Wanawake wenzangu, ndoa sio umeme wa LUKU

Wanawake wenzangu, ndoa sio umeme wa LUKU

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
wedding-couples-poses.jpg

OHH mke wangu kila nikirudi anavimba domo, kunipakulia tu shida nikisema hivi visingizio kibao! Heee heeeiyaaaa, utalalama sana mwaka huu, mwanamke wako mwenyewe shida zako uzilete kwangu, inahu?

Shoga leo nimekuja kivingine, nahisi mdomo wangu kama vile umemwagiwa pilipili mbuzi maana si kwa kuchachuka huku, kila mada natamani niongee tu, acha leo nianze na wale wanaume wanaojifanya wameoa kumbe wameoa umeme wa luku, halooo ehhhh, langu kalio mchana naketi kibarazani usiku feni, upo?

Baada ya kukupa udambwidambwi nianze kushusha pumzi na weeeweee! Dume zima unayejua kuwa ukishaoa na kuweka ndani unafikiri kinachofuata ni shoping na kujaza friji kama siyo kuweka umeme wa luku!

Kwanza nataka utambue mwanamke siyo umeme wa luku, ukishaoa basi unaweka ndani na kumtumia kama vocha za shilingi mia tano, utue babu nikutue ennnh! Tena nachukia wanaoendelea kukomalia kuwa mwanamke ni pambo la nyumba! Zamani sawa ila siku hizi mwanamke kuhangaika, mwanamke kusaidiana na mwanaume, akisomesha watoto basi wewe unalisha na kuvalisha watoto, upo?

Utakuta mzee mzima akishaoa basi anaona amemaliza, kila siku atakuwa akiondoka asubuhi kurudi usiku wa manane tena siku nyingine akija ananuka mipombe kama siyo harufu za pafyumu za wanawake, looo! Unafikiri huyo mwanamke kwao hakuwa anakula na kulala? Wazazi wake walishindwa kumgeuza vocha au umeme wa luku kutwa kukaa ndani na kupiga kelele unapoisha?

Badilikeni bwana nyie wanaume mlio ndani ya ndoa, hata wewe ambaye unafikiria kuoa! Labda nilipapase sikio lako kidogo kama ulikuwa hujui, mwanamke anababaika na vitu vidogo sana! Ukijitengea muda wako wa mapumziko ya kazi jaribu kushinda naye karibu, ongea naye mambo yenu ya familia, jaribu kumtoa hata outing, haloooo eeehh ya kisoda bia nitalewa miye!
romantice-couple-in-love+(2).jpg

Siku hizi, wanawake wengi wanafurahia ndoa zao kwa sababu wanaume wao wanajua jinsi ya kuwapetipeti, pamoja na kuwa wanafanya kazi Jumatatu hadi Ijumaa lakini Jumamosi au Jumapili lazima wataitenga kuwa pamoja siku nzima au nusu siku, hiyo shoping wanafanya pamoja, wanasaidiana usafi wa ndani akimaliza hapo basi anaenda kuonana na marafiki zake na huko wala hakai kwa muda mrefu anakuja kumaliza siku na wewe, upo?

Siyo umekaakaa kama feni ya panga boi iliyochakaa mpaka uilazimishe kuisukuma ndiyo iwake, shuuutuuuu! Mwanaume badilika, rejesha furaha ya nyumba, mpe nafasi mkeo ya kukaa naye, jua matatizo na umshirikishe mipango yako!

Shoga, wiki ijayo bado nitakuwa na wanaume nyienyie mnaopenda kuficha wanawake zenu mishahara, heeee heeeiyaaa kama nakuona unavyoniangalia, niko na weweeee! Tukutane wiki ijayo, ni mimi kungwi la makungwi niliyepigwa mishale mingi hadi kuota sugu,
 
Aisee, kweli wewe ni mjukuu wa chifu, kila la kheri ingawa sijui kama hii mada ni ya kujenga ama ya kubomoa. Watakuja wajuzi zaidi wataidadavua
 
yani me ndo hata aya ya kwanza nimeshindwa kuimaliza, uandishi wake umenikosesha interest ya kusoma, nimeaona nishuke kwenye comments
 
Mi nimemwelewa na kwa nature ya mada lazima aielezee kwa staili aliyotumia. Theme hapa ni jinsi ya kumfanya mke awe na furaha na aweze kufurahia maisha ya ndoa. OUTING na ku tumia muda pamoaj na mwenzi wako ameipigia mstari kama kitu muhimu kuliko nguo na madikodiko mengine unayomletea wife kila siku.
Sikutoka bure nasubiria post nyingine .
 
yani me ndo hata aya ya kwanza nimeshindwa kuimaliza, uandishi wake umenikosesha interest ya kusoma, nimeaona nishuke kwenye comments
Tatizo mko shule bado someni kwanza hebu hizi post za wababa mtuachie sisi tunazielewa !!!!
 
Sijamuelewa sana nilichoelewa nimwanamke aliyeolewa apendwe nakujaliwa mwanaume ajue kaoa na atenge time kuwa na mke wake .
 
Back
Top Bottom