Wanawatapeli wanaotafuta kazi

Wanawatapeli wanaotafuta kazi

gamba2000

Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
10
Reaction score
6
Kuna hawa jamaa Matapeli wamejitangaza kama Employers kwenye hii website ya 3Wjobs.com kwa kutumia jina la Kampuni moja maarufu inayochimba madini hapa nchini. Kuna nafasi za kazi zimetangazwa pale na utatakiwa kutuma CV yako kwenye hii website na hawa matapeli watajulishwa na hii website kwasababu wamejiweka wao ndiyo Employers.

Baada ya siku moja au 2 baada ya kuweka CV yako watakupigia simu kukuomba uwatumie nakala za vyeti vyako na kukuambia kwamba kutokana na maelezo ya kwenye CV yako na vyeti vyako inaonekana kwamba ‘you are the right candidate for the job’. Watakuambia inabidi uwapoze wazee kwasababu wameshaamua kukupa hiyo nafasi. kwasababu wewe uliomba hiyo nafasi online na kwenye website inayofahamu kuwa ni ‘legitimate’ na pia kwasababu unashida ya kazi unaamua kuwatumia pesa.

Baada ya hapo watakutumia ‘fake contract’ yenye nembo ya kampuni hiyo ya madini watakuambia uweke sahihi alafu uwatumie. Usiposhituma mapema wataendelea kukurubuni na vijisababu vingi tu ili uendelee kuwatumia pesa.. k.m. watakuambia kuna Bosi moja wa HR ambaye alikuwa na mtu wake ambaye anadai apozwe kwasababu mtu wake hakuchukuliwa… utawatumia pesa tena, mara watakuambia anayehusika na kuidhinisha tiketi za ndege anazingua kwasababu anajua kuwa wale wenzake wamepewa hela naye anataka apozwe.

Baadaye watakutumia hadi barua ya ajira kwenye e-mail yako ikiwa na nembo ya kampuni hiyo.. sasa itakapofikia kukutumia tiketi ya ndege, wanaanza ooh.. mara kuna matatizo yametokea pale ofisini, subiri watakutumia. They are sweat talkers, huwezi kuamini ni matapeli na ukiwapigia simu wanapokea na kukupa ahadi za uongo.

Namba za simu wamesajili kwa kutumia majina na vitambulisho feki. Ndg zangu mnaotafuta kazi kuweni makini na hawa jamaa, wapo jamaa wane na wanakaa maeneo ya Kinondoni. Sasa ukishawashtukia na kuwaambia wakurudishie pesa yako, wanakuambia tutafutie mtu mwengine alafu tuchukue pesa kwake tukurudishie wewe.. just imagine!

Jamaa wenyewe, namba na e-mail zao ni hawa hapa:-

Boniface Mrema – 0655787879 (huyu ndiyo kiongozi wao)
Emmanuel John – 0712547980
Rweyamamu Z.Nyakale (Mr. Shukuru) – 0714219993 / 0758838388 (huyu anajiita HR Manager)
Regnard Mluma – 0715990556

LAURENT KILAMA <jonkilama@yahoo.com>
Emmanuel Ngawilo <engawilo@aol.com>
 
Ndo ajira million moja hizo za kikwete wewe tulia ukipigwa kausha huko huko mambo ya kuleta huku jf sio ishu
 
pole mkuu ukiona kitu kipo kirahisi sana basi stuka then kusanya info za kutosha kujiridhisha.
 
sio 3wjobs tu,hata zoom na site zingine za ajira kuna matapeli,hamna sababu ya kutuma ela ila uajiriwe kama ume qualify then inabidi wakuajiri direct,au waambie nitawalipa nikipokea mshahara wangu wa kwanza,organisaton zingine hazina website wala physical address lakini utakuta mtu ana apply,maisha magumu kila mtu anahangaika atoke vipi?
 
Hata wewe mleta post nina wasiwasi nawe you might be among of,ila mmedhurumiana ukaamua kumwaga mboga ama sijui ugali vile?Yaani umejiunga Jf June,2012 leo ndiyo unapost hapa June,2014?!!!!!!!!
 
Kuna hawa jamaa Matapeli wamejitangaza kama Employers kwenye hii website ya 3Wjobs.com kwa kutumia jina la Kampuni moja maarufu inayochimba madini hapa nchini. Kuna nafasi za kazi zimetangazwa pale na utatakiwa kutuma CV yako kwenye hii website na hawa matapeli watajulishwa na hii website kwasababu wamejiweka wao ndiyo Employers.

Baada ya siku moja au 2 baada ya kuweka CV yako watakupigia simu kukuomba uwatumie nakala za vyeti vyako na kukuambia kwamba kutokana na maelezo ya kwenye CV yako na vyeti vyako inaonekana kwamba ‘you are the right candidate for the job’. Watakuambia inabidi uwapoze wazee kwasababu wameshaamua kukupa hiyo nafasi. kwasababu wewe uliomba hiyo nafasi online na kwenye website inayofahamu kuwa ni ‘legitimate’ na pia kwasababu unashida ya kazi unaamua kuwatumia pesa.

Baada ya hapo watakutumia ‘fake contract’ yenye nembo ya kampuni hiyo ya madini watakuambia uweke sahihi alafu uwatumie. Usiposhituma mapema wataendelea kukurubuni na vijisababu vingi tu ili uendelee kuwatumia pesa.. k.m. watakuambia kuna Bosi moja wa HR ambaye alikuwa na mtu wake ambaye anadai apozwe kwasababu mtu wake hakuchukuliwa… utawatumia pesa tena, mara watakuambia anayehusika na kuidhinisha tiketi za ndege anazingua kwasababu anajua kuwa wale wenzake wamepewa hela naye anataka apozwe.

Baadaye watakutumia hadi barua ya ajira kwenye e-mail yako ikiwa na nembo ya kampuni hiyo.. sasa itakapofikia kukutumia tiketi ya ndege, wanaanza ooh.. mara kuna matatizo yametokea pale ofisini, subiri watakutumia. They are sweat talkers, huwezi kuamini ni matapeli na ukiwapigia simu wanapokea na kukupa ahadi za uongo.

Namba za simu wamesajili kwa kutumia majina na vitambulisho feki. Ndg zangu mnaotafuta kazi kuweni makini na hawa jamaa, wapo jamaa wane na wanakaa maeneo ya Kinondoni. Sasa ukishawashtukia na kuwaambia wakurudishie pesa yako, wanakuambia tutafutie mtu mwengine alafu tuchukue pesa kwake tukurudishie wewe.. just imagine!

Jamaa wenyewe, namba na e-mail zao ni hawa hapa:-

Boniface Mrema – 0655787879 (huyu ndiyo kiongozi wao)
Emmanuel John – 0712547980
Rweyamamu Z.Nyakale (Mr. Shukuru) – 0714219993 / 0758838388 (huyu anajiita HR Manager)
Regnard Mluma – 0715990556

LAURENT KILAMA <jonkilama@yahoo.com>
Emmanuel Ngawilo <engawilo@aol.com>

Join Date : 25th June 2012
Posts : 1
Rep Power : 0
Likes Received0
Likes Given
0
Hata wewe mleta post nina wasiwasi nawe you might be among of,ila mmedhurumiana ukaamua kumwaga mboga ama sijui ugali vile?Yaani umejiunga Jf June,2012 leo ndiyo unapost hapa June,2014?!!!!!!!!
 
Ndo ajira million moja hizo za kikwete wewe tulia ukipigwa kausha huko huko mambo ya kuleta huku jf sio ishu

we niaje, asiwashtue wenzie kwanini au wewe ndo huyo hr feki.
 
Hata wewe mleta post nina wasiwasi nawe you might be among of,ila mmedhurumiana ukaamua kumwaga mboga ama sijui ugali vile?Yaani umejiunga Jf June,2012 leo ndiyo unapost hapa June,2014?!!!!!!!!

Mwache atoe tahadhari ili watu wajue utapeli wao ukute yamemkuta ndo mana katoa tahadhari
 
Unapotoa taarifa kama hii, nia na maksudi ni kuwawaonya wenzio kwamba kuna hawa matapeli wasije wakatapeliwa… tuache ushabiki, if it happens to you, you would understand how it feels…
 
wanaoponda mkuu alichoandika ni matapeli ilo halina ubishi.

utapondaje tahadhari kama hii. ilo la muda wa kujiunga linaingiaje hapa. watz acheni porojo.

asante kwa mtoa mada kuelimisha jamii
 
Join Date : 25th June 2012
Posts : 1
Rep Power : 0
Likes Received0
Likes Given
0
Hata wewe mleta post nina wasiwasi nawe you might be among of,ila mmedhurumiana ukaamua kumwaga mboga ama sijui ugali vile?Yaani umejiunga Jf June,2012 leo ndiyo unapost hapa June,2014?!!!!!!!!

Multiple ID.

Another doubt?

:focus: Washawahi nifanyia huo upuuzi ila nilishtuka mapema sana. Wanatumia company name ya ABG-African Barrick Gold. Wanawaviziaga graduates miezi kama hii coz ni wapya wapya na wana zile ndoto za "nikifika tu kitaa mwezi mmoja nishajiriwa"!
 
Vijana mjifunze, hakuna shortcut. Sio kwa rushwa ya ngono, wala rushwa ya hela. Kama unastahili, chukua size yako. Dont bite more than you can chew.

pili, kampuni yoyote yenye akili haitumii yahoo, hotmail, sijui live! Unless kuna official email address, achana nao. Ubinafsi usituponze, kama ni riziki yako utapata tu. Usipokuwa na tamaa hautatapeliwa.
 
Kwani kama ameona jambo kama hilo na akajua kuwa litaleta madhara kwetu sisi wasaka ajira asitujulishe? tusimuhukumu cha msingi tuchukue ujumbe wake na kujitahadharisha. Kama yeye ni mmoja wao basi ila ujumbe umetufikia na tutaufanyia kazi.
 
jaman ni kweli matapeli wapo kwenye ishu za ajira,inabidi mtu kuwa makini mi mwenyewe nimekutana nao lakini niliwagundua mapema maana walisema nitume ela ili HR apitishe jina langu nikawaambia nikipokea mshahara wa kwanza ndio nitawapa hiyo ela,hahahah baada ya hapo hawakunitafuta tena
 
Multiple ID.

Another doubt?

:focus: Washawahi nifanyia huo upuuzi ila nilishtuka mapema sana.
Wanatumia company name ya ABG-African Barrick Gold. Wanawaviziaga
graduates miezi kama hii coz ni wapya wapya na wana zile ndoto za
"nikifika tu kitaa mwezi mmoja nishajiriwa"!
mimi ni mwez jana tu yalinitokea kwa hao barrick, bahati nzuri tapeli huyo
hajui hr practices na me ni hr na hapo ndo mungu aliponiokolea.Nlichomfanyia kilimfanya atupe line zake alizokua ananipigia ndani ya nusu saa.
 
Dah hao jamaa ni soo jana tu tarehe 25 wamenitumia email aisee duh maelezo kibao eti nimeitwa kwenye internship blah blah nyingi mwishoni naambiwa nitume 50,000 for medical check duh jf nzuri sana aisee
 
Back
Top Bottom