Kimbley
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 3,050
- 2,103
Mi mgeni kwenye jukwaa lenu wapendwa ila limenivutia sana nikaona si mbaya kama nitashare nanyi ujuzi na kupata mawazo mapya kuhusu mapishi mbali mbali.
Leo wapenzi ningependa muonje uji wa tangawizi mbichi niliouandaa na mahitaji ni kama ifautavyo;
1.Unga wa ulezi wa mchanganyiko mbalimbali,dona au unga wowote uupendao kwa uji.
2.Maziwa 1/2 ya maji.
3.Sukari/asali
4.Tangawizi mbichi iliyosagwa kijiko kimoja cha chakula.
5.Maji.
6.Siagi kijiko kimoja cha chakula.
JINSI YA KUPIKA:
-Weka maji katika sufuria yako 1Litre na nusu.
-Weka tangawizi iliyosagwa kwenye maji,unaweza ukachuja tangawizi ili kuondoa makapi kama hupendi kuyasikia wakati unakunywa uji.
-Tia unga vijiko saba vya chakula kabla mji hayapata moto ili kuepuka mabuja katika uji wako huku ukiendelea kukoroga.
-Ongeza maziwa yaliyochemshwa kwenye uji wako
-Tia sukari uipendayo/asali kwenye uji wako.
-Endelea kukoroga na uache jikoni kwa dk15.
-Epua na tenga mezani kwa ajili ya wanywaji.
KUMBUKA;Kama unatumia uji wa ulezi hakikisha uji umeiva ndipo uongeze maziwa yaliyochemshwa.
Uji huu unanywewa na watu wazima na watoto kama wanatumia tangawizi.
KARIBUNI
Ccfakhrina mshana jr MziziMkavu na wengine wengii.