Wanawake wenzangu kimbieni kifungo cha mapenzi

Wanawake wenzangu kimbieni kifungo cha mapenzi

Heloo

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
4,391
Reaction score
3,409
Wasalaam!

Wanawake wenzangu ni wakati sasa wa kuamka toka usingizini na kutafakali kama uhusiano uliopo kwa sasa ni wa AFYA AU wa kupotezeana muda!Inatokea mara nyingi unakuta dada anageuzwa mtumwa wa mapenzi bila kujitambua.ananyanyaswa,anadhalilishwa,utu wake unapotea,anakuwa ni mtu wa kupigana na huyu na yule eti kwa jili ya kulinda penzi.

Dada yangu hakuna penzi hapo bali ni utapeli,ivi mpenzi wa kweli anaweza akakuumiza,mfano kwa kujihusisha na wanawake wengine tena waziwazi,akidai ni marafiki,au visingizio vya kwamba wanakuwa pamoja kwa jili ya mipango?

NI kweli ni vizuri kuwa na mpenzi unayempenda lakini ni bora zaidi kuwa na mpenzi mtakayependana mana kwa kuwa na mpenzi unayempenda wewe na ilihali haonyeshi mapenzi,hakujali,anakubari uumie,anadhalilisha utu wako ni utumwa zaidi kuliko kufungwa GEREZA LA GUANTENAMO, na ni UPUUZI NA ukosefu wa AKILI.

KUNA baadhi ya wanaume anapogundua ana mpenzi na hapindui wala haoni kwake basi atamwanzishia vitimbi na vituko akijua atafanya nini bila mimi,atamgeza ATM ,Atamuumiza kwa kila namna na hata kumshusha,SASA rafiki yangu popote ulipo kimbia,mwache Endelea na maisha yako mengine.

Mbona kabla hamjakutana ulikuwa ukiishi kwa raha na furaha mpaka akakufuata? sasa kama ni rimbukeni wa mapenzi muache nae akutane na ya dunia!ONYESHA msimamo wako kwa kuanza upya!!

Unaweza kuta kwa kumg'ang'ania mpenzi asiyejali mapenzi yako ukawa unajipotezea bahati ya kukutana na mtu sahihi maishani mwako,kwa nini uanze kuwa mwanamasumbwi kwa kugombana na huyu mara yule,kwa kitu gani hasa ambacho mwingine hana....AU huyo anajidaia nini....MWACHE!!!

Yaani kuna wanaume na MAGUMEGUME!! Unatokea kumpenda mtu kwa dhati,unamwamini,kumbe moyoni mwake anakuwa na mengi,unampomgundua unaamua kusitisha mahuasiano...anakufuata kwa kila hali kwa kuwa unampenda unaamua kuanza nae upya...bada ya muda anarudia yaleyale....(Jamani waume wa ivi acheni ni DHAMBI KUBWA)

ONYESHA MSIMAMO KWA KUMKATALIA KWA NIA! MANA BILA KUFANYA IVYO UTAJIKUTA UNACHINA NA WAKATI HUO YEYE ATAKUWA HAKUJUI.Kama unashindwa hama eneo alilopo KAMA mpo eneo moja,ama laa,epuka kuwasiliana nae kwa namna yoyote ile,futa no.zake za simu ikiwezekana au ziache ili akikupigia iwe rahisi kukata.

Epuka kumfuatilia mambo yake,kuwa busy kama ni kazi,biashara au masomo,,tembelea ndugu na jamaa na marafiki,usipende kukaa sehemu mlizokuwa mnakaa wote,epuka kuwasiliana na marafiki zake,zile za shemeji shemeji zaweza kukutonesha kwani unamwacha ukiwa unampenda unachofanya hapa ni kumsahau polepole na hatimae kuufanya moyo kuwa na nafasi pengine wa kumkaribisha mwingine.

Ila hapa napo kuwa makini usije ingia mahusiano mapya eti ujisahaulishe na wa mwanzo unweza jiuta ukawa FRUSTRATED in a way you become CRAZY!!SABABU unaweza kuta ni afadhali ya kule ulikokimbia......!

Other thing ni kwamba unaweza ukawa busy hata kwenda kanisani baada ya shughuli zako na ukaweza kujiunga na kwaya kama we ni mkristo....HAKIKA UTASAHAU NA UTAMPATA ALIYE SAHIHI KWENYE MAISHA YAKO! AKSANTE.
 
kweli hii thread mvurugo...

Mtoa mada, kama hadi leo ulikua hujajua hayo basi rudi tu kwenu mahenge ukapembue mchele

Yaani kila neno ulilosema hapo ni marudio ya ushauri ambao una zaidi ya miaka 20... wenzako walikalia kikao kabisa Beijing wakiongozwa na Getrude Mongella miaka ileeeeeeeeeeeeeee

kweli maisha kwa wengine yapo Sloooww moooo--tion
 
Nikuulize swali kidogo na usikimbie unijibu..unapenda shul yoyte kusoma ivi unakuta yote mapya au ni ya miaka hata 50 iliyopita ila inabidi ujifunze.......tafakari bwana huwezi jua yamenikuta yapi....
 
Lini mwanamke akawaza kama kuna future katika relationship?

ninyi mkishaambiwa '' i love you '' , basi inakuwa ndo basi, uhoji kwani uko peke yako? marriage is a fate nowadays!

wa kukuoa huwezi jua anatokea wapi! unaweza kuwa dar lakini husband akawa yuko sumbawanga hata hamjuani!

at the end, mkaja kukutana in just a coincidence... then marriage without time wastage!

Gravitation, remember!-- has nothing to do with falling in love!
 
NILIJUA utacomment namna hiyo mana ndo zako wewe...sijui kwa nini THE boss!!
siku hizi unaijua future eenh?

hebu tuambie Rais wa 7 wa Tanzania ni nani?

huhuhuuu! natania mkuu!

relax..!
 
Lini mwanamke akawaza kama kuna future katika relationship?

ninyi mkishaambiwa '' i love you '' , basi inakuwa ndo basi, uhoji kwani uko peke yako? marriage is a fate nowadays!

wa kukuoa huwezi jua anatokea wapi! unaweza kuwa dar lakini husband akawa yuko sumbawanga hata hamjuani!

at the end, mkaja kukutana in just a coincidence... then marriage without time wastage!

Gravitation, remember!-- has nothing to do with falling in love!

Uliyoongea yote ni ya kweli lakini kma umenisoma naongelea kwa wale wanaume wanaojua fika wanadanganya but still pretending being in that relationship...so why doing this?
 
siku hizi unaijua future eenh?

hebu tuambie Rais wa 7 wa Tanzania ni nani?

huhuhuuu! natania mkuu!

relax..!
Na wewe unavyoonekana ni lazima umeliza au uliliza wengi!
 
kweli hii thread mvurugo...

Mtoa mada, kama hadi leo ulikua hujajua hayo basi rudi tu kwenu mahenge ukapembue mchele

Yaani kila neno ulilosema hapo ni marudio ya ushauri ambao una zaidi ya miaka 20... wenzako walikalia kikao kabisa Beijing wakiongozwa na Getrude Mongella miaka ileeeeeeeeeeeeeee

kweli maisha kwa wengine yapo Sloooww moooo--tion

akirudi asisahau kuniletea pepeta na samaki wa kilombero..
 
Wakati naandika kweli machozi yalikuwa yananitoka lakin kwa ulivyoandika....nimejikuta nacheka.
AKSANTE!

Usijali mama ni ya kawaida tu, piga moyo konde maisha ya songe si unajua dunia inazunguka
 
Back
Top Bottom