Wapemba ni watu gani?

Twambieni Malenga, Wapemba ni watu gani,
Mmeishusha nidhamu, kuwatangaza wageni,
Kumbe wao Wazaramo, walohamia zamani,
Malenga twambieni, Wapemba ni watu gani?

Pemba mahali hadhimu, kapabariki Manani,
Pana mazao muhimu, tele tele mashambani,
Nayo matunda matamu, vile vile yapo ndani,
Malenga twambieni, Wapemba ni watu gani?

Mmanyema yupo humu, kahamia kisiwani,
Mnyamwezi mfahamu, yupo Pemba vijijini,
Kabila zote za humu, wapo huko visiwani,
Malenga twambieni, Wapemba ni watu gani?

Zanzibar si adimu, wapo pia visiwani,
Hatuwezi kulaumu, ndugu zetu kwa yakini,
Makanisa yamo humu, kuabudu zao dini,
Malenga twambieni, Wapemba ni watu gani?

Sote tunakufahamu, atokako Dr Salim Ahmed Salim,
Dr. Shein Makamu, ametoka nchi gani?
Wamevua umuhimu, ili akae kitini,
Malenga twambieni, Wapemba ni watu gani?

Tunajua mahalumu, wapo tokea zamani,
Kwani twawafahamu, kuwa wao si wageni,
Bure mnakituhumu, ni kisiwa cha udini,
Malenga twambieni, Wapemba ni watu gani?

Naiachia kalamu, taratibu JF Javini,
Kina Brain Power muadhamu, na Mwanakiji Tutani,
Bubu Atakusema mtaalam, wa JF Humu Ndani,
Malenga twambieni, Wapemba ni watu gani?

Ni waafrika wanaokataa uafrika wao!!..wanasema wao ni waarabu! hivyo ni bora kuliko waafrika!..wewe kama unabisha jaribu kufuatilia ni wapi mpemba aliusifu uafrika wake..woote utawasikia sijui dubai..sijuia oman sijui...saudi
Kazi kweli bado tunayo wandugu! sijui ni lini waafrika tutaelimika na kujiheshimu jinsi tulivyo na siyo kujifananisha na watu wa mabara mengine...
 
Nilishawahi kusikia mmoja akijitapa mimi babu yangu alitoka Oman unaona hata nywele zangu zilivyo za shombe shombe!!!! :confused: nikamkata jicho la kiutu uzima lakini si kutia neno :) Wanapenda sana kujibabatiza na kuunga na gundi uarabu wasiokuwa nao kama vile ukiwa mwarabu wewe ni wa maana sana kuliko Mwafrika.
 
Punguza ghadhabu Mzee. Wapemba ni Wa-Zanzibari . sasa kama babu yake imetokea kuwa ni mtu mwenye asili ya Oman kuna dhambi gani kujitapa kwa asili hiyo. Huo Uafrika unaosema ni upi? U-Naigeria umo humo?
 
basi wapemba- waarabu koko=waarabu pori= WAMANGA, lakini nao huwa wakishuka huko Dubai/Oman sijui Saudia wanaitwa WASWAHILI kwa sababu they dont know anything about arabs and more enough they cant even speak the language they just know greetings and blah blah....
 
Pemba!
 
Attachments

  • DSC_5068[1].JPG
    DSC_5068[1].JPG
    19.4 KB · Views: 83
Last edited:
Nilishawahi kusikia mmoja akijitapa mimi babu yangu alitoka Oman unaona hata nywele zangu zilivyo za shombe shombe!!!! :confused: nikamkata jicho la kiutu uzima lakini si kutia neno :) Wanapenda sana kujibabatiza na kuunga na gundi uarabu wasiokuwa nao kama vile ukiwa mwarabu wewe ni wa maana sana kuliko Mwafrika.

Son:

Mwafrika maana yake sio mtu mweusi. Mwafrika ni mtu anaishi kwenye continent la Afrika. Na ndani ya Afrika kuna watu wenye background tofauti.

Mtu ambaye babu yake ni mwaArabu hiyo ni fact. Je haifiche hiyo fact? hatakiwi kuificha kwa sababu hipo ndani ya DNA yake.

Hila upuuzi wa kuwafanya wengine wapumbavu hautakiwi.
 
basi wapemba- waarabu koko=waarabu pori= WAMANGA, lakini nao huwa wakishuka huko Dubai/Oman sijui Saudia wanaitwa WASWAHILI kwa sababu they dont know anything about arabs and more enough they cant even speak the language they just know greetings and blah blah....

Sawa. Kama ni kutoa ushauri., Nafikiri achana na hisia zote hizo. Wapemba ni Wa Zanzibari.
 
Back
Top Bottom