Wanayofanya mastaa kambini uzinzi 125% | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanayofanya mastaa kambini uzinzi 125%

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Apr 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  Na Mwandishi wetu
  MASTAA waliopiga kambi kwenye hoteli moja (jina tunalo) iliyopo Makongo Juu, Dar es Salaam wakirekodi filamu ya Tatakoa, wamenaswa usiku wakiwa wamelala kitanda kimoja jinsi tofauti, kitendo kilichotafsiriwa na watu kuwa ni kichocheo cha uzinzi kwa takribani asilimia 125, Risasi Jumamosi linashuka na data zilizoshiba.
  Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, mastaa hao walinaswa na kamera saa 6:36 usiku wakiwa kwenye chumba kimoja chenye vitanda viwili, lakini kimoja kikiwa kimelaliwa na wasanii wenye jinsi tofauti bila kujali ni mke, mchumba wa mtu na kondom huonekana zikizagaa ovyo wakati wa asubuhi.

  ISHU KAMILI

  Msanii mmoja wa kiume ambaye jina lake halikupatikana mara moja inasemekana huonekana kwenye Tamthiliya ya Red Apple, wa kike ni Zerishi aliyewahi kutamba na Kundi la Chemchemi Arts Promotion ‘Kidedea’.
  Kitanda cha pili, walilala Dora Redson ‘Kadadaa’ (msanii wa zamani wa Kaole Sanaa Group) na staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’.


  WAFUNGUKA

  Baada ya kuiweka kibindoni picha hiyo, paparazi wetu alimuuliza Kadadaa uhalali wa kupiga kambi huku wasanii wenye jinsi tofauti wakitumia kitanda kimoja ambapo alifunguka kwa kusema:
  “Mh! Unajua wakati mwingine watu wanakuwa wamechoka tu, wanapumzika, lakini inategemea uhuru wa mtu. Mimi kambini huwa nalala na wanawake wenzangu.”
  Baada ya kuzungumza Kadadaa, paparazi alimwendea hewani Nisha ambaye kwa upande wake alisema:
  “Aaaa, hapo tulikuwa kwenye shooting, wala hakuna tatizo kabisa.”
  Msanii Zurishi yeye hakupatikana kwenye simu yake ya mkononi kuzungumzia ishu hiyo.
  [​IMG]TABIA ZA KAMBINI
  Uchunguzi zaidi wa Risasi Jumamosi umebaini kuwa, vitendo vinavyofanywa na wasanii wanapokuwa kambini havitazamiki licha ya kwamba, baadhi yao wana familia.
  Nyota mmoja ambaye hakuwa tayari jina lake lichorwe gazetini, alisema kuwa, mara nyingi mastaa wanaporekodi sinema, hugeuza kambi kuwa kilinge cha mambo yasiyofaa.
  “Kama ni uchafu sisi wasanii nafasi yetu ni kambini. Kule hapajalishi umeolewa, umeoa. Hata yule ambaye akiwa nyumbani familia inambana, basi humalizia machungu yake kambini.
  “Wapo wasanii ambao wakati wa kuwekodi, wapenzi wao huja kambini na wao huwa wapole lakini wakiondoka usiku, kazi huanza hapo, pombe kwa sana, mapenzi usiseme, mpaka unajiuliza hivi kweli huyu kaolewa au ameshaachika ?” Alisema staa huyo wa kike.


  CHUZ NAYE AKIRI

  Risasi Jumamosi pia lilizungumza na bosi wa Kampuni ya Chuz Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’ na kumuuliza kama kambini kuna tabia hizo.
  “Ah! Si kambini tu, hata mitaani zipo. Kikubwa watu wanaangalia zaidi kambini kwa sababu jamii moja inakusanyika kwa wakati mmoja, unataka kuniambia mtaani, wake za watu au waume za watu hawatoki nje ya ndoa zao?
  “Sisi tunachukua wasanii kwa makubaliano ya kushiriki filamu tu, tabia binafsi ni vigumu sana kuzidhibiti kwa sababu ni watu wazima na hazipo kwenye mikataba,” alisema Chuz.

  Picha zaidi bonyeza hapa
  WANAYOFANYA MASTAA KAMBINI UZINZI 125% - Global Publishers
   
 2. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  shit...!
   
 3. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hawasi mastaa bali malaya wa kawaida wanaotafuta soko kupitia uigizaji. Staawatatoka Tanzania? Tanzania hakuna sanaa bali balaa. Jitu maskini kielimu hatakifedha. You are not stars but scars to our culture. Jitu linajiona superstareti kwa vile linaonekana kwenye televisheni. Acheni ushamba na ulimbukenimtauana bure kwa kuigiza masupa staa wa ulaya wanaolipwa kuliko nyie vinukajasho.<o:p></o:p>
   
Loading...