Wanawake wanapoogopa mimba kuliko UKIMWI

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933


Kuna mada kadhaa ambazo siku za karibuni hapa JF zimeelezea wanawake wasivyo makini katika kijikinga na magonjwa hatari kama ukimwi na kuachia kazi hiyo ifanywe na wanaume pekee, na wenyewe kuwa na woga tu wa kupata mimba kuliko ugonjwa wa ukimwi.

  • Pale mwanamke anapoonekana kumeza vidoge vya kuzuia mimba baada ya kufanya ngono dalili wazi ni kwamba hakuwa makini kujikinga zaidi kupata mimba na yuko radhi kwa ukimwi, kinachofanywa ni kuogopa mimba zaidi.

  • Pengine dalili ni wale wanawake ambao hugeuza ngono kama bidhaa na pale wateja wanapotaka sharti la kuwapa pesa nyingi ni full kwa pekupeku kwa kwenda mbele na baada ya tukio kuishia kumwonea huruma akipaparikia kutafuta vidonge vya kinga ya mimba badala ya kufikiria maambukizi ya ukimwi.


  • Biashara ya ngono mfano wanaume wanaijeria wanaiweza kumkomoa mwanamke kwa kuridhia mapenzi na wafikapo kwao atakutana na jopo la vijana kadhaa bila condom hapo kila mmoja afaidi kadiri ya uwezo wake, nani ni salama wanajuana wenyewe, ila mwanamke yatakayompata ni kuhangaikia vidonge vya mimba badala ya hatari ya ukimwi.

Muhimu umakini, tusiwe kama wanyama ambao wamekuzwa miili yao bila ukuaji wa self control lakini wamejaliwa nguvu za silika zinazowakinga, wanyama hawafanyi ngono zembe kama binadamu.

Binadamu tumejaliwa akili na utashi lakini wengi tunaonekana kukua kimiili bila kukua kimaadili na self control.

 


Kuna mada niliileta hapa JF siku za nyuma ikieleza athari za matumizi ya vidonge vya kuzuia mimba, madhara yake makubwa kiafya licha ya kusababisha kusuasua au kuharibika kwa mimba mtumiaji napokusudia kupata mimba baada ya kuachana na matumizi ya vidonge vya majira.

Soma zaidi: Kinga ya mimba na madhara yake kwa wanawake

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…