Judgement
JF-Expert Member
- Nov 13, 2011
- 10,326
- 4,789
Hivi walivyo Muumba kawanyima mgao wa misuli , nguvu , ujasiri , na ubaramaki nanga zinapaa !!
Wangapiwangapi mijadume tunaiona ikizidiwa power za kiutendaji na wapenzi wao !
Janadume la haja na misuli yake , linapelekeshwa kama kihongwe .
Wakati Muumba akitoa mgao wa pembe kwa wanyama wafugwao , Punda hakuwepo eneo la tukio .
Na mara alipofika tukioni , akadai nae pembe .
Muumba akamwambia Pembe zin'kwisha! Akauliza "kumebaki nini?"
akajibiwa
"Yamebaki maskio na miguu iliyo mahirika upigaji mateke!"
Punda akajikuta kaomba salio bakizi , na Muumba akampa .
Na ndiyo Punda (Donkey) tulienae hivi sasa .
Hivi unadhani Punda angepata pembe , na hii miguu mahiri ya mateke , Binadamu angemmudu kumfuga ?
Ni dhahiri pangechimbika kama sio kukalika.
Tumrejelee mwanamke !
Mwanamke angepata musuli , nguvu , ujasiri na ubaramaki , aidha kichwa cha nyumba , ukachanganya na ile nguvu asili ya haiba ya kike , sie wanaume tungepumulia wapi ?
Ama Mungu aliwajua mapema ndiyo akaumba hivi ilivyo?