Mkwanzania
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,256
- 5,013
Waungwana habari zenu. Leo nimekaa nikawa napitia pitia makarabrasha mbalimbali ya mipango ya serikali nikakutana na hili la mji mpya wa Kigamboni. Katika pitia zangu nikaona jinsi ile master plan ilivyokuwa inavutia na kubarisha kabisa maisha na taswira ya jiji la Dar es Salaam.
Hapa naona mradi ulikuwa unaanza mwaka 2011 mpaka 2030 na ulikuwa unaendeshwa kwa awamu (phases). Kwa mujibu wa Master plan kwa sasa 2011-2020 ilikuwa ni phase ya kuendeleza miundombinu kwa ajili ya kuunganisha Dar es Salaam CBD na maeneo mengine. Maana yake ni kwamba sasa hivi Kigamboni ingekuwa imetapakaa barabara mpya za kisasa ili kurahisisha mobility ya mji mpya na Dar CBD.
Nakumbuka kipindi cha miaka kama minne nyuma jinsi hii project ilivyokuwa imeshika kasi na kupelekea kusababisha mivutano isiyokwisha baina ya Waziri wa Ardhi enzi zile Mama Tibaijukwa na Mbunge wa Kigamboni Mh Ndugulile. Lakini toka serikali mpya iingie Madarakani sioni dalili zozote za mradi huu wa aina yake kuendelea. Maswali yangu machache ni kwamba je mradi bado upo? Kama upo nini kinakwamisha huu mradi? Kama sio kipaumbele cha serikali mpya je ni nini kilikuwa nyuma ya pazia ya huu mradi?
Karibuni sana.