Wapi nitanunua simu kwa bei ya jumla

Joel360

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
981
631
Habari zenu wadau wa jukwaa la biashara.

Mdau mwenzenu nimewaza sana biashara ya kufanya baada ya kudunduliza kwa mda mrefu sana Tsh 10 millions na nikakopa 10 million jumla nna 20 million, nimeona nifanye biashara ya kuuza simu.

Mpango wangu ni huu.
Soko/Frame: Arusha mjini.

Brand: Samsung ambazo bei zake ni ndogo na za kati.

Kwa sasa nimeshughulikia maswala ya frame na leseni ya biashara tayari. Ila sasa ninapokwama ni kupata muuzaji wa simu wa bei ya jumla, ambae ataniuzia bei ambayo namimi nikiuza nipate faida.

Au kama hakuna wauzaji wa bei za jumla Tanzania basi naomba kama kuna mtu atanielekeza namna ya kununua china ili nijipange tena kwa muda mwingine nisafiri.

Natanguliza shukrani
 
Vizuri...
Na kweli Arusha kuna uhaba wa maduka ya simu za kueleweka aisee, Benson & Company naye yupo juu sanaa....

Jitahidi usikubali mtu akudalalie...

Kwa simu za samsung OG zenye uhakika jaribu hawa Highlife Tanzania
Screenshot_20200524-022059.jpg

Ingia tuu kwenye social network search hilo jina au ingia google search website yao
 
Tumia muda tembelea wauzaji wa jumla kama 5 pia usinunue mzigo wote kwa wakati mmoja kusudi upate muda wa kujifunza na kujua ulikokosea na demand ya wateja ukikosea ni umepotea.

Asiyesikia la mkuu jitahidi upate muda kujua kila kitu hatua za mwanzo ukiwa na middle men unayemsikiliza umepotea lazima ujiongeze sana biashara mpya ni ngumu mno

Kila biashara ina siri zake ambazo kamwe huwezi kuambiwa mpaka uingie na nyingine unaweza usikae kuzijua na biashara ndio imekukuza. Mungu akuongoze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vizuri...
Na kweli Arusha kuna uhaba wa maduka ya simu za kueleweka aisee, Benson & Company naye yupo juu sanaa....

Jitahidi usikubali mtu akudalalie...

Kwa simu za samsung OG zenye uhakika jaribu hawa Highlife TanzaniaView attachment 1457970
Ingia tuu kwenye social network search hilo jina au ingia google search website yao
Asante sana. Japo kwa jinsi nilivyowaona hao high life nao wanaonekana ni retailers kama mimi. Kwa kweli nahitaji muuzaji wa jumla.
 
tumia muda tembelea wauzaji wa jumla kama 5 pia usinunue mzigo wote kwa wakati mmoja kusudi upate muda wa kujifunza na kujua ulikokosea na demand ya wateja ukikosea ni umepotea. asiyesikia la mkuu jitahidi upate muda kujua kila kitu hatua za mwanzo ukiwa na middle men unayemsikiliza umepotea lazima ujiongeze sana biashara mpya ni ngumu mno

Kila biashara ina siri zake ambazo kamwe huwezi kuambiwa mpaka uingie na nyingine unaweza usikae kuzijua na biashara ndio imekukuza. Mungu akuongoze

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa ushauri mzuri sana. Kuna muuzaji yeyote wa jumla unaemfahamu unisaidie?
 
Sema umekosea sana kukopa kwa biashara unayoanza, ilitakiwa utumie mtaji wako kwanza kuijua biashara, ili ukikopa uwe unajua na challenges zake, hapo utalipa riba kwa pesa amabyo huitumii au labda ujitoe mhanga na mtaji wote , which is highly not recommended.

Sent
 
Asante kwa ushauri. Japo tayari nishakopa ila ilinibidi nifanye hivyo kwa sababu biashara ya simu huwa inahitaji mtaji mkubwa kidogo. Cha msingi ni kutafuta wateja kwa bidii ili pesa ya watu irudi kwanza.
 
Asante kwa ushauri mzuri sana. Kuna muuzaji yeyote wa jumla unaemfahamu unisaidie?
Uko kwenye hali ngumu kwanza taarifa unazotafuta muda huu ulipaswa kuwa nazo kitambo sana kabla hujakopa ukiingia kariakoo kuna madalali kibao kwa Mara ya kwanza lazima upigwe tu hakuna namna utauziwa masimu yenye matatizo mengine batri mbovu, nyingine zimetolewa housing, nyingine hazina earphones mambo ni mengi.

Vipi fremu tayari ushalipia, je muuzaji unaye? Tafuta marafiki wanaofanya biashara kama hiyo muwe mnabadilishana mawazo na changamoto. Ukikutana na mtu mmbaya utauziwa mizigo ambayo haitoki kirahisi yaani mzigo wa zamani uliopitwa na wakati

Nakupa mbinu apo arusha tembelea Maduka ongea nao jua simu zipi zinatembea sana waambie unahitaji kuanza hii biashara unamuomba ukupe muongozo utamlipa mtajie kuwa una mtaji wa chini kidogo lakini badae utachukua mkopo asijue kama una pesa nyingi ataingia tamaa kuona wewe ni fursa anakutapeli ni kawaida sana.....

Tayari ukimpata Kijana aliyeajiriwa kuuza ndio wazuri huwa wanatoaga taarifa kwa wepesi sana muhimu muambie kuwa utamlipa unachotaka ni akupe tu muongozo unaweza mkaongea hapo hapo ama mkakutana jioni baada ya kazi.

Kuchukua mzigo safiri nae usimkabithi pesa yako ili na wewe ujue chocho zote mjini ukifika uko nako unajiongeza tembelea Maduka mengi ya size yako taarifa sahihi ni mtaji namba moja kwenye biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana
Uko kwenye hali ngumu kwanza taarifa unazotafuta muda huu ulipaswa kuwa nazo kitambo sana kabla hujakopa ukiingia kariakoo kuna madalali kibao kwa Mara ya kwanza lazima upigwe tu hakuna namna utauziwa masimu yenye matatizo mengine batri mbovu, nyingine zimetolewa housing, nyingine hazina earphones mambo ni mengi.

Vipi fremu tayari ushalipia, je muuzaji unaye? Tafuta marafiki wanaofanya biashara kama hiyo muwe mnabadilishana mawazo na changamoto. Ukikutana na mtu mmbaya utauziwa mizigo ambayo haitoki kirahisi yaani mzigo wa zamani uliopitwa na wakati

Nakupa mbinu apo arusha tembelea Maduka ongea nao jua simu zipi zinatembea sana waambie unahitaji kuanza hii biashara unamuomba ukupe muongozo utamlipa mtajie kuwa una mtaji wa chini kidogo lakini badae utachukua mkopo asijue kama una pesa nyingi ataingia tamaa kuona wewe ni fursa anakutapeli ni kawaida sana.....tayari ukimpata Kijana aliyeajiriwa kuuza ndio wazuri huwa wanatoaga taarifa kwa wepesi sana muhimu muambie kuwa utamlipa unachotaka ni akupe tu muongozo unaweza mkaongea hapo hapo ama mkakutana jioni baada ya kazi.

Kuchukua mzigo safiri nae usimkabithi pesa yako ili na wewe ujue chocho zote mjini ukifika uko nako unajiongeza tembelea Maduka mengi ya size yako taarifa sahihi ni mtaji namba moja kwenye biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupe mrejesho mkuu ulifika wapi? Ulijaribu kuulizia Nairobi? Huwa naskia pako vizuri.
 
Kwani hapo Arusha bei zikoje wakubwa,natamani sana kujua bei za memory cards jumla hasa 128mb kwa hapo Arusha
 
Samsung utokaji wake Ni mdogo...wekeza nguvu kubwa kwenye Tecno ndogo
528,660,661,301,351,372...313,and so more
Itel
Xtigi
Jx

Pia smartphones tecno,itel,infinix and so more.....

Pia covers ,za aina zote kwa ukihitaji taatifa zaidi usisite kuuliza hapa

Mnama.....mbeya
Uko sahihi, anatakiwa auze simu, ambazo zina wateja wengi, Smart phone, pia zisiwe nyingi kuliko simu ndogo.

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom