Habari wadau, wap naweza pata computer ya mkono yaan laptops aina ya LENOVO THINKPAD T490S AU LENOVO THINKPAD L390 AU LENOVO THINKPAD X kwa hapa Tanzania??
Nataka iwe mpya.....pia laptop ipi inakarbiana na hizo lenovo thinkpad ....the millitary machine.
Kuna laptop City. Wapo Morocco BRT Terminal.
Niliona wana T480 na X1 carbon Gen 7. Sijui kma watakua na t490s or newer models.
Pia kuna ile shop ya mhindi ipo pale Mcity. Wanakuaga na Thinkpad. Ila kupata models mpya huku bongo ni kazi aisee. Nyingi ni kuanzia T480 kushuka chini. Au X1 carbon gen 7 kwenda chini.
kwa Tanzania thinkpad zimejaa sana, sidhani kama kuna model utaikosa.
na kwa ushauri wangu usipoteze hela kununua gen ya 8 ama 9 mpya sasa hivi cpu za gen ya 11 zikianza tu kuingia mtaani tutaanza kuzipata kwa bei chee hizi za 8 na 9, kama una hela yako tunza subiria gen ya 11, ama kama una haraka sana hata gen ya 10 ice lake si mbaya.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.