Wapi naweza kujifunza Kingereza cha kuongea na kuandika

sijui kwa hapa arusha ntawezaje kupata huduma kama hiyo,mimi naweza kuongea na kuandika vizuri tu(kwa level za 2nd language) ila ukinichomekea swali la ghafla,naanza kuyumba!!au ghafla nikitakiwa nielezee kitu ambacho hakikuwa kwenye mawazo yangu kabisa,utanionea huruma mswahili mie! Stutter stutter zinaanza chap!
 
kweli AIBU na kutojiamini tu.. mbona paulsen ,maximo walikuwa nachapia sana... hata wazungu wenyewe wanachapia sana kiswahili ila hawana AIBU wao wanaongea ..mie nadhani kuthubutu kuongea kwa kujiamini ndio ngao .. na kujitahidi kusoma sana vitabu na majarida mbalimbali kama unapata wasaa wakuhudhuria makongamano na warsha unajitahidi kuongea..
 
Mimi pia si mzuri ktk lugha hii ila niko tayari kushare kile kichache kwa kuzungumza ktk simu.
Ambae yuko tayari apige cm hizi tutakua tunazungumza kwa kujifunza nadhani tunaweza kupata faida kidogo kwa kuzungumza na kuelekezana.
Nawakaribisha wote tusaidiane.
Hii ni kwa anaeweza kuzungumza vizuri na hata asie weza vizuri.
For the sake of learning here we go
0755009876 or 0712279177
Call me and lets speak some english.
 
Mimi pia si mzuri ktk lugha hii ila niko tayari kushare kile kichache kwa kuzungumza ktk simu.
Ambae yuko tayari apige cm hizi tutakua tunazungumza kwa kujifunza nadhani tunaweza kupata faida kidogo kwa kuzungumza na kuelekezana.
Nawakaribisha wote tusaidiane.
Hii ni kwa anaeweza kuzungumza vizuri na hata asie weza vizuri.
For the sake of learning here we go
0755009876 or 0712279177
Call me and lets speak some english.

Nyie ndo mliokuwa mnakimbia vibao vya speak english eeeee
 
Kwa levo uliyonayo hustahil kutafuta pa kufundishwa kuongea, utashangaliwa, tatzo huna system ya kuingea mara kwa mara, So tafuta rafiki hata kweny mtandao ambae hajui Kiswahil uwe unaongea nae sana na kuchat

kweli sometime interaction yetu na watu tulionao mimi binafsi marafiki wamenisadia sana tena wa nchi tofauti tofauti kila siku nilikuwa naifunza kitu kipya .
 
Huna haja ya kuanza kutafuta sehemu kama umesoma mpaka chuo,ingawa nakubali kwamba kufika chuo haimanishi mtu yuko vizuri ila naamini una basics na unaweza kujifunza mwenyewe.
Tatizo lako liko na watanzania wengi na chanzo chake ni sisi wenyewe,sijui siku hizi ila wale tuliopita st.Government tulikuwa tunavunjana moyo sisi kwa sisi,watu hawafanyi mazoezi au hawaongei kiingereza muda mwingi,primary na secondary ukiongea english wenzako wanakuona unajiona,unajifanya unajua kumbe in a long run tunaumizana.Kwa level yako nakushauri soma vitabu ukiweza pata vile vya zamani ni vizuri kama "Brighter grammar series”, “revision English”, “common mistake in English” na vingine vingi.Tafuta watu wa kuongea nao kama una access na mtu anayejua English only it is better,pia angalia movie upime uwezo wako wa kusikia maneno na penda kujisomea vitabu na kusoma habari zilizoandikwa kingereza.Siku hizi resources ni nyingi kuliko unavyoweza kufikiria,youtube unaweza pata video zinazofundisha chochote unachotaka kujua only if you will search using the right words.
Wewe mwenyewe penda kuongea kingereza angalia wazungu wakija Bongo ,muda wote wanataka waongee Kiswahili ,why?Anahitaji kujifunza kutoka kwako.
 
kingereza kingreza ....njo nkupige msasa..una sh ngapi?
wengine wanawaza hela wengine wanawza kijua kingreza, basi mji umejaa mawazo.....
 
Hii thread ni ya mwaka jana bila shaka atakuwa ameshajua kiingereza na amebadili Avatar nyingine ya kiingereza
 
jf mi ni mhitimu wa shahada chuo kikuu, ila napenda kuimprove kingereza changu sijui wapi pa kujifunzia penye walimu waliobobea

Kama wewe ni mhitimu wa elimu ya juu basi msingi unao, kinachofuata ni wewe kujisukuma na kufanya mazoezi. Unaweza ukaenda ata uingereza, kama haufanyi mazoezi ya kuongea, utaishia kuwa bubu kwenye majadiliano. Pa kujifunza ni kuanza na wewe, ila kama wasisitiza kwenda kwenye taasisi basi nenda British Council, ila ukitoka hapo kama haufanyi mazoea ya kuongea ni kazi bure.
 
Back
Top Bottom