- Thread starter
- #41
Nyundo2017Mfumo wa mafunzo ubadilishwe na uwe wa kiujuzi na kinkakati katika kutokomeza rushwa na kuwe na uhuru kama ilivyo ktk nchi nyingine siyo ubabe ndani na nje ya taasisi.
Niwazi bado mafunzo yao siyo yabkimkakati kwani ni semina tu ya miezi 3 kwa mtu mwenye shahada yoyote ile iwe kilimo,uchumi,maktaba,sayansi ya jamii,n.k ambapo hujifunza partial marshal art kwaajili ya self defence na baadhi ya sheria na walimu wakiwa maboss wao au watangulizi wao na baadhi ya wakufunzi waalikwa kutoka polisi,mahakama,nk na ndito maana wanatoka nje ya majukumu yao.
Ndani ya hito course wanajifunza za pcca,cpa,tea,eoca na pc juu tu siyo kwa undani kwa hiyo miezi mitatu pasipo kujifunza masomo mengine yahusuyo RUSHWA na UCHUNGUZI.
Baada ya hapo eti watu wanakuwa wamehitimu tayari kupambana rushwa,kweli?
Haya baada ya miaka kama kumi kazini wanaenda semina ya senior ambao sasa hawa ndiyo wanachaguliwa kuwa dbcs,agrbcs,rbcs,directors,nk kwa fadhira za DG siyo kwa sababu ya elimu ya rushwa na ubobezi ktk maswala ya uchunguzi.
Haya hao watu unawaingiza mtaani na shahada zao na hiyo BIC wakachunguze na kupambana na rushwa kwa kupokea taarifa tu na siyo ujuzi.
Je huyo mtu atatenda miujiza ndani ya taasisi au nje ya taasisi katika kupambana na rushwa au utamlinganisha na polisi aliyepitia mafunzo na hatua mbalimbali ya uingozi?
Tukubali kubadilika takukuru hamna weredi na fairness zaidi ya ubabe na kuogopwa kwa fikira tu humo ndani kuna viongozi viraza kweli ambao wapo kulinda maslahi yao kwa kumpotosha kila DG ajae kwa kumlisha matango pori na kuwachongea subornates wenye vipaji pamoja na mwenda zake kuwaondoa baadhi yao na kuwapeleka taasisi nyinginezo mmoja wao akiwa aliyekuwa AgDPP.
Polisi wakisimamiwa wanaweza kabisa kutokomeza rushwa siyo kwa hii takukuru kupambana na rushwa siyo degree/master/phd, majengo,idadi kubwa ya watumishi,upendeleo na magari bali WEREDI
Viongozi wa takukuru wengi wanalipiana fedha za serikali kusomea elimu za juu vyuoni i.e pgraduate,masters,degree,phd badala ya kuwaandaa watu wa kada ya chini kwa kuwapa elimu nzuri zenye msingi ktk maswala ya kupambana na rushwa kwa kuanzia chini hadi juu.
Hivi kweli mtu mwenye shahada ya maktaba na hizo semina za bic na uandamizi anapewa mkoa au wilaya eti atokomeze rushwa bila nyongeza yoyote ya ujuzi wa uchunguzi wa maswala ya rushwa kunaweza kuleta tija?
TUTAFAKARI!!!!
Kwa kweli umeliweka kwa kina jambo hili. TAKUKURU inakosa mashiko na misingi ya kitaaluma ya mapambano ya Rushwa.
Wako pia wafagia ofisi na wahudumu. Wakipata degree wanakuwa wachunguzi automatically bila taalumu nyingine.
Nakumbuka Kuna wakati walikuwa na mkakati wa kujenga chuo chao cha mafunzo. Sijui likiishia wapi wazo hili