Wapenzi wa push-ups & squats

sabuwanka

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
690
751
Salaam wakuu na hongereni kwa kushiriki vita ya kuitokomeza corona

Katika kuweka mwili fiti nimeona Kuna mazoezi mawili yasiyohitaji eneo kubwa, na hata chumbani unaweza kuyafanya, nayo Ni pushups kwa kujenga mwonekano wa juu wa mwili , na squarts kwa kujenga mwonekano wa chini wa mwili

Wapenzi wa mazoezi hayo karibuni mtuambie ulianzaje kupiga push-ups na unamudu kupiga pushups ngapi, squats ngapi na utimamu wa mwili wako ukoje.

Karibuni
 
Push-up huwa napiga kila siku 140 , asubuhi 70
(jioni)usiku 70

Na push up za nyuma 50,
na hiki kifaa pia natumia ktk mazoez ili kujiweka mwili sawa.
1591957548336.jpg
 
Hahahah shadee una haraka kama cha kwqnza..
We nieleweshe bana sababu na mie pia ni mfanyaji mazoezi mzuri tu japo Push - ups kwangu huwa ni changamoto yaani siziwezi kabisaa labda nikite mikono na miguu chini ila si kupanda na kushuka sana sana nikishuka naeza shusha kiuno lakini mgongo na kichwa vikawa juu basi na si kushuka na kupandisha mwili mzima :D:D:D
 
Anza kidogo kidogo, mie nilikuwa sizidishi push-ups tatu...nikaendelea bila kukata tamaa sasa naendelea vizuri na napiga nyingi tu
 
Push up Ni zoezi zuri...

Anza pale ulipo...halafu Hakikisha unajichalenge mwenyewe kila siku..

Mfano leo ukipiga tano.. kesho piga Saba, keshokutwa 8,

Hakikisha unaizidi Jana...

Utakaa sawa TU...
Mimi nilianza na Saba....
Ila Sasa nakimbiza 50+ mzunguuko mmoja
 
Back
Top Bottom