Wanawake wanatuchukuliaje wanaume aina hii?

Wanawake wanatuchukuliaje wanaume aina hii?

Ndenji five

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
1,985
Reaction score
3,120
Habari wakuu

Moja kwa moja kwenye mada. Kuna binti mmoja nilitokea kukutana nae kwenye bus ambapo nilikaa nae siti moja kama unavyojua sisi wanaume ni katokea kumtamani ila sikuonesha hisia zozote vijana tunasema nikamlia ngumu bila salam wala tabasam tumefika katika ya safari

Akaanza kuniongelesha kwa kuomba simu yangu basi nikasema inshallah bora alivyoanza yeye tukaanza piga story za uongo na ukweli akawa ananinunulia vitu vya hapa na pale

Tumefika muda tukawa kama tumewahi Kutana sehem au ni ndugu na katika ile safari nilikuw naelekea
mimi ni mgeni sijawahi kwenda
ila kwa upande wa yule binti ni mwenyeji basi akawa ananielekeza baadhi ya maeneo maana safari ilichukua kama masaa13 mpaka kufika hiyo sehem

Basi akawa ananielezea maisha yake nilipenda sana jinsi alivyokuwa na tabia ya ucheshi akapelekea nimchukulie kama dada yangu kufikia hapo tamaa zangu za kumtaka kum....zikakata kumbe mwenzangu anahisia tofauti na mm

Basi hadi kufika mwisho wa safari tukaagana vizuri end the day tukawa tunasaidiana akiishiwa kitu na mtumia pesa nikiishiwa ananitumia

So tunaishi hivyo na jana amenicheki anaomba aje kwangu kwa hiyo nimuongezee nauli na ukiangalia mimi nimeoa na sijamwambia kuhusu hilo

Na sijui yeye ananichukulieje maana hatujawahi kuongelea kuhusu mahusiano sasa sijui nimkubalie aje hom kwangu au nifanyeje maana wife nilimueleza kuhusu hilo akasema mwambie aje ila kwa upande wa yule binti ndio sijamjuza chochote ushauri wenu wakuu
View attachment 2017975
 
Hili nalo jambo kubwa la kuandalia uzi mkuu?

Kama Mwanaume huelewi ni maamuzi gani ya kuamua mpaka sasa?

Mwanamke umemtamani, akaanza kununulia vitu kwenye Gari na story kibao, mkaanza kusaidiana shida zenu anakutumia pesa na yeye unamtumia, sasahivi anataka kuja kwako unamuambia Mkeo, jomba upo Sawa kweli?

Huyo mwanamke una undugu naye?

Hujui anataka kuja kwako kuja kufanya nini?


Ndoa yako ina muda gani mkuu?
 
Back
Top Bottom