wanawake wenzangu mnaonaje hili

wanawake wenzangu mnaonaje hili

ha haha kibweka vipi huwa wanakuwa wakarimu kwako nini ndo maana mnataka kuwapa tip hata kama hawajakua wakibehave vizuri
 
Acheni ujinga bana..sasa hapa mnadiscuss nini....yaani mambo haya si ya kawaida..ni mapaka ulete kwenye jf forum...siku hizi tumekuwaje....yaani swala la kumfukuza hg na kuleta mwingine ni lazima uandike jf....wanawake mmekuwaje siku hizi au digital...
 
ukiona hvyo mumeo anataka aendelee kukaa wakat anajua watoto wanateseka kutakua na k2 kat yao
 
Pole,
Hivi issue inayohusiana makuzi ya kila siku ya watoto wako inatakiwa mjadala kweli.
Majirani 3 wamekuambia kuhusu mateso ya watoto uliozaa mwenyewe lakini umeziba masikio;

Ila ungehisi tu kuwa dada anamahusiano na mume wangu ungeshamtimua tena kwa
maneno ya karaha na kashfa kubwa.

Hivi siku ukirudi ukakuta amewafanya watoto wako kama yule mjakazi wa sinza utasemaje?
 
Kwanini unamuajiri mfanyakazi ambae hawezi kutekeleza wajibu wake?
Huyo ni mfanyakazi na yupo hapo kwaajili ya kazi kwahio kama haiwezi kazi hana umuhimu wa kuwepo hapo kabisa..Huyo analipwa sio kwamba kajitolea akusaidie bure...
Kama keshaonesha ishara kwamba si msadizi mzuri katika malezi ya watoto wako anaweza kuwadhuru watoto kwa aina yoyote ile kwasababu anaonekana yupo violent and abusiv inawezekana anawafinya au anawapiga makonzi wewe huna habari..Hebu muondoe haraka sana utafute mtu mstaarabu anayejua kuwajibika!!
 
unahousegl ukimpa maelekezo pika mboga ya majani hapiki unakuta maharage tu ukimuuliza baadae anakuambia amesahau, anapiga watoto na kuwasukuma hawezi kuvumilia mtoto sekunde akimwita mtoto akavae au kuoga akitembea taratibu anashika kichwa anasukuma hilo nimelishuhudia anakuja mtu wa 2 analalamika hivyo hivyo anakuja wa 3 analalamika kwamba huyu dada watoto hawawez atawaumiza ukimwambia atafute kitu kila siku hakioni, ukiwepo anakuwa busy ukiondoka tu kwenye tv, kazi anasaidiwa na mtu mwingine aliyeko nyumbani kufua kuosha vyombo anasaidiwa kuogesha watoto anasaidiwa hlf inafika mwisho wa mwezi mwenzako anaongeza juu zaidi ya nusu ya mshahara wake eti kwasababu mwenzake alikua amesafiri tumwongezee na huu ndo mwez wa 2 toka afike na mwez wa kwanza tu alipofika unajua kama kawaida watoto wanakuja kuna vitu wamepungukiwa kwahiyo inabidi umnunulie vile vitu muhimu nafikiri mnanielewa nikisema hivyo na nilimleta mtu mwingine kwasababu ya kumsaidia wkt mwingine kwasabau niliona hataweza toka mwanzo. kwangu kumpa nyongeza mdada ni kawaida kwasababu ndio wanalelea watoto wangu na huwa inatokea sana pia ili kuwapa moyo ila kwa huyu tabia zake hajanifurahisha je imekaaje hii

Mkiambiwa mchukuwe ma house-girl waliokwenda kusomea hizo kazi hamtaki, mmekalia ubahili halafu mnalalamika.

Nenda kachukuwe ma house girl kutoka vyuo vya hotel management, utapata wapishi na ma house keeper mpaka mwenyewe utaona raha mradi uwalipe ipasavyo uone kama hayo yatatokea.
 
Back
Top Bottom