Trubetzkoy
JF-Expert Member
- Oct 31, 2018
- 298
- 542
Habari za wakati huu mabibi na mabwana!
Leo ikiwa ni siku ya kumi tangu tulipouanza
mwaka 2022 naomba msaada wa mawazo yenu ambayo kwa namna ya pekee naweza kuyatumia kama njia ya kuelekea kufanikisha malengo niliyojiwekea kwa mwaka huu wa 2022.
Mimi ni mwandishi mchanga/chipukizi. Nina uwezo na kipaji cha kutunga na kuandika vitabu pamoja na makala zinazohusu masuala mbalimbali ya kijamii. Uwezo na kipaji changu vimedhihirika tangu nikiwa chuoni 2016--2019.
Ndoto zangu zikiwa ni kuwa mwandishi nguli huku role model wangu akiwa ni Late Prof Euphrase Kezilahabi, nimeona ni vema nijieleze humu ili nipate mawazo yenu huku nikiamini kuwa hili ni jukwaa ambalo msaada wa aina yoyote unaweza kupatikana.
Lengo la uzi huu ni kuomba kufahamishwa juu ya hatua ninazopaswa kuzichukua pindi nimalizapo kuandika muswada wa kitabu ikiwa ni pamoja na namna ya kupata muhariri, wachapishaji mpaka kufikia hatua ya kuingiza kitabu sokoni.
Naomba nipewe elimu ili kipaji changu kisipotee.
Nawasilisha.