Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 10,884
- 18,824
CHUI
KATIKA wanyama wote wanaomshabihi paka hapa Afrika hakuna aliye mkubwa kuliko chui ila simba tu. Urefu wake, chui, toka pua yake mpaka ncha ya mkia wake wapata futi saba na uzito wake ni kama ratili mia na hamsini.Anajulikana kwa ajili ya uzuri wa ngozi yake yenye madoa meusi.
Madoa haya siyo ya uzuri tu, yanamsaidia ajifiche vizuri, maana rangi yake inafanana kabisa na rangi ya miamba na mwitu anapokaa, hata ni shida kwa adui kupata kumwona.
Chui ana njia nyingi za kujilinda. Meno yake ni makali na yenye nguvu, hata na makucha yake pia. Kwa hiyo ni fundi wa kupigana. Makucha yake yanafanana na yale ya paka wetu wa nyumbani. Aweza kuficha makucha ndani ya miguu, basi ni makali siku zote, siyo kama yale ya mbwa ambaye hawezi kuyaficha.
Chui anajilinda kwa kuwinda usiku. Mchana hujificha kwenye pango lake. Anaweza kuona vizuri gizani kama sisi tunavyoweza kuona vizuri kwenye mwangaza. Miguu yake ina nyama laini chini apate kutembea pasipo kelele; yule mnyama ambaye anamfuata hajui kwamba chui yu karibu mpaka amemrukia. Huweza kupanda juu ya miti na makucha yake makali yanamsaidia kushika miti kwa nguvu wakati anapojikokota juu na kupita mpaka mwisho wa matawi makubwa. Mwendo wake ni mwepesi sana ingawa ni mnyama mkubwa na mnene. Ajua kuruka upesi akiona hatari na pia kuruka ghafula akitaka kukamata mawindo yake. Wakati anapowindwa mwenyewe anajiokoa kwa kupiga mbio na kuruka juu ya mti.
Labda ni sababu hizi zote zilizo zimemsaidia chui asifukuzwe mbali ya miji na kukaa msituni tu kama wanyama wote wengine. Zamani za kale wanyama wote walitembea ovyo huko na huko katika kontinenti zima la Afrika na chui walionekana kusini hata pande za Cape of Good Hope. Lakini
Fisi
binadamu alipoanza kujenga miji nikubwa na kufanya vita na wanyama wakali, wao, walilazimishwa kuondoka na kwenda kukaa katika milima na misitu na nyika na majangwa na kila mahali palipokuwa hakuna watu. Lakini hata leo chui hupenda kukaa katika
Mbweha
milima inayopakana na miji iliyo mikubwa kabisa.
Chui ni adui mkuu wa binadamu ambaye anafuga wanyama maana chakula kinachompendeza chui ni nyama ya kondoo au ya mbuzi au ya ndama wa ng'ombe. Kwa kawaida anajificha katika vilima na miamba na mikoko karibu ya mashamba ya mfugaji akingoja giza la usiku na hata mvua. Ndipo anapotoka na kujikokota polepole mpaka kwenye zizi.
Palahala Mweusi
Huingia na kuwaua mbuzi na kondoo wengi awezavyo kwa furaha ya uuaji tu. Mwenye zizi anapokuja asubuhi ataona wanyama wengi wameuawa; akitazama nyayo zilizopo chini atatambua kwamba chui amemchukua mnyama mmoja tu apate kushiba kwa siri. Pengine anapanda mtini akichukua mzoga wa mnyama, maana chui anazo nguvu zakutosha achukue
Wibari
kondoo mzima katika meno yake. Akipeleka chakula chake juu anajua hakika kwamba hataibiwa na mnyama mwingine. Fisi na mbwa mwitu wanapenda sana mawindo ya chui. Yeye, chui, pia ni mwizi; anapenda kula nyama anayoikuta njiani, hata hakatai ikiwa imeoza kwa kukaa kwenye jua kali.
Sio wanyama waliofugwa tu wanaompendeza chui; anatumia pia paa na vinyama vidogo kama wibari na sungura. Mara nyingi hukamata ndege kama kanga wakikaa juu ya miti au kuja kutafuta maji jioni kisimani. Akiona njaa asiweze kuona kitu bora aweza kujishibisha na vyura wanaokaa katika maziwa ya maji ya mvua. Haingii kwenye maji; vyura ni wajinga, nao hurukaruka katika ukingo wa ziwa na pale chui huwakamata upesi hapendi kujitia mtoni lakini, akiona ni lazima yu hodari wa kuogelea.
Sungura
Tumbili wote wanamwogopa chui maana yeye ndiye adui wao mkuu. Nyani na tumbili hutembea kwa makundi na wakimwona chui anawajia wanamrukia wote pamoja na kumwua. Lakini chui akimfikia tumbili mmoja peke yake anajikokota polepole apate kumrukia ghafula. Anamshika kwa nguvu na kumwuma shingo kusudi asitoe sauti ya kuwaita wenzake kuja kumsaidia. Kundi la nyani wakiona uuaji wa namna hii watamshambulia chui na kumlazimisha aache mawindo
Kanga
yake na hata watamwua.
Chui anawinda kwa busara nyingi. Pengine hujilaza katika matawi ya mti na kumngoja mnyama apite chini yake; hivyo humrukia upesi na kumkamata. Mara akiisha kumkamata mnyama anampasua tumboni na kumtoa matumbo. Anakula haya kwanza, mzoga anauficha kwa siku nyingine. Ikiwa amewinda vizuri na kushiba anatoa mlio wa ngurumo Hu-hu-hu-ho ' anaposhika njia kwenda kunywa maji kisimani; kisha hurudia kwenye pango lake apate kulala wakati wa hari ya jua kali.
Chui jike akijiweka tayari kuzaa watoto hujitafutia mahali paliposetirika vizuri, hata ni shida kwa binadamu kupata kuwaona watoto wachanga wa chui. Kwa kawaida wanazaliwa watoto wawili pamoja, na mara kwa mara watatu au hata wanne, hata pengine ni mmoja peke yake tu. Juma ya kwanza watoto ni dhaifu sana na mama yao huwaficha nyumbani. Usiku hutoka nje awatafutie chakula. Yeye ni mama mzuri. Akiona hatari atawapigania watoto wake. Wakianza kukua huwatokeza nje akawafundisha kuwinda wenyewe na kujipatia chakula. Akawaonyesha jinsi ya kujificha karibu ya kisima na kuwangoja
Dondoro
paa wajapo kunywa maji alfajiri, tena jinsi ya kujilaza kimya katika matawi; jinsi ya kupanda juu na kumrukia mnyama ghafula pasipo kelele na kumwuma shingoni. Watoto wa chui wanajifunza haya yote upesi maana wanyama wakali wote hawachelewi kujifunza kazi zao; baada ya siku si nyingi wanajua kujiangalia wenyewe.
Binadamu wenye kazi ya kuwinda wanyama wanamtambua chui kuwa adui mbaya kwa sababu ana busara nyingi na nguvu nyingi, tena ni kimya kabisa. Akiumizwa anajificha na kumngoja yule aliyempiga, naye anapokaribia chui anamrukia upesi. Mtu yule hajajua kwamba chui yupo, chui anaruka asipotazamiwa, basi ni shida mtu kupata kuokoka. Kwa hiyo ni ujinga kumfuata chui aliyejeruhiwa, zaidi akiingia kwenye msitu au katikati ya miamba.
Mbwa wakimwendea chui aliyeumizwa anajilaza chali apate kutumia makucha yake yote na meno yake pia. Kwa kuwa makucha yake ni makali kama visu, naye ni mwepesi sana katika kupigana, mara nyingi mbwa huumizwa vibaya na hata kuuawa.