Wangapi wangefanya kinyume na Klyn?

Na wako bitter kweli, na wame-dragg issue iwe ya Klyin na hujuma dhidi ya Mzee wetu wa Kichaga. Mali ya Mengi imegeuka ya Kabila...hahahaaa
Asante mkuu na wewe umeliona hilo, nilipo hapa nimezungukwa na wachaga, seriously wana hasira na Jackie coz mali za mzee zitaenda kwa mtu baki. Wasijue kuwa Jackie kazaa na mzee, alikuwa analala uchi na mzee, she knows better than every chagga out there...
 
Im number one Man Utd fan. GGMU
Mkuu mie Hadi najihisi kukosa amani siku hizi tulizovurunda!ushabiki wa hivi itabidi nipunguze aisee ntakuja kukwama Mambo mengine huko mbele ya safari coz sioni tumaini hivi karibini.
Pamoja Sana mkuu
 
adui wa mwanamke siku zote ni mwanamke mwenzie!
 
Weee nani anapenda shida?
Wengine ooh kwa nini Jacky aliingilia familia ya watu, jamani kwani Jacky ndo aliyewaachanisha? Afu kwa nini hawakumshauri basi mzee asioe tena ; maana yeye mwenyewe ndo aliamua kumuoa Jacky. Basi sasa hivi itakuwa hata kuolewa na single dad/mom ni kuingilia na kuvunja familia ya watu; wenyewe wakishindwana waendelee tu kubaki single walee watoto

Nimecheka jamani eti Jacky hakualikwa kwenye msiba wa mama Mercy; kwani kuna ulazima wa kwenda kwenye msiba wa ex wa mume wako? Me binafsi hata kama ndo ningealikwa, nisingeenda, ningewaacha waomboleze kwa amani tu. People are so bitter, hapa hawaamini kama Jacky na wanae wamepewa heshima kiasi kile; of course they deserve it; ni familia ya mzee na kama yeye mwenyewe aliiheshimu, nani wa kupinga?. Wanaishia tu kutoa kasoro, ooh Jacky halii sana, utafikiri waliambiwa Jacky ni mnyakyusa, (kwa kulia hatujambo)
 
Kwa hiyo wanazengo walitakaje labda? Walitaka waseme marehemu hakuwa na mke au..?
 
watanzania na sie tukiamua kuchekesha. Ikitokea Mengi anaamka hapa hakika hawezi kutuelewa. Umesema mali za ndugu yetu? Hahaha hivi sisi ambao roho zinatutoka tuna hata undugu na marehemu?
Me mwenyewe siwaelewi; ila nahisi walitaka Jacky na wanae wasiruhusiwe kuwepo msibani; na sielewi ni kwa misingi ipi. Ila binadamu tunatia aibu jamani; mali za ndugu zetu zinatutoa roho mweeh.
 
Ndio maana nikauliza, hawa wanaomuona Klyn golddigger wangepata hio nafasi wangechomoa? Kwa chuki wazoonesha,sidhani.
 
ile ya Mengi ilikufa mama alipokufa ,ya Jack haikuhitaji kanisa ,ilifungwa kwa kuisgi chini ya paa moja Kama mke mwaka mmoja hiyo ni ndoa halali,
Tunachomlaumu na kumshangaa dada jaqline ni kutaka 50% ya Mali,atambue nusu ya Mali ni za mama Mengi na walithi ni abigael na Regina ,nusu inayobaki ni ya Mengi walithi ni hao wawili na wadogo zao hivyo Regina na abigael wanabeba 75 per kylin 25% ambayo jamani ni 100mil USD kwa mujibu wa Forbes ,Sasa Hawa mabush lawyer wanamdanganya apambane apate nusu jamani wamachame watamuua yy au watoto achukue fair yake akae kimya
 
Neno n moja tu huwez kushindana na mwenye Kinywa wataongea weee wakichoka wataacha na maisha yataendelea kwan Mengi s alioa kwa hiar wangap wanadanga na babu zao
 
Mkuu wewe ni lawyer wa marehemu?
abigael=Abdiel
 
Wanaosema hivyo utafikiri kwao wapo clean! Ila mali kitu ingine bana. Unaweza kushangaa hata Wanafamilia waliokuwa wanamheshimu sana Mengi ghafla leo wanatengeneza 'timu' ya maangamizi ili binti asipate kitu. Hata hii 'blackmail' nayoiona ni kazi ya 'ndani'

Na kweli Mtu ambaye alikuwa analala na Mengi uchi na wamezaa Watoto leo adui wa Kabila zima...hahaa. Habari ya Yesu 'na asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe'.

Familia moja Mtoto wa Mzee mwenye Mji siku akaniambia 'usione hapa Mzee anaheshimiwa sana na ndugu ikiwemo sisi, siku akiondoka utaona moto'. Na amejipanga, siku Mzee akiondoka kabla yake baada ya kila kitu anamhamisha hapo Mama yake na hatadai urithi wowote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…