwinshehe(Baba yake Ditopile) lakini bado unavuma mtaa wa Morogoro.
 
Huo naujua nmeambiwa ni mbele eti kma unaenda machinga
 
Mbele yake ni mtaa wa tabora au Rajabu Diwani kule sana sana naona kuna kisoko kidogo wanauza nyanya kwa jumla na wachuuzi wa viungo vya nyumbani kama vitunguu, tangawizi, vitunguu saumu n.k biashara ya nguo mtaa ule sio sana.
 
Nmeelekezwa kua n mbele kabsa sio hapo jilan ninjilaninna machanga naambiwa ivo sasa sielewi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom