Wapi hukuelewa kuhusu movie ya Jumong na Spatacus?

1.Sikujua kwann thracian walikataa ofa ya legatus kujiunga na jeshi la roma?
2.kuna uhusiano gani kati ya bathiatus na vigogo wa serikali wakati anamadeni na sio kiongozi..
JIBU LA SWALI LA 2
Quintus lentulus bathiatus alikua mridhi wa baba yake titus lentulus bathiatus katika ludus ya familia yao iliokua jijin capua. ludus ambayo mwanzo ilikua chini ya baba yake ilijihusisha na kuwatafuta, kuwafundisha na kuwauza ma gladiator ambapo kwenye utawala wa baba yake champion alikua ni gannicus na mwisho wa utawala wa baba ake alipatikana cricsus na kwenye utawala rasmi wa quintus akapatikan mthrecian ambaye hawakulijua jina lake wakaamua kumuita spatucus (former threcian king). biashara hiyo ya magladiator ndio iliompa pesa na umaarufu mkubwa hasa baada ya ujio wa spatucus maana mapambano yake yalichukua vichwa vya habari nchini rome hasa capua. baadae quintus alitaman kuingia kwenye siasa japo alishindwa
 
1.Sikujua kwann thracian walikataa ofa ya legatus kujiunga na jeshi la roma?
2.kuna uhusiano gani kati ya bathiatus na vigogo wa serikali wakati anamadeni na sio kiongozi..
JIBU LA SWALI LA KWANZA
wa threcian na warome hawakua kwenye mahusiano mazuri kwa miaka mingi wa rome waliwachukulia wa threcian kama wapiganaji tu na watumwa ila sio kama wenzao kwa maana ya kwenye uongozi wao wangetumika tu kupigana hivyo kwa kulinda utu wao na kabila lao wa threcian wasingeweza kukubali hata kiongozi wa rome alietuma ombi hilo alisema kabsa hawawezi kukubaliana na wazo letu
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Jumong mwanzo hadi mwisho sikuelewa,naomba nieleweshwe hatua kwa hatua,yaan episode kwa episode..asante
movie ya jumong inaanza baada ya wavamizi kuivamia ardhi ya wagojosen na kuligawanya taifa hilo katika matabaka na makabila mengi. Han na puyol ndio zilizochukua eneo kubwa hasa Han empire. mataifa haya mawili (han na puyol) waliweza kuzifuta records zlte za taifa la joseng na kubaki na nyaraka zao muhim kuhus mipaka ya taifa hilo majina ya miji ya taifa hilo technologia ya taifa hilo ambayo waliificha kwa maandishi ya code na namna ya uongozi wake kwa ujumla. wagojosen baada yake waligeuka watumwa wa ardhi yao wenyewe. alitokea mtu wa kuwapambania wagojosen alieitwa haemosu alipendwa na kuungwa mkono na wagojosen ila kwa wakati huo haemosu alikuahana taarifa zozote kuhus taarifa za mipaka (boundaries) za nchi anayotaka kuipambania alifanya hivyo kuokoa watu tu wanaoteseka. Haemosu alikua na rafiki yake ambaye ni prince wa taifa la puyol prnce geumwa (kikorea kumwa). Rafiki huyu ndio anaeleta wazo la haemosu kujiunga na puyol kupigana na han empire
 
Kuna mwamba alitakiwa kuuwawa sasa wakati anaenda mbele kukatwa kichwa. Alitoa kakichupa kamoja ikumbi wote wakaanza kutombana. Nini kilipelekea iwe vile na nini hasa ujumbe wake kwa Hadhira?
 
Unahisi pengine sosunho asingeamua kuondoka goguryeo na watoto wake 2, jumong angewezaje kuchagua crown prince kati ya mtoto wake na wale wengine 2 wa sosunho?

Cc: adriz
nadhani walifanya vile kwasababu ya movie tu iliwalete story ya baikije lakin kwa maon yang hata angebaki jumong angeweza kumchagua aliefaa kuna kipande jumong alisema alishapitia ushindani wa crown prince hilo jambo analielewa na atafanya uamzi sahihi ila sosunho hakutaka maana mtoto wake alishajarib kumuua jumong kwa hila za shangazi yake
 
Kuna mwamba alitakiwa kuuwawa sasa wakati anaenda mbele kukatwa kichwa. Alitoa kakichupa kamoja ikumbi wote wakaanza kutombana. Nini kilipelekea iwe vile na nini hasa ujumbe wake kwa Hadhira
sikumbuki kipande kama iko maana kweny movie ya spatacus uchawi sio moja ya ujumbe uliopo
 
Kuna mwamba alitakiwa kuuwawa sasa wakati anaenda mbele kukatwa kichwa. Alitoa kakichupa kamoja ikumbi wote wakaanza kutombana. Nini kilipelekea iwe vile na nini hasa ujumbe wake kwa Hadhira?
Hii ni movie tofauti, nadhani inaitwa perfume
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom