Strong25
JF-Expert Member
- Dec 6, 2021
- 426
- 912
- Thread starter
- #81
Ni ukweli ambao mgumu kueleweka ni hivi Waganga hawana uwezo wa kukupa utajiri ingekuwa hivyo koo zao zingejaa wakina Bhakhresa.Uganga ni ujanja ujanja tu wa watu fulani ambao hunufaika jamii ya watu wavivu i mean wapenda short cut,Wasiojielewa i mean hawajajikomboa kiakili.Unakuta mtu anaibiwa kiasi cha milioni moja then anakimbilia kwa mganga kuzitafuta badala ya kwenda polisi.Sasa kama waganga wanaweza kumdhuru au kumfanya arudishe hela basi kampuni zisingekuwa zinatangaza donge nono kwenye magazeti kumtafuta mtu alietokomea na mil 50 badala yake kwenye kila kampuni kungekuwepo muajiriwa kitengo cha mganga wa kienyeji ili apige Lamli kwenye kila tukio lisiloeleweka litakalotokea kwenye kampuni kama ikivyo mhasibu anavyowajibika na mambo yote yahusuyo fedha.Mimi nimekaa na babu yangu mganga wa kienyeji tumekula sana mi mbuzi,na mikuku ya majitu majinga na mengine ni ma viongozi makubwa tu serikalini ambapo babu yangu anayavisha mashuka meusi anayaogesha madawa ya mizizi kutoka porini.
YAANI NILICHOKUJA KUGUNDUA WAGANGA INCLUDE BABU YANGU wanacheza na kichwa chako unakuja na fikila zako kuwa mfanya kazi mwenzako mliogombana nae ndo huyo anaitwa mchawi wako unapewa dawa za uongo na kaushauri mwisho wa siku linaisha pito unalopitia unahisi mafekeche yamefanya kazi.WAGANGA WANA SAIL KWENYE ISSUE YA KUFANANISHA MATUKIO AU MATOKEO CHANYA UNAYOTEGEMEA NA STORI ZA VIJIWENI.Mfano pale kwa babu wateja wake wengi ni wachimba madini babu alivyo mjanja ametegesha masela wenye ushawishi kule mgodini wanashawishi watu waje kwa babu kwa kubaliano la gawio yaani mchezo unachezwa hivi shimo lolote litakalo tema dhahabu wale masela wanaiunganisha ile story kuwa Jamaa mwenye shimo lililotema alishawahi kumpeleka kwa babu ndo matokeo ya shimo kutema na wanaongezea kuwa hiyo siri mwenye shimo hawezi kukuambia hata kama ukienda kumuuliza.So ukienda kumhoji mwenye shimo akikana na ukarudi wanakuambia hawezi kukuambia siri ya mtaalam wake.SO UCHAWI NA UGANGA NA HATA MAMBO YA KILOKOLE,ALBADILI ni ujinga ambao haupo ila unakuzwa kwa promo za vijiweni na kusambazwa na wajinga.Asanteni
Bado huyajui maisha ww