Wanawake. . . .

ni kweli lugha zetu zimetofautiana lkn kitu ni kile kile.Labda ww uhang sana na wanaume lkn wanaume wenye wivu,roho ya kwa nini na majungu wamejaa tele.Kinachofanya sisi tuonekana haka katabia ni ketu ni sbb sisi wanawake tuko wengi kuliko wao hivyo ni rahisi hii tabia kuonekana kwa wingi kwetu zaidi yao na sbb nyingine ni kwamba sisi tumejaliwa maneno mengi hivyo mahali pakiwa na wivu tu hautajificha sbb ya maneno na vijembe vyetu na makelele mengi, mtu akiuliza nini tatizo hakuna sbb ya maana atakayopata zaidi ya huyu ana nyodo huyu ananionea wivu.
Narudia tena kusema tofauti yetu na wanaume ni ktk lugha tu wkt sisi tukioneana wivu tutasema "anaringa angejua huyo bwana ana mwanamke kila kona" wanaume wao wanasema"jamaa limbukeni kweli tokea apate shori mkali hata hatoi hi kwa washikaji maskani".Pia sisi kitu kidogo tunakivalia sana njuga kuliko wanaume ndo mana sisi tunaonekana sana kuliko wao ktk hili.

Pia nataka kuongezea kwenye kuhisi kuchukiwa.Unakuta mtu kafanikiwa,nyie wala hamumuonei wivu lkn kumbe yeye rohon mwake anahisi kawivu kanawamaliza,yeye mwenyewe sbb anadhani mnamuonea wivu anaanza vitu vya ajabu,mfano anaweza kuanza kutoa vijembe kama....kama ipo ipo tu,mwenye wivu ajinyonge...bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi..na pia anaweza yeye mwenyewe akawakatia mawasiliano.Nyie mnaopigwa vijembe mtaona yeye aliyefanikiwa anawafanyia nyodo,lazima mtajisikia vibaya na ni vigumu kumuombea mema na hata akiporomoka mtamcheka na kufurahia sbb nani anapenda kuona maendeleo ya mtu mwenye dharau na nyodo?

Mim naomba tu ujiulize,je ni kweli kwamba sisi wanawake tukiwa na maendeleo kushinda waume au boyfriend zetu lazima tu tutawadharau?
Kama utajibu hapana,sio wote ni baadhi ,basi jiulize kwa nini wanaume kwa kiasi kikubwa sana huwa hawafurahii mwanamke awe na kipato kikubwa kumshinda yeye kama sio wivu?
Kama ni wivu jiulize kauli hizi umezisikia kwa wingi kiasi gani.

cheusie umeeleze vizuri sana hapo kwenye wanawake kuhisi wanachukiwa na kuonewa wivu.
Hiyo ya vijembe nayo kweli ni matokeo ya hisia.
 
Hapana usifanye hivyo aisee. Huyo nimekuwa nikimtafuta zaidi ya miaka 10 sasa bila mafanikio yoyote.

wewe endelea tu kumbishia mtaalamu wa mafaili, maadam hata mimi alikuwa fevoriti wangu tukiwa uf basi ngoja nibanie tu
 
CM bado mwenyewe marafiki zangu wengi ni wa kiume. . .Hawana majungu wala kugeukana hata mkifikia kutoelewana tofauti na wanawake. Kwa wanawake chuki na kukomoana ni vitu ambavyo vina nafasi kubwa sana tofauti na wanaume.

Kuhusu wanaume kutopenda wenzi wao wafanikiwe sana, ni matokeo tu ya woga wa kuachwa solemba na kudharauliwa kwasababu wanajua sana kwamba baadhi ya wanawake ni malimbukeni linapokuja swala la pesa na mafanikio. Ndio maana wengine wapo radhi kuwaacha waume/wapenzi wao kwa wenye nazo zaidi au pale mambo yanapowaendea vibaya, wapo radhi kucheat na yule mwenye nazo zaidi, wako rafhi kuwaibia marafiki zao mabwana na kutembea na waume za watu kwasababu 'WANAZO', ni wepesi kuonyesha dharau pale wanapokua na uwezo zaidi ndani ya familia and so so. Hayo yanatokea kila siku uraiani. . .ndio maana wengine hua hata wanaogopa kusomesha wake na watarajiwa wao kwasababu wanajua kwamba uwezekano wa kuja kutukanwa na kudharauliwa kama matokeo ya elimu waliyolipia wao wenyewe upo sana.

Mim nahang sana na wanaume lakini pia marafiki zangu wa kike nimewaona wakifanikiwa nikafurahi pamoja nao kutoka moyoni nao wakanisaidia kwa ushauri na mbinu mbali mbali hadi na mim leo niko kama wao na wengine waliotangulia kufanikiwa nimewazidi lakini ni miaka imepita sijawahi muonea mwenzangu wivu wala hakuna katika marafiki zangu hao anayenionea wivu wala aliyenibadilikia.Soetimes kuna mambo kwenda vibaya,ikiwa hivyo wanakuja kwangu nasaidia niwezavyo na yakiwa mabaya upande wangu nakimbilia kwao na wananisaidia kadri wawezavyo.

Hata wanaume wana chuki na kukomoana na wenzao,hapa majuzi kuna kaka wa watu amegundua kuwa ni rafiki zake wa karibu ndo walimchomea hadi akafukuzwa kwenye duka la kaka yake alilokua anauza kisa alinunua kagari wakadhan wakimfukuzisha dukan atafulia kumbe hawakujua hiyo gari kanunua kwa shughuli zake za kilimo na alivyofukuzwa dukani ndo akazidi kufanikiwa sbb amepata muda wa kujikita zaidi kwenye kilimo.Mifano iko mingi ndo maana inaniwia vigumu kukuelewa.

Pia wapo wanaume waliokua "mume mwema" wakati hawajakamata pesa,lkn walipokama pesa ndo dharau kwa wake zao zikaanza,vimada na kutumia magari yao kupata watoto vikaanza.Kwa upande wa wake zao ukiwauliza,watakwambia tumejaliwa mali lakini aman ya ndoa imetoweka,mume wangu amebadilika,napata kila kitu lkn mume wangu hanidhamin tena,haya yanatokea sana uraian,uliza wanandoa watakueleza zaidi.Sasa hii inatofauti gani na ile ya mwanamke aliyepata pesa akabadilika?Au akifanya mwanamke ni dhambi lkn akifanya mwanaume ni kosa?Kitu ni kile kile kile mbaya zaidi mwanamke hawezi kumzuia mumewe asichukue masters yake pale anapohisi kuwa hii masters itanipotezea amani ya ndoa lkn mwanaume anao uwezo wa kumzuia mwanamke asichukue masters yake tena kisa amehisi tu huyu mwanamke akiongeza elimu kunishinda atanidharau.
Wapo wanawake wengi sana wenye pesa nyingi na elimu ya juu lakini wanaishi na wanaume ambao wao wanawake ndio wanawahudumia kwa kila kitu na mara nyingi magari na pesa zao wanazowapa hawa wanaume huishia kwenda kutongozea wanawake wengine huko nje.
 
Kala ban. . .Alafu na wewe ulimboa sijui nikulambe fimbo ngapi. . . .!!!!

Alimbwatukia nani hadi akala ban? She is so innocent....lol

Mimi nilimboa? Basi mwambie ntamnunulia Coke kutoka kwenye ile vending machine....
 
CM siwezi kataa kwamba wanaume hamna wenye tabia hizo, wapo hata mimi nimewaona ila bado sio wengi ukilinganisha na wanawake.

Ya wanawake nimeona kwa wengine, ndugu jamaa na marafiki zangu wa karibu na mie mara moja nilijionea namna watu walivyo na vituko. Kama mambo mengine yote mazuri kwa mabaya, kila kundi lina watu wanaojishughulisha nao. Ila tofauti ya wingi ipo kutegemeana na jambo pia kundi la watu. Ndio maana vitu kama roho mbaya/wivu/umbea hua vinahusishwa na wanawake. . .Sio kama wanaume hamna wenye hayo, ila wanaoongoza ni wanawake na ndio maana hua tunahusishwa nayo hata kama sio wote tuko hivyo.
 
Alimbwatukia nani hadi akala ban? She is so innocent....lol

Mimi nilimboa? Basi mwambie ntamnunulia Coke kutoka kwenye ile vending machine....
Heheehe Matola. . .hata sikufuatilia walikua wanaambizana nini.

Ila wewe ulimboa kweli. . Hata mi nilivyoona kilichomboa kabla hata sijajua kaboreka nilijisikia vibaya. Plus vimbelembele vilivyojifanya kukuza mambo baadae ndio kabisaaaa wakaharibu.
 
Heheehe Matola. . .hata sikufuatilia walikua wanaambizana nini.

Ila wewe ulimboa kweli. . Hata mi nilivyoona kilichomboa kabla hata sijajua kaboreka nilijisikia vibaya. Plus vimbelembele vilivyojifanya kukuza mambo baadae ndio kabisaaaa wakaharibu.

Nilimboa nini tena? Kumsahihisha Kingredha?

Maybe she was just having a bad day.
 
Nilimboa nini tena? Kumsahihisha Kingredha?

Maybe she was just having a bad day.

You could have done it differently. . .
Watu walikibebea bango mpaka PM. . . .maneno mengi utadhani wapo kwenye kampeni.
 
You could have done it differently. . .
Watu walikibebea bango mpaka PM. . . .maneno mengi utadhani wapo kwenye kampeni.

Duuh! Kumbe yalifika hadi kwenye PM?!

It wasn't that serious...oh well....watajiju.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom