Starwars91
Member
- Jul 12, 2020
- 52
- 47
Mimi ni mkatoliki. Kuna kwaya huwa inanikosha sana hapa Tanzania. Ni kwaya ya mtakatifu kizito parokia ya mtakatifu mwenye heri anuarite iliyoko makuburi Dar es salaam. Kwa kweli ni kwaya ambayo inaimba vizuri sana. Ikiongozwa na mwandishi machachari Wa nyimbo za ki injili za kikatoliki bwana Bernard Mukasa. Jaman kwa wale wakatoliki nahisi wanaifahamu hiii kwaya. Hata wale wasio wakatoliki wanaweza kuwa washawahi kusikia nyimbo zao nzuri na tamu sana. Nyimbo yao bora zaidi ambayo imeweza kupenya mpaka nje ya mipaka ya Tanzania inaitwa "mimina" wanazo pia nyingine nzuri nyingi tu. "Nyota ya mashariki", " wewe ni mungu" , "nusu kwa nusu", " Mungu ni upendo" , "mwanzi uliopondeka" ya kwake Bernard mukasa mwenyewe. Kwa kweli inapendeza sana. Ingawaje ninapenda waimbaji hawa, lakin nyimbo zangu mbili bora za kikatoliki ni "bwana unibadili" ilioimbwa na kwaya ya mtakatifu maria Goreti chuo kikuu cha ushirika moshi na "mbingu zilifunguka" ilioimbwa na kwaya ya parokia ya korogwe ilioko Tanga. Kongole kwa waimbaji hawa. Wapenzi mnaweza kuziangalia katika YouTube. Jumapili njema kwenu watanzania wote.