Wanawake wapata maendeleo makubwa nchini China

Wanawake wapata maendeleo makubwa nchini China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,244
Reaction score
1,213
VCG111371718919.png


Wakati dunia inapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, mwanaanga wa China Bibi Wang Yaping, ametoa salamu kutoka kwenye Kituo cha Anga ya Juu cha China, akiwatakia wanawake wote duniani ulimwengu “wafuate nyota inayong’aa zaidi kwa ajili ya maisha na kazi wanayopenda.” Kutoka “kufunga miguu”, hadi kuwa wanawake wanaoweza kusafiri kwenye anga ya juu, wanawake wa China wamepata maendeleo makubwa.

Katika zama za kale, wanawake wa China walikuwa na desturi ya kuifunga miguu yao kwa kitambaa kuanzia wanapokuwa na umri wa miaka mitatu au minne hadi wanapokuwa watu wazima, ili kuifanya miguu yao iwe midogo, na kupendwa na wanaume. Mchakato huo ulikuwa mchungu sana. Nyuma ya desturi hiyo, ni mawazo maovu ya kuwakandmaiza wanawake, na kuwachukulia kama mali ya wanaume.

Baada ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, wanawake wamekombolewa, na mawazo mapya kama vile “wanawake ni sawa na wanaume”, na “wanawake wanabeba nusu ya anga” yamepokelewa na watu. Wanawake wa China walianza kuchukua majukumu kama wanaume, ambapo hadhi yao ya kisiasa, kiuchumi na kijamii imeboreshwa siku hadi siku.

Kwanza ni kuboreshwa kwa hadhi ya kisiasa. Wanawake wa China sasa wanaweza kushiriki kwa kina katika masuala ya utawala wa kisiasa na kijamii. Mambo ya kisiasa si tena eneo la wanaume tu, wanawake pia ni washiriki muhimu.

Pili ni kuboreshwa kwa hadhi ya kiuchumi. Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, wanawake wa China wanaweza kuchagua ajira kama wanaume, na mapato yao pia yameongezeka kwa kiasi kikubwa. Aidha, China inahakikisha kisheria haki za wanawake za kupata ajira, mali, na huduma za kijamii.

Tatu ni kuboreshwa kwa hadhi ya kijamii. Haki za elimu, ndoa na afya ni mambo matatu muhimu ya kijamii kwa mwanamke. Sheria ya Elimu ya Lazima ya China inahakikisha haki ya wasichana ya kupata elimu. Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 92.3 ya wanawake wa China walio na umri wa zaidi ya miaka 6 wanapata elimu, na asilimia 13.6 wamepata elimu ya juu. Katika suala la ndoa, wanawake wana haki ya kuchagua ndoa kwa uhuru, na wanafanya maamuzi ya mambo makuu ya familia. Kwa upande wa haki ya afya, hali ya afya ya wanawake nchini China inaimarika siku hadi siku, na huduma za uzazi zimekuwa huduma ya msingi ya afya ya umma nchini China.

Ikilinganishwa na historia na hali ya sasa, wanawake wa China wamepata maendeleo makubwa. Katika zama mpya, China itaendelea kufanya juhudi ili kuhimiza maendeleo zaidi ya wanawake, na kuimarisha zaidi usawa kati ya wanawake na wanaume.
 
Back
Top Bottom