Wanawake wanapogeuka ombaomba...!

Wanawake wanapogeuka ombaomba...!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,438
DSC00444.JPG


Wanasaikolojia sasa wamebaini kwamba, mwanamke ana uwezo mkubwa wa kuvumilia kwenye hali ngumu kuliko mwanaume. Kwa hiyo, anaweza kuanzia chini sana, kwa kuuza muhogo wa kukaanga hadi akafika juu na kumiliki biashara kubwa. Lakini wanawake walio wengi wamefundishwa kwamba, wao hawawezi, hawana nafasi bali ni hadi waume zao wapende au wawasaidie mtaji. Mimi ninawajua wake wa watu wenye uwezo kifedha ambao, mmoja alikuwa akipika maandazi na kuyasambaza kwenye mighahawa kadhaa. Hivi sasa huyu mama anamiliki mghahawa mzuri na maarufu huko mkoani Arusha.

Mwingine alikuwa anatengeneza na kudarizi vitambaa vya mezani kwa miaka tisa, wakati mumewe angeweza kumpa mtaji mkubwa zaidi, kwani alikuwa na uwezo. Lakini hakukaa kusubiri mumewe ampe, aliamua kufanya kwa kutumia akili na mwili wake. Huyu mama hivi sasa anamiliki duka kubwa la nguo za kike na watoto hapa jijini Dar. Kwa nini waliamua kufanya wenyewe, tena kwa kuanzia chini, bila kusubiri waume zao? Kwa sababu wao ni binadamu kamili ambao wanaweza sawa na wengine. Waliamua kuweza siyo kusubiri kuwezeshwa. Kwani hata wanaume ambao wanapata fedha au mali si wameanzia mahali fulani! Mtu anasubiri kupewa hajishughulishi, halafu anatarajia atendewe haki! Utatendewa vipi haki nawe ni ombaomba ambaye unaamini kwamba, kuomba ndiyo haki yako?
Mama+lishe+8.jpg


Kuna wanawake ambao ukiwatazama, utagundua kwamba, wanaamini kuwa waliletwa hapa duniani kuwasubiri wanaume wayafinyange maisha yao kama wanavyotaka. Kwa hiyo, badala ya kutenda, badala ya kuanza kujitafuta, wanasubiri waume zao wawape mitaji. Wengine wanapewa kweli hiyo mitaji, lakini wanalipia puani fadhila hio. Naita fadhila kwa sababu hakuna mahali ilipoandikwa kwamba, mwanaume au mume anapaswa kumpa mkewe mtaji au kumtafutia kazi. Ninachojua mimi ni kwamba kila mtu ameletwa hapa duniani kuja kuishi kama yeye. Kwenye zile ndoa ambazo wanawake hawako tayari kuthubutu, hawana ubunifu wowote na wanasubiri waume zao wawafanyie kila kitu, hata kuwaambia wafanye nini, hakuna amani. Hakuwezi kuwa na amani kwa sababu wanawake kama hawa wana utegemezi kwenye kila kitu, ni wavivu wa kufikiri na kutenda. Unaweza kushangaa hata kulea watoto kunawashinda.

Mwanamke hana ajira, hana shughuli yoyote ya kumwingizia anayofanya, lakini anashindwa hata kuwasaidia watoto wake kufanya homework jioni. Kazi yake ni kuzurura na kutafuta umbea au kutafuta kusifiwa kwa kuvaa dhahabu kochokocho na nguo za fasheni. Na ndio maana wanawake wengi waume zao wanapokufa hawalii kwa sababu wamepoteza wenza, wamepoteza watu waliokuwa wamezoeana nao…………, hapana. Wanalia kwa sababu hawajui waanzie wapi, waguse na kupapasa wapi. Wanalilia nafsi zao, siyo za marehemu wao. Kwao kufiwa na mume ni sawa na kufa wenyewe. Wengine husema kabisa, ‘umeniachia watoto, sasa nitawalea vipi?’
DSC06465.JPG


Unataka kusema wewe ulikaa tu, hukuwa na mchango wowote kwenye kulea watoto wenu! Na ni kwa nini usiwe na mchango mkubwa kuliko wa mumeo katika kuwalea? Ni kwa sababu uliamua kujifanya nusu-mtu! Kila binadamu anaweza kufanya lolote, kila binadamu anaweza kuyakabili maisha kwa namna anavyotaka na kumudu. Lakini wanawake wengi hawakulelewa na kufanywa kuamini hivyo. Wanaamini kwamba, wanaume ndiyo wanaoweza na wao wamezaliwa ili kuwa wategemezi. Hiyo si kweli, ingawa kwa wanawake hao inaonekana kuwa ndiyo ukweli.

Ni kweli kwamba, wanawake wamenyimwa nafasi nyingi na wamefanywa raia wa daraja la pili na mfumo-dume. Lakini kwa leo kuendelea kujikunyata na kusubiri waume zenu wawafanyie kila kitu ni dhambi kubwa. Kuna idadi kubwa ya wasomi ambao mama zao waliwasomesha kwa kuuza maandazi na vitumbua. Kuna mama namjua ambaye mumewe alikuwa hajui kama kuna kitu kinaitwa kutunza familia. Huyu mama aliweza kwa mwili na akili yake kuhangaika hadi watoto wake wawili kati ya sita wakafika chuo kikuu. Hakuwa mwanamke msomi wala hakuwa na ajira. Alikuwa na moyo mkuu wa kutumia nafasi za kutafuta maisha alizoziona na kuzibuni. Unaweza kushangaa, mume anakufa mwanamke anaachiwa mali. Kwa sababu hajui chochote, hakuwahi kuhangaika kujua namna ya kutafuta, anatafuta mwanaume au mume mwingine ili amsaidie kusimamia mali. Mwanaume huyo anamtapeli mali zote na kumwacha akijikung’uta.

Mwanamke, simama mwenyewe, anza leo kujituma hata kwa kuuza maji.
 
Uombaomba wa akina mama hasa kwa Tanzania umejikita kwenye ubunge wa kupendelewa maarufu kama ubunge wa chupi. Walioko chini ni kutowezeshwa tu. Nadhani dawa ya kuepukana na hili ni kuubomoa mfumo dume. Hata hivyo mambo yameanza kubadilika. Ushahidi ni kiduchu ni jinsi humu JF vijana wengi wanavyotafuta mijimama ya kuwalea. Zama zetu hili lisingewezekana na kama lingetokea basi wazazi wako wangekuwekea mkwara wa kukukachia laana na ungeachana na shipa hilo. Kwa sasa ni tofauti.
 
Somo zuri. Ila hujatupa mbinu ya kuepuka kutapeliwa. Ni kuwa mchungu kama mhogo mchungu, wallet yangu ina passcode!
Haya, ombaomba mwingine huyu wa mbinu. Hili neno 'tukiwezeshwa twaweza' ndo linawaharibu kabisa. Na hii imani ya 'mfume dume' ndo inawapa upofu kabisa kwenye kufikiri. Wanawake ni wazuri sana wa kutafuta 'eksichuzesi'.
 
Haya, ombaomba mwingine huyu wa mbinu. Hili neno 'tukiwezeshwa twaweza' ndo linawaharibu kabisa. Na hii imani ya 'mfume dume' ndo inawapa upofu kabisa kwenye kufikiri. Wanawake ni wazuri sana wa kutafuta 'eksichuzesi'.

sijakuelewa kabisaa. Na kati ya siku ambazo nina akili timamu ni leo manake sijavuta bhange toka jana. Unamaanisha mimi ni omba omba amaa?
 
Huu ugonjwa kidogo kidogo unaingia kwa the young men wa this generation jamani...mpaka inaboa yani!***..........yani ni wavivuuuu!!!!!! kila kitu 'baba...mama...bi mkubwa hajantoa leo...pambafff'

si bora wewe unawasikia wakilalamika hawajatolewa. Sie tunaofuatwa kuombwa ombwa? Utaskia mie nakupenda, nitakupa raha, afu wewe una hela najua utanitunza na kunisaidia mengi. Vijana wa siku hizi, no wonder wadada hawapati waume wa kuwaoa. Manake wenyewe vijana wanasaka waume!
 
kumegwa ni kawaida yao, inakuwa shida wanapoamua kutumia kawaida hiyo kuwa bidhaa iuzwayo. Kwani kama mwanamke amejitosheleza huwa hamegwi?
muulize mpenzi wako! alafu kwanini wamegwe tu j.mosi na j.pili na siku za sikuu
 
muulize mpenzi wako! Alafu kwanini wamegwe tu j.mosi na j.pili na siku za sikuu

ni katika kutimiza a biological needs, nimesema ubaya ni pale wanapovuka malengo kutoka biological needs hadi kwenye masuala ya kipato. Kwani wenye nazo j. Mosi na j.pili hawamegwi?
 
Uombaomba wa akina mama hasa kwa Tanzania umejikita kwenye ubunge wa kupendelewa maarufu kama ubunge wa chupi. Walioko chini ni kutowezeshwa tu. Nadhani dawa ya kuepukana na hili ni kuubomoa mfumo dume. Hata hivyo mambo yameanza kubadilika. Ushahidi ni kiduchu ni jinsi humu JF vijana wengi wanavyotafuta mijimama ya kuwalea. Zama zetu hili lisingewezekana na kama lingetokea basi wazazi wako wangekuwekea mkwara wa kukukachia laana na ungeachana na shipa hilo. Kwa sasa ni tofauti.

Umesema kweli mkuu, na ndio sababu katiba mpya inatakiwa iyaangalie yote hayo.
Hakuna tena viti maalum wala nini ili kila mwanamke akomae mwenyewe kwa kijipima ubavu wake bila kutumia rushwa ya ngono
 
wanawake wameumbwa ivyo yani....kuomba omba ni nature yao,yani ata awe na nini lakini atataka kuomba apate zaidi maana hawatosheki na walichonacho wana tamaa sana.
 
Asante sana Mtambuzi kwa somo zuri, mimi mwenyewe ni ushuhuda tosha katika familia yetu tupo watoto watatu na wote tumefika chuo kikuu kwa nguvu za mama yetu mpendwa ambaye alisimama kidete kuhangaika kwa ajili yetu alijinyima sana na Tunamshukuru Mungu watoto wote hatukumuangusha kwenye elimu.I truly love my mum I have learn alot from her life
 
Bravo Mtambuzi. Ki ukweli siku hizi unakutana na mtu hata kwenye dala dala anakuuliza unafanya kazi wapi, ukisema huna kazi unatafuta na story inaishia hapo. Ebu tuwe waungwana. Hivi unapomfanya mwenzio kama pochi, as if yeye hana kazi na hela yake inakuwaje?

Tuache tabia za kujinga, hasa wanaume siku hizi mmekuwa na tabia za ajabu mpaka mnafikia hatua ya kuingiza mikono kwenye pochi za masugar mami zenu kuiba hela. siyo lazima uwe na biashara kubwa sanaa, cha kufanya angalia kinachowezekana ili uanze taratibu mpaka ufikie level ya kuwa mfanya biashara mkubwa.

Ndiyo maana hatuolewi wala kuoa, nani anavumilia tabia za kishenzi kama hizi? Mtambuzi tupe mbinu za kujikwamua, hii thread ilikuwa vya kutuamsha toka usinginzini
 
Back
Top Bottom