Wapemba kulazimishwa kupiga kura?

wagagagigi

JF-Expert Member
Dec 9, 2014
890
984
Wana JF, napenda kuwajuza yanayotokea kisiwani Pemba ni kwamb Wafanyakazi wote wa serikali ya SMZ wamelazimishwa kuwasilisha vitambolisho vyao vya kupigia kura kwa wakuu wao wa kazi ili nambari za vitabulisho hivyo zisajiliwe.

wa kweli haijaeleweka lengo la CCM kufanya hayo hasa ni nini, lakini kuna na vitisho kwa asiepeleka kitambulisho chake cha kupigia kura.

Tungewaomba wahusika wakuu wa CUF/UKAWA kufuatilia haya mambo.

Inavyoonekana CCM wanahaha kutaka kuhalalisha haramu yao kwa kila hali.
 
hatimae sintofahamu ya burundi yainyemelea tanganyika
Ni kweli kabisa. Hapa ni swala la watu kuomba MUNGU huyu shetani apishe mbali.

Hii tabia ya nchi za Afrika ya chama kimoja cha siasa kuwa na uwezo na nguvu za kuzuia chama kingine kisiingie madarakani lazima italingamiza bara la Afrika
 
Wana JF, napenda kuwajuza yanayotokea kisiwani Pemba ni kwamb Wafanyakazi wote wa serikali ya SMZ wamelazimishwa kuwasilisha vitambolisho vyao vya kupigia kura kwa wakuu wao wa kazi ili nambari za vitabulisho hivyo zisajiliwe.

.

MLETA MAADA MUONGO HAKUNA KITU KAMA HICHO
 
Ni kweli kabisa. Hapa ni swala la watu kuomba MUNGU huyu shetani apishe mbali.

Hii tabia ya nchi za Afrika ya chama kimoja cha siasa kuwa na uwezo na nguvu za kuzuia chama kingine kisiingie madarakani lazima italingamiza bara la Afrika
Kufumbatia maji Kama jiwe ni ujinga. Sote ni ndugu, watoto wa baba mmoja.. Yanini kugombea fito?? Kwanini watu wanatumia nguvu nyingi kubaki madarakani?? Kuna nini huko ikulu?? Nyerere alisema hata huwezi kusema uweke sturi uuze karanga,, au Ikulu sikuhizi ni tofauti na enzi hizo???
 
Mbona jecha alisema hakuna kampeni wala kusajili upya majina ya wapiga kura, smz pemba kufanya hivyo ni kukiuka maagizo ya jecha, baadae waje wamsingizie jecha kumbe wao ndo wanaovuruga kila kitu, mshaambiwa cuf hawapigi wapige wao sasa wasiwasi wa nini, kweli ninaamini kuwa wao ni chanzo cha vurugu
 
hatimae sintofahamu ya burundi yainyemelea tanganyika
Bwana mdogo huelewi unachoongea.
Wapiga kura wanaoleta figisufigisu wako Zanzibar, na wao hawazidi laki tano.
Laki tano hata hapa Kawe kuna watu wengi zaidi, achilia Da es sakaam ya watu milioni tano!

Na hao laki tano wakiongozwa na CUF wanapiga kelele utafikiria nchi nzima, na wanawapata watu msiojua kama wewe!
Na lazima uelewe kuwa hao watu, HAWAKO Tanganyika!
 
Serikali kushawishi watumishi wake kupiga kura si dhambi kama ilivyo si dhambi CUF kushawishi wafuasi wake kutopiga kura.
 
Serikali kushawishi watumishi wake kupiga kura si dhambi kama ilivyo si dhambi CUF kushawishi wafuasi wake kutopiga kura.
Watu kama nyinyi wenye akili ndogo ndio mnao sababisha watanzania kuwa masikini,hivi unajua maana ya serekali na chama?
 
Serikali kushawishi watumishi wake kupiga kura si dhambi kama ilivyo si dhambi CUF kushawishi wafuasi wake kutopiga kura.
mkuu umefananisha vitu viwili TOFAUTI, Unafananisha Wafuasi(vyama) na watumishi(serikali).ungekuwa sahihi kama ungesema "CCM kushawishi wafuasi wake kupiga kura si dhambi kama ilivyo si dhambi kwa CUF kushawishi wafuasi wake kutopiga kura". variables ulizotumia hazina correlation kabisa na kama ungepima null hypothesis yako basi nina hakika ingekataa.
 
Usilazimishe unalowaza wewe ndio niseme Mimi! Serikal ipo sahihi kushawishi Watumishi kwa kuwa Msimamo wa tume ni msimamo wa Serikal
 
Back
Top Bottom