Wapewa talaka kwa kuunga mkono CCM Zanzibar

Wapewa talaka kwa kuunga mkono CCM Zanzibar

Msolid1990

Senior Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
144
Reaction score
51
Takriban wanawake 14 kutoka kisiwani Zanzibar nchini Tanzania wanaotuhumiwa kukiunga mkono chama tawala cha mapinduzi CCM katika uchaguzi uliopita kinyume na matakwa ya waume zao wamepewa talaka.

Kulingana na gazeti la Zanzibar daily Newspaper. Watalakiwa hao wamesema kuwa wanaume zao waliamua kuwapatia talaka nyakati tofauti kutokana na tofauti za kisiasa kwa mujibu wa gazeti hilo.

Limeongezea kwamba wanaharakati kutoka kwa muungano wa mawakili wanawake kisiwani pamoja na muungano wa wanahabari wa kike nchini Tanzania wamesikia kuhusu visa kama hivyo na wameahidi kufuatilia swala hilo.

Chanzo:
BBC Swahili
 
Huku ccm kuna watu tunahitaji wachumba.
Waleteeeee....
 
ni uwendawazimu uliopitiliza
"Political extremists"
 
Mbona na Mtwara pia ni hivyo hivyo. Tena huko ukiwa CUF unaambiwa ukienda sokoni usinunue bidhaa kwa CCM. Haijaenea sana lakini imeanza kujitokeza.
 
Hata kama wangeunga mkono ukawa, ktk uislamu hakuna siasa za aina hiyo, ufxad,uwendawazmu, uchwara na upumbavu, watajiju wakaolewe na MAGUFULI AU SHEIN
 
mimi nisingekubali kuacha mke aiseee kwa ajili ya siasa. yaani niiache ile kitu hivi hivi iende kwa ajili ya siasa! awapi!
bila shaka hao walikuwa wanatafuta visababu tu na sio vinginevyo.
 
  • Thanks
Reactions: nao
11147210_920246028067551_4226195459736501981_n.jpg
 
Ni sawa tu imeandikwa 'enyi wanawake watiini waume zenu.... kama hakuna.utiio timualia mbali....
 
Huwezi kuishi na mtu ambaye interest zipo tofauti. Hahaaaa
 
Ha ha haaaa!, wakadai "HAKI SAWA" kwa Magufuri wauone moto wake. Miaka mitano ijayo tusahau swala la haki sawa magufuri hawezi kukubali haki sawa na mwanamke. Ha ha haaaaaa!. Poleni sana waachwa, CCM mbele kwa mbele imeanza kufanya kazi kwa upande wenu tayari
 
Wako sawa mwanaume ni kichwa cha familiya kama hawakuwaelewa waume zao walitegemea nini?Hata mie kimada changu nilikitupilia mbali kwa kujifanya kinapenda ccm.
 
Back
Top Bottom