Wapi hapa Tanzania yanalimwa matunda ya kiwi?

abaa4all

JF-Expert Member
Mar 5, 2013
313
290
Habari wanajamvi

Anayejua wapi yanalimwa matunda ya kiwi kwa hapa Tanzania nayahitaji sana.

kiwi-fruit_625x350_81445871711.jpg

Ahsanteni
 
Mkuu hayo matunda huwa yapo supermarkets tu nadhani huwa ni imported kama upo dar nenda shoppers na game pia nimeshayaona
 
Hakika ila tungepata mazao mengi
Najua
Wenzetu wanatuletea mbegu na kuondoka na mbegu
Unajua maembe sio zao letu yalitoka India pamoja na mchele?
Hata miwa walileta wahindi
Na Tende waarabu
Lakini wao wameondoka pia na mbegu nyingi sana na hata maua na wanyama na wadudu wenye faida na wengine wamewekwa kwenye Zoo kwa kuwaingizia kipato
 
Sisi tatizo tunawaza pafupi ndiyo tatizo letu. Ndo maana hatujiongezi kwenye vitu vingi
 
Mkuu haya matunda KIWI FRUITS asili yake ni CHINA na huko yanajulikana kama "Chinese goosebery". Miaka ya 1700s yalianza kulimwa nchini NEW ZEALAND na kubadilishwa jina na kuitwa KIWI FRUITS ili kuyapa umaarufu ili yajulikane kuwa yanatoka New Zealand.

Matunda haya yaliitwa Kiwi kutokana na ndege maarufu wa huko New Zealand ambaye ndiye alama ya Taifa la nchi hiyo. Manyoya ya ndege huyu(Kiwi Bird) yanafanana sana na jinsi tunda hili lilivyo kwa nje. Hapa Tanzania sidhani kama kuna mahali yanalimwa.
kiwi bird.PNG
kiwi fruit.PNG
 
Hayo matunda mengi yanatoka South Africa, bei yake ipo juu sana sijui kwanini.
 
Mkuu haya matunda KIWI FRUITS asili yake ni CHINA na huko yanajulikana kama "Chinese goosebery". Miaka ya 1700s yalianza kulimwa nchini NEW ZEALAND na kubadilishwa jina na kuitwa KIWI FRUITS ili kuyapa umaarufu ili yajulikane kuwa yanatoka New Zealand.

Matunda haya yaliitwa Kiwi kutokana na ndege maarufu wa huko New Zealand ambaye ndiye alama ya Taifa la nchi hiyo. Manyoya ya ndege huyu(Kiwi Bird) yanafanana sana na jinsi tunda hili lilivyo kwa nje. Hapa Tanzania sidhani kama kuna mahali yanalimwa.
View attachment 818723 View attachment 818727
Inategemea na hali ya hewa ya sehemu
Kama New Zealand wamepanda yakaota nafikikiri na sisi tukipata wataalamu wakajaribu kwa udongo tofauti jibu litapatikana tu
 
Hayo matunda ni Complicatade sana yanalimwa nchi za Ulaya kwa wingi na mengi yanayo uzwa Tanzania yanatokea Italy.

Haya matunda kwanza mbegu zake Ku germinate sio mchezo. Nina mbegu zake nimejaribu hadi nimeacha.

Pia yanaanza kutoa matunda after 3 to 4 years.

Na unaweza lima yote yakawa madume na yasiotoe tunda hata 1
 
Tanzania hailimwi hii!
Kwa kenya ndiyo wa najaribu kuilima

Ova
 
Halafu New Zealand nao wakalima
Huenda yanaweza ota hata kwetu
Yaani tungekuwa kila tunapokwenda unarudi na mbegu za aina fulani tungekuwa tuna kila kitu kwa kweli
Mkuu, kumbe wewe ni wa siku nyingi humu JF😀👏

Siku ukirudi Tz uje na mbegu ya huko ughaibuni🙏
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom