Asante sana. Japo kwa jinsi nilivyowaona hao high life nao wanaonekana ni retailers kama mimi. Kwa kweli nahitaji muuzaji wa jumla.Vizuri...
Na kweli Arusha kuna uhaba wa maduka ya simu za kueleweka aisee, Benson & Company naye yupo juu sanaa....
Jitahidi usikubali mtu akudalalie...
Kwa simu za samsung OG zenye uhakika jaribu hawa Highlife TanzaniaView attachment 1457970
Ingia tuu kwenye social network search hilo jina au ingia google search website yao
Asante kwa ushauri mzuri sana. Kuna muuzaji yeyote wa jumla unaemfahamu unisaidie?tumia muda tembelea wauzaji wa jumla kama 5 pia usinunue mzigo wote kwa wakati mmoja kusudi upate muda wa kujifunza na kujua ulikokosea na demand ya wateja ukikosea ni umepotea. asiyesikia la mkuu jitahidi upate muda kujua kila kitu hatua za mwanzo ukiwa na middle men unayemsikiliza umepotea lazima ujiongeze sana biashara mpya ni ngumu mno
Kila biashara ina siri zake ambazo kamwe huwezi kuambiwa mpaka uingie na nyingine unaweza usikae kuzijua na biashara ndio imekukuza. Mungu akuongoze
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa ushauri. Japo tayari nishakopa ila ilinibidi nifanye hivyo kwa sababu biashara ya simu huwa inahitaji mtaji mkubwa kidogo. Cha msingi ni kutafuta wateja kwa bidii ili pesa ya watu irudi kwanza.Sema umekosea sana kukopa kwa biashara unayoanza, ilitakiwa utumie mtaji wako kwanza kuijua biashara, ili ukikopa uwe unajua na challenges zake, hapo utalipa riba kwa pesa amabyo huitumii au labda ujitoe mhanga na mtaji wote , which is highly not recommended.
Sent
Uko kwenye hali ngumu kwanza taarifa unazotafuta muda huu ulipaswa kuwa nazo kitambo sana kabla hujakopa ukiingia kariakoo kuna madalali kibao kwa Mara ya kwanza lazima upigwe tu hakuna namna utauziwa masimu yenye matatizo mengine batri mbovu, nyingine zimetolewa housing, nyingine hazina earphones mambo ni mengi.Asante kwa ushauri mzuri sana. Kuna muuzaji yeyote wa jumla unaemfahamu unisaidie?
Uko kwenye hali ngumu kwanza taarifa unazotafuta muda huu ulipaswa kuwa nazo kitambo sana kabla hujakopa ukiingia kariakoo kuna madalali kibao kwa Mara ya kwanza lazima upigwe tu hakuna namna utauziwa masimu yenye matatizo mengine batri mbovu, nyingine zimetolewa housing, nyingine hazina earphones mambo ni mengi.
Vipi fremu tayari ushalipia, je muuzaji unaye? Tafuta marafiki wanaofanya biashara kama hiyo muwe mnabadilishana mawazo na changamoto. Ukikutana na mtu mmbaya utauziwa mizigo ambayo haitoki kirahisi yaani mzigo wa zamani uliopitwa na wakati
Nakupa mbinu apo arusha tembelea Maduka ongea nao jua simu zipi zinatembea sana waambie unahitaji kuanza hii biashara unamuomba ukupe muongozo utamlipa mtajie kuwa una mtaji wa chini kidogo lakini badae utachukua mkopo asijue kama una pesa nyingi ataingia tamaa kuona wewe ni fursa anakutapeli ni kawaida sana.....tayari ukimpata Kijana aliyeajiriwa kuuza ndio wazuri huwa wanatoaga taarifa kwa wepesi sana muhimu muambie kuwa utamlipa unachotaka ni akupe tu muongozo unaweza mkaongea hapo hapo ama mkakutana jioni baada ya kazi.
Kuchukua mzigo safiri nae usimkabithi pesa yako ili na wewe ujue chocho zote mjini ukifika uko nako unajiongeza tembelea Maduka mengi ya size yako taarifa sahihi ni mtaji namba moja kwenye biashara
Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi, anatakiwa auze simu, ambazo zina wateja wengi, Smart phone, pia zisiwe nyingi kuliko simu ndogo.Samsung utokaji wake Ni mdogo...wekeza nguvu kubwa kwenye Tecno ndogo
528,660,661,301,351,372...313,and so more
Itel
Xtigi
Jx
Pia smartphones tecno,itel,infinix and so more.....
Pia covers ,za aina zote kwa ukihitaji taatifa zaidi usisite kuuliza hapa
Mnama.....mbeya