wanawake wenzangu mnaonaje hili

wanawake wenzangu mnaonaje hili

melisafilbert

Member
Joined
Sep 3, 2013
Posts
67
Reaction score
9
unahousegl ukimpa maelekezo pika mboga ya majani hapiki unakuta maharage tu ukimuuliza baadae anakuambia amesahau, anapiga watoto na kuwasukuma hawezi kuvumilia mtoto sekunde akimwita mtoto akavae au kuoga akitembea taratibu anashika kichwa anasukuma hilo nimelishuhudia anakuja mtu wa 2 analalamika hivyo hivyo anakuja wa 3 analalamika kwamba huyu dada watoto hawawez atawaumiza ukimwambia atafute kitu kila siku hakioni, ukiwepo anakuwa busy ukiondoka tu kwenye tv, kazi anasaidiwa na mtu mwingine aliyeko nyumbani kufua kuosha vyombo anasaidiwa kuogesha watoto anasaidiwa hlf inafika mwisho wa mwezi mwenzako anaongeza juu zaidi ya nusu ya mshahara wake eti kwasababu mwenzake alikua amesafiri tumwongezee na huu ndo mwez wa 2 toka afike na mwez wa kwanza tu alipofika unajua kama kawaida watoto wanakuja kuna vitu wamepungukiwa kwahiyo inabidi umnunulie vile vitu muhimu nafikiri mnanielewa nikisema hivyo na nilimleta mtu mwingine kwasababu ya kumsaidia wkt mwingine kwasabau niliona hataweza toka mwanzo. kwangu kumpa nyongeza mdada ni kawaida kwasababu ndio wanalelea watoto wangu na huwa inatokea sana pia ili kuwapa moyo ila kwa huyu tabia zake hajanifurahisha je imekaaje hii
 
wewe ni melisa gani?wa masogange?sasa hapo hujui dada cha kufanya?utaishi naye vipi na kumuachia mwanao mtu ambaye humuamini?si anaweza hata mlisha sumu mtoto
 
tafuta mtu mwngine,ukishampata fukuza huyo....hafai
 
mwondoshe kabla hayajawa makubwa, kama umeshajua kuwa hawezi kucheza na watoto wako , basi pia hawezi ishi nao ukiwa kazini, so usiangalie makunyanzi ukaja jutz baadaye, fanya kazi zako ukisaidiana na huyo amsaidiae yeye. wakati huo unaendelea kutafuta msichana mwingine.
 
huyo asiyependa watoto unakaa nae ili aweje? Mpaka awatie kwenye friza?


Agiza meingine

Badilisha hg kadri uwezavyo mpaka upate unayemtaka haswa mwenye maoenzi na watoto mradi umtreat vyema
 
Kama kweli mtu hawezi kukaa vizuri na watoto(kitu ambacho nadhani ndio sababu kubwa ya wewe kumuajiri) na bado unaomba ushauri basi mi nakwambia MVUMILIE mpaka kieleweke!!!
 
Jitihada za makusudi zichukuliwe dhidi ya huyo mdada,anacho kifanya kina madhara ya kimwili,kiakili na kisaikolojia kwa watoto wako sasa na baadae,nipendekeze kwako kumsimamisha kazi huyo dada ,hana jema,
 
Japo me sio "Ke" lakin bora huyo, house girl wetu alikuwa anampangusa mtoto mdomo kwa kumlamba mdomoni, tukamtimua fasta
 
Ndo maana wenzetu Wafilopino na baadhi ya mataifa mengi wafanyakazi wa ndani huwa ni watu wazima kabisa ila kwa huku Bongo tunahangaika na Visichana vidogo wakati hata vyenyewe kuoga havijui sasa sijui huyo mtoto wako kama atatakata!!
 
Kama kweli mtu hawezi kukaa vizuri na watoto(kitu ambacho nadhani ndio sababu kubwa ya wewe kumuajiri) na bado unaomba ushauri basi mi nakwambia MVUMILIE mpaka kieleweke!!!
welcome back Lizzy.....
Yaani mimi ninapotafutaga mdada kitu cha kwanza namwambia yupo pale kwa ajili ya watoto tu na si kingine. Kwa hiyo kama haweza au hapendi watoto aniambie kabisa aondoke. Kazi zote za nyumbani naweza kuzifanya mwenyewe but nahitaji mtu wa kukaa na wanangu nikiwa job, ndo kazi niliyomwajili.
Sasa huyu dada ambaye ana uwezo wa kuwashurutisha watoto hata mbele ya watu ni hatari, na yeye anamvumilia tu? na kuja kuomba ushauri?
 
acha ushamba mdada, yan anafanya yote hayo na wewe unamwangalia? na huyo mumeo nae anamwangalia? nahsi ningemtimua na kipigo heavy
 
Huyo lazima ni mkarimu kwa MUMEO.............................!:A S 41:
 
Kuna siku utakuta kamchoma moto mtoto kwenye papuchi alaf kasepa.rudisha kwao huyo mbona kila cku watu wanatafta kazi za uhousegl humu ! Hafai huyo!!!
 
mi simtaki toka mwanzo kusema la ukweli ila kwenye nyumba mpo wawili wewe unapoamua hivyo mwenzako anakuambia mwache kwanza sasa swali langu kubwa ni kweli huyu anastahili kupewa hiyo tip mwenzangu anayotaka kumpa au ananitafuta ubaya tu
 
Lizzy mi simtaki kabisa kabisa hapa siombi ushauri wa kuendelea kukaa nae ila nilikua nawauliza imekaaje hii msichana na mambo yote hayo halafu bado mwenzio anakupa mshahara wake na tip ya zaidi ya nusu wa mshahara wake juu
 
Back
Top Bottom