Nimesukumiwa kesi na rafiki yangu wa karibu nikashindwa kuitolea suluhisho ndipo nimeamua niiweke humu jamvini tupeane mawazo. Alinitaarifu kuwa nyumbani kwake moto unawaka ana muda wa mwezi sasa hajapata unyumba kisa yeye binafsi hataki kuoga na mkewe. Anasema toka wameoana yapata miaka mitatu iliopita hawakuwa na huo utaratibu.
Lakini ghafla kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu mkewe anataka wawe wanaoga wote kitu ambacho yeye hakiafiki kabisa, kikubwa ni kuwa hana sababu ya msingi ya kukataa zaidi ya kudai kuwa yeye hajazoea na hataki hilo jambo.
Sasa naombeni wadau mnipe mawazo ambayo yanaweza kumsaidia huyu bwana ili akubaliane na hiyo hoja ya mkewe na hatimaye apewe tena unyumba kwa faida yake mwenyewe. Kwa wale wajuzi wa haya mambo labda ingesaidia pia kama mtatuwekea uzuri na ubaya wa hili jambo kwa wanandoa au wapenzi.
Sasa kama yeye keshakataa kuoga nae unataka ushauri gani tena? Kama kashindwa kumsikiliza mkewe anayempa unyumba sisi watu ambao hata hatujui atatuelewa na ushauri wetu?
Sasa kama hana sababu za msingi kukataa hilo kwanini akatae? Kuna ugumu gani ingali wanachunguliana na kukutanisha vikojoleo miaka yote!? Ataanzaje kuzoea hali hiyo ikiwa hataki tena bila sababu za msingi?
Kama anaipenda ndoa yake mwambie abadilike kabla hajasaidiwa kazi waziwazi
Huo muda wa kusubiriana kuoga pamoja uko wapi? Halafu ili iweje? Naona kama unakuwa yu usanii. Badala ya kufikiria ya msingi wanawaza kuoga pamoja hahaha. Dah shida tuuupuu
Hapo jamaa alijurupuka kuoa, hana yale mapenzi ya dhati kwa mkewe, huwenda ata sehemu ya siri ya mkewe hajui inafananaje, pia nahisi sababu nyingine jamaa anaona aibu wakati akiinama mkewe atamchungulia huko nyuma.
Miaka mitatu hawajawahi kuoga pamoja ghafla mamaa anahitaji waoge pamoja lazima kuna mtu alioga nawe akaonja raha ya kuoga na mwanaume chezea unasomea nje field unafanyia nyumbani
Labda niulize, wakiwa wanado....huwa wanazima taa pia? Km hawez kuoga na mkewe inamaana ktk hiyo miaka mi3 sidhani km waliwahi ku-do na mwanga.
Mpeni ushauri, ni psychological issue ndogo tu na anaweza kubadilika.