- Source #1
- View Source #1
Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa zinazosema kiongozi mkuu mpya wa Iran Bwana Alireza Arafi ameuwawa.
Ngoja tusubiri tuone kama itakuwa ni kweli.
Ngoja tusubiri tuone kama itakuwa ni kweli.
- Tunachokijua
- Jeshi la Israel (IDF) lilithibitisha kumuua Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Iran, katika shambulio kubwa la anga lililofanywa mjini Tehran, na hivyo kumaliza utawala wake uliodumu kwa miongo kadhaa. Iran pia ilikiri kifo chake na kutangaza mipango ya uongozi wa muda.
Kufuatia kifo cha Ali Khamenei kilichodaiwa kusababishwa na mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel, Iran ilimtaja Alireza Arafi kuwa Kiongozi Mkuu wa muda. Arafi ni mwanazuoni wa juu wa kidini mwenye uhusiano mkubwa na taasisi za kidini na kisiasa za Iran, na aliwahi kushika nyadhifa muhimu ikiwemo katika Baraza la Guardian Council.
Madai
Kumekuwapo na taarifa inayosmbazwa mtandaoni kuwa kiongozi mpya wa Iran Alireza Arafi ameuawa.
Je, ni upi uhalisia wa Taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli, kwani hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichothibitisha au kutoa taarifa hiyo. Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa madai hayo yanatokana zaidi na uvumi wa mitandaoni kuliko taarifa za mamlaka au vyombo vya habari vinavyoaminika.
Hakuna uthibitisho rasmi uliotolewa na vyombo vya habari vya serikali ya Iran, serikali za kigeni, au mashirika makubwa ya habari ya kimataifa kuhusu madai ya kifo hicho.
Taarifa rasmi zinaonyesha kuwa Arafi aliteuliwa kuongoza baraza la uongozi wa muda wa Iran kufuatia kifo cha kiongozi mkuu wa muda mrefu, Ayatollah Ali Khamenei.