Wanawake wanapokiri kuwa ni waongo!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,335
Sio mimi Mtambuzi, bali hata utafiti uliowahi kuripotiwa kwenye jaridala That's Life! ambalo huaminika kwa kuandika habari za wanawake ulithibitisha juu ya jambo hili.

Imebainika kwamba, wanawake wengi wako tayari kudanganya kwenye jambo lolote maishani mwao. Nusu ya wanawake huwa wanadanganya karibu kila siku katika masuala mbalimbali.

Lakini pia imebainika kwamba, wanawake tisa katika kila kumi huwa wanadanganya kwa mambo ambayo wala hayana maana, yaani mambo ambayo mtu anashindwa kujua ni kwa nini wadanganye kuhusiana nayo. Kiasi cha wanane kati ya kila kumi, huwa wanajua kwamba, wanasema uongo, lakini uongo huo husemwa ili kuchokoza hisia za wengine. Hata kulia kwa uongo ili kuvuta hisia za wengine hutumiwa sana na wanawake.

Susan Quilliam, ambaye ni mtaalamu wa saikolojia anasema wanawake wengi kuongopa ni dalili kwamba wanashinikizwa na maisha ya kifamilia, kikazi na hata kwenye uhusiano. Kwa hiyo, hudanganya ili waweze kukabiliana na mazingira hayo magumu, ili waweze kuishi kwenye maisha haya ya kasheshe.

Lakini, Je, wanawake hudanganya kwenye mambo yapi hasa? Haya yafuatayo ndiyo ambayo wanawake hudanganya sana kuhusiana nayo. Kuna ununuzi wa vitu. Huonesha kwa waume zao kwamba wamenunua vitu kwa bei rahisi wakati siyo. Hudanganya kuhusu fedha, kuhusu mahali walipokuwa, kuhusu kuwa wanaumwa wakati siyo, kuhusu hisia zao, ambapo husema wanampenda mpenzi wakati siyo.

Kuhusu kunywa pombe, husema hawajanywa au hawanywi, wakati wamekunywa au ni wanywaji wazuri, hudanganya kuhusu uhusiano wao wa nyuma, na mengine ya aina nyingi tu. Kuhusu mapenzi, wanaume ni waongo zaidi , lakini kuhusu masuala mengine ya kimaisha hasa fedha na vitabia vingine, wanawake hawaaminiki kabisa.

Ukitaka kujua mengi juu ya jambo hili waweza kubofya hapa:
To tell the truth, women lie | Mail Online
 
Evarm

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
1,862
1,266
Thank you mtambuzi labda ni kweli usemayo, ngoja tuwasubiri wadau
 
Tegelezeni

JF-Expert Member
Dec 31, 2009
268
124
Mimi nasema hivi...Na asiye muongo na awe wa kwanza kunyanyua jiwe kumpiga Bwana Mtambuzi.........LOL
Ukweli ni kwamba hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuja hapa akadai kuwa hajawahi kudanganya hata mara moja, nadhani atakuwa ni kiumbe wa ajabu kabisa.
Kuna tofauti kutoka uongo mmoja hadi mwingine, kuna uongo wenye madhara na ule usio na madhara................ kama tukisema ni upande gani unaongopa zaidi kati ya KE na ME........ KE hudanganya zaidi na huo ndio ukweli wenyewe.............
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,335
Kweli kabisa ila binafsi nitadanganya vyote ila sio mahusiano.

Hilo eneo la mahusiano haliikwepeki kudanganya, kama umefanikiwa kumudu kutodanganya............... nakupongeza bibie.......
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,474
6,538
Aksante Mtambuzi uzuri sababu za kufanya hayo zimeainishwa so tuache kumtupia mawe mkosaji. Mwanamke/mume mwongo amefanywa hivyo kutokana na mazingira yanayomzunguka. Mfano kama anaishi na mwanaume asiyemuamini anayemchukulia kuwa ni mfujaji tu wa pesa.....ukiulizwa hicho kishida umenunua bei gani, (knowing kuwa nachukuliwa mfujaji- nitasema shilingi 500 ilhali ni 5000. Na hasa kama ni mahusiano ambayo yana kijiharufu cha abuse.
 
Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,787
9,115
Hilo eneo la mahusiano haliikwepeki kudanganya, kama umefanikiwa kumudu kutodanganya............... nakupongeza bibie.......

nikikudanganya saa nimenunua mia tano wakati nimenunua alfu moja impact yake ni ndogo ukilinganisha na nikisema nipo single wakati nimeolewa. Kwahiyo kwenye mahusiano nipo muwazi sana ili nisicreate matatizo.
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,801
24,508
umenena vyema, wanawake tunadanganya kuhusu vitu ambavyo sio vya msingi. ukimuuliza mwanamke most probably atakudanganya kuhusu umri, weight na height. anaweza kukudanganya kuhusu kipato ili usimchune, kuhusu kunywa pombe na # of exs. ila hawezi kukudanganya kua yuko single wakati ako married, au hana watoto wakati anao.. ila sasa wenzetu nyie mtu anadanganya hadi kabila,dini, marital status ndo usiseme.
 
Vin Diesel

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
9,095
6,327
Kudanganywa kunauma sana...hasa kwenye mahusiano...
Awezae kudanganya kwenye mambo madogo hata makubwa anaweza kukudanganya pia...
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,335
.....ukiulizwa hicho kishida umenunua bei gani, (knowing kuwa nachukuliwa mfujaji- nitasema shilingi 500 ilhali ni 5000. Na hasa kama ni mahusiano ambayo yana kijiharufu cha abuse.

Duh...........Oh no...... this is too much, yaani kutoka 5000, unapunguza mpaka 500............... hii hata mimi sikubali, jamani mdanganye lakinin uongo ufanane na ukweli japo kidogo................
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,335
umenena vyema, wanawake tunadanganya kuhusu vitu ambavyo sio vya msingi. ukimuuliza mwanamke most probably atakudanganya kuhusu umri, weight na height. anaweza kukudanganya kuhusu kipato ili usimchune, kuhusu kunywa pombe na # of exs. ila hawezi kukudanganya kua yuko single wakati ako married, au hana watoto wakati anao.. ila sasa wenzetu nyie mtu anadanganya hadi kabila,dini, marital status ndo usiseme.

Hiyo ya kudanganya kuhusu mtoto, ninao ushahidi wa dada mmoja alikuja kwangu kutaka ushauri, zaidi ya miaka 5 ya ndoa ukijumlisha na miaka miwili ya uhusiano kabla ya ndoa ambapo unapata miaka 7 tangu ajuane na mumewe, alimdanganya kuwa hana mtoto, in the begining ya uhusiano wao.............jambo hiilo linamtesa hadi leo, anaishi na huyo binti yake lakini amempiga marufuku kumwita mama na anamwita Shangazi........ alitaka nimsaidie namna ya kumweleza mumewe. nikiwa kama rafiki wa mumewe, nilimsaidia, lakini mumewe amepoteza imani na mkewe kiasi kwamba ndoa yao iliyumba kidogo.
Jamaa aliuliza, kama aliweza kumdanganya kwa miaka zaidi ya 7 kwa jambo kubwa namna ile kuna mangapi ameshamdanganya?
Bado ana ndoa lakini haiko kama mwanzo...........imekuwa shaken.............
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,335
nikikudanganya saa nimenunua mia tano wakati nimenunua alfu moja impact yake ni ndogo ukilinganisha na nikisema nipo single wakati nimeolewa. Kwahiyo kwenye mahusiano nipo muwazi sana ili nisicreate matatizo.

Hilo la kuwa single najua huwezi kudanganya juu ya jambo hilo, lakini, Je vipi kuhusu mahusiano yako ya nyuma waweza kueleza ukweli juu ya jambo hilo? I mean, if I ask "Have you ever cheated in your previous relationship?"................. wengi swali hili hawalitolei majibu ya kweli...........LOL
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
Mimi nasema hivi...Na asiye muongo na awe wa kwanza kunyanyua jiwe kumpiga Bwana Mtambuzi.........LOL
Ukweli ni kwamba hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuja hapa akadai kuwa hajawahi kudanganya hata mara moja, nadhani atakuwa ni kiumbe wa ajabu kabisa.
Kuna tofauti kutoka uongo mmoja hadi mwingine, kuna uongo wenye madhara na ule usio na madhara................ kama tukisema ni upande gani unaongopa zaidi kati ya KE na ME........ KE hudanganya zaidi na huo ndio ukweli wenyewe.............

Hapo kwenye red....... Walau uongo wao haupelekei maangamizi ya familia....HIV/AIDS, kufilisika na kutelekeza familia/watoto. Katika haya wanaume mwalimu wetu mmoja na tumekubuhu, Teteteteeeeeeeeeee. Kidume asimame apinge hili. Mweeeeeeeeeee!
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,474
6,538
Hilo la kuwa single najua huwezi kudanganya juu ya jambo hilo, lakini, Je vipi kuhusu mahusiano yako ya nyuma waweza kueleza ukweli juu ya jambo hilo? I mean, if I ask "Have you ever cheated in your previous relationship?"................. wengi swali hili hawalitolei majibu ya kweli...........LOL

Hili hata mie Mtambuzi nisingekujibu.............swali gani liko uchi hivi?? Tafuta vijikona kona vya kupindia lakini direct namna hii!! Kama nilicheat nitacheka tu na kukujibu kwa swali ingine mf. kwa nini unaniuliza hivyo? bna ukirogwa ukatoa sababu tu umekwisha hahahahahaha eti ah nataka tu nijue!! ntakurudishia we ulishawahi? Ukisema ndio narukia ehee ilikuwaje? of coz utalitolea maelezo ikiwemo na justification ya kuwa ulilazimika baada ya kunyanyaswa na mpenzio, bla bla blah by teh time unamaliza nshakuchomekea story nyingine

hahahahahaha
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,335
Hapo kwenye red....... Walau uongo wao haupelekei maangamizi ya familia....HIV/AIDS, kufilisika na kutelekeza familia/watoto. Katika haya wanaume mwalimu wetu mmoja na tumekubuhu, Teteteteeeeeeeeeee. Kidume asimame apinge hili. Mweeeeeeeeeee!

Mimi napinga bana.............kwa hilo wote KE na ME tupo sawa tu........
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,335
Hili hata mie Mtambuzi nisingekujibu.............swali gani liko uchi hivi?? Tafuta vijikona kona vya kupindia lakini direct namna hii!! Kama nilicheat nitacheka tu na kukujibu kwa swali ingine mf. kwa nini unaniuliza hivyo? bna ukirogwa ukatoa sababu tu umekwisha hahahahahaha eti ah nataka tu nijue!! ntakurudishia we ulishawahi? Ukisema ndio narukia ehee ilikuwaje? of coz utalitolea maelezo ikiwemo na justification ya kuwa ulilazimika baada ya kunyanyaswa na mpenzio, bla bla blah by teh time unamaliza nshakuchomekea story nyingine

hahahahahaha

Bora wewe umekiri ukweli, lakini ningefurahi kama Husninyo angejibu swali hili.............ngoja nimsubiri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Top Bottom