Maombi au sala kama hiyo ilikuwa sahihi wakati wa Agano la Kale. Wakati huu wa Agano Jipya sio sahihi kwa Mkristo kuomba kama mwandishi wa Zaburi 109 alivyoomba. Hiyo ni sala ya laana (imprecatory psalm). Mwandishi wa Zaburi hiyo aliomba Mungu awaadhibu vikali adui zake.
Yesu Kristo alituletea Agano Jipya. Ndio sababu Yesu na mitume wake walifundisha mtazamo tofauti juu ya adui.
Yesu anatufundisha kuwapenda adui zetu. Kwa mantiki hiyo alibadilisha mtazamo wa kulipiza kisasi kwa kuhimiza upendo na msamaha:
Mathayo 5:44 –
“Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.”
Katika Agano Jipya, Paulo anatuhimiza pia kuwabariki hata wale wanaotutesa badala ya kuwaombea mabaya:
Warumi 12:14 –
“Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msiwalaani.”
Katika Agano Jipya tunatakiwa kumwachia Mungu. Yeye ndiye atakayelipa kisasi:
Warumi 12:19 –
"Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.”
Hata Yesu aliwasamehe waliomtesa. Alipokuwa msalabani, hakuwalaani watesi wake kama katika Zaburi 109, bali aliomba Mungu awasamehe:
Luka 23:34 –
“Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.”
Zaburi ya 109 inatufundisha tu jinsi zamani ilivyokuwa sawa kumuombea adui mabaya. Lakini kwa sasa tunafuata mafundisho mapya ya msamaha, upendo, na kuwaombea baraka maadui zetu. Kwahiyo,
usiitumie Zaburi hiyo kama mwongozo wa sala yako. Ukisali au ukiomba hivyo utakuwa unaomba kinyume na mapenzi ya Mungu, na kwa sababu hiyo maombi hayo hayatajibiwa.
Mpaka hapo naamini
Mwanamke wa mithali 31 amepata jibu sahihi.