Wanawake wanaodharau watu soma hapa

Wanawake wanaodharau watu soma hapa

hii ni STORI TU...hakuna ukweli wowote ule!
 
stori inafundisha,
mwenye masikio na asikie!!!but in life we should learn to play safe

huwa nafurahi tu nikisoma michango yako yenye mafundisho. Inakuwa kama vile umeniibia diary yangu niliyohifadhi data zangu.
 
yani mimi niolewe na mtu chini ya degree iyo ni big NO tunaanglia pesa,elimu na mambo mengine ndo yanafuata apa mwnaume mwny masterz na kuendlea ndo anapewa kipaumbele mambo cjui kuwa na ngoma cjui vitu gani maisha BAHATİ NASİBU na kufa ni kufa tu
 
Ndugu mwana JF hebu soma haka kastory kuna kitu cha kujifunza USHUHUDA.., ASOMAYE NA AFAHAMU!!
Naitwa Anna naishi Tabata, nimezaliwa
mwaka 1987 hapahapa Dar, nina Elimu
ya Chuo Kikuu.
Ninatoa ushuhuda huu uwe onyo na
fundisho kwa wadogo zangu na dada
zangu. Hapa nilipo ni mwathirika wa
Ukimwi. Niliokoka mwaka 2003 na
kwakweli nalimuona Bwana katika
maisha yangu ya wokovu, nilifurahia
maisha niliyokuwa nayo kwakweli,
washirika na Mchungaji walinipenda
sana na pia nilikuwa kiongozi wa sifa
pale kanisani.
Baada ya kumaliza Chuo na kupata
shahada yangu nilifanikiwa kupata kazi
katika Benki moja hapa hapa Jijini Dar.
Miaka ikaenda na umri wa kuolewa
ulipofika pale kanisani kulikuwa na
kijana mmoja alikuwa akimpenda sana
Mungu na kujitoa kwa huduma pale
kanisani, huyo kijana alitaka kunioa....,
nikakubali! Tatizo yule kijana alikuwa na
Elimu ya kidato cha nne na alikuwa
akifanya biashara ndogo ndogo ambazo
zilikuwa zikimwingizia kipato na kuweza
kuyamudu maisha yake ya kila siku.
Kuna wakati nilikuwa najaribiwa
nimwache kwani niliona hanifai kwani
mimi nilitaka mtu mwenye elimu kama
yangu au angalau anizidi na pia niliwaza
kuwa itakuwa shida kwangu kumtii na
kunyenyekea akizungumza kama
Kiongozi wa famila na wakati nimesoma
kuliko yeye, kweli hilo lilinitesa saaana.
Alipotaka kumwambia Mchungaji juu ya
mahusiano yetu nilimwambia tusubiri
kidogo tusomane tabia ingawa kiukweli
sikuwa na nia hiyo,,, nilikuwa nataka
kubuy time ili ikitokea kijana handsome
na msomi kuliko huyo atokee ili nibadiri
maamuzi. Kweli siku ikaja nikiwa natoka
kanisani siku moja kijana mmoja
tulikuwa tunasali naye alinibeba kwa gari
yake njiani kila mmoja alikuwa
kimyaaaa!!! Nikawa nawaza moyoni
kuwa huyu ndiye mwanaume mwenye
sifa za kuitwa mume wangu lakini
kamwe nisingeweza kumwambia kitu.
Safari ikaendelea tukafika nyumbani
akanishusha. Niliumiaaaa sana kwanini
hakusema neno lolote?????
Ikawa jioni kisha asubuhi siku nyingine,
siku hiyo nikiwa kazini simu yangu ya
mkononi iliita moyoni nikawa natamani
awe yule kijana. Kuangalia simu ilikuwa
ni ya yule kijana kweli, niliruka kwa
furaha bila hata kujua anaenda kusema
nini.., alinisalimu kisha akaomba anitoe
out siku hiyo.., nikwambie ndugu yangu
toka niokoke ndio mara ya kwanza
nilimsikia mtu akiniambia kutoka out, na
hapo nilijibu bila kufikiri mara mbili..,
YEEEEES!!! Alicheka akakata simu nami
nikabaki nimeishika ile simu mpaka rafiki
yangu pale ofisini aliponishtua akinitania
kuwa mapenzi yataniua kwani yeye
alijua naongea na yule mchumba wangu
kwani walimfahamu baadhi ya rafiki
zangu na hapo wapo walionitia moyo
kuolewa naye na wengine waliniona zuzu
kuwa nataka kuolewa na mtu
nisiyeendana naye kwani hakuwa na
cash ya kutosha.
Baada ya simu ile kiukweli nilishaanza
kumdharau yule mchumba wa mwanzo
hata sikutaka hata kuona simu yake
wala meseji, nikawa najibu nionavyo
ingawa yeye alikuwa mnyenyekevu na
siku zote alinitia moyo kuwa ipo siku
maisha yatabadirika na kuwa vile
nataka.., hapo tena sikutaka kusikia kitu
ila huyu kijana mpya.
Siku hiyo tumetoka out tulienda Serena
na hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza
kwenda hapo kufurahi.., tukiwa hapo
tuliongea mengi ila sikusikia lolote juu
ya mahusiano, nilianza kumchukia
kidogo kidogo. Baada ya masaa kama
mawili alisimama akaenda msalani, siku
hiyo ndo niligundua kuwa alikuwa ni
Mhasibu kwenye Kampuni moja hapa
jijini na alikuwa na Masters so hapo
niliona niko na mwenye sifa haaaasa!!
Ambaye nilijua ndugu, rafiki na hata
kanisani wakijua ndo mtarajiwa
nitaheshimiwa zaidi. Aliporudi yule
kijana alikaa kimyaa kama mtu
aliyekuwa akitafakari jambo.., akaniuliza
swali.., Anna will you marry me?? Kweli
nilingoja wakati kama huo ufikeeee..,
nilitabasamu.., nikajibu.., Yes baby!!
Alisimama akanikumbatia nami bila
kufikiria niliitikia. Alinirudisha home siku
hiyo nilikuwa na furaha sana.
Yule kijana alizidisha upendo kwangu
kweli nikajisahau kuwa nimeokoka..,
akawa ananichukua kwenda kwake
Mbezi Beach tukawa tunashinda wote
mpaka usiku, na wakati mwingine
nalipotoka kazini nilikwenda kwake bila
hata kusema, penzi lilipozidi tukawa
tunashiriki tendo la ndoa na kwa jinsi
nilivyompenda sikujali kwenda bila kinga
sembuse kuwa tutendalo ni dhambi
mbele za Mungu. Yule kijana wa mwanzo
alipoona vituko vimezidi aliniacha akaoa
binti mwingine.
Mchumba wangu mpya nikamwambia
tumwambie Mchungaji tuoane
akaniambia twende taratibu kwani mimi
ndio wake.., nilikubali japo kwa shingo
upande. Haukupita muda niliumwa sana,
nikalazwa hospitali VIPIMO
NILIVYOFANYIWA VILIONYESHA MBALI NA
MARALIA KALI NILIYOKUWA NAYO.....,
NILIKUWA NIMEATHIRIKAAAAA!!
Nililia kwa uchungu saaana, nikajichukia
na kumchukia sana yule kijana. Ajabu ni
kuwa yule kijana sikumuona tena kuja
kuniangalia wala baada ya kutoka
sikumuona kanisani tena. Mdogo wangu
na dada yangu, NIPO KITANDANI sasa
nikisubiria siku nitaondoka.
Nimeandika ushuhuda huu kukuonya....,
WEWE MSICHANA MWENZANGU...,
SIMAMA NA MUNGU....., MTANGULIZE
MUNGU KWA KILA JAMBO...., MACHO
YASIKUPOTEZE, ELIMU YAKO, PESA YAKO,
UZURI WAKO USIACHE VIKUPOTEZE.
MUHESHIMU MUNGU OKOKA KWELI
KWELI, KAMA WATEMBEA KWA IMANI
BASI AMINI JUU YA MUMEO MUNGU
ATAKUPA AFANANAE NAWE KWA VIGEZO
VYAKE NA SIO VYAKO WEWE.
USIMCHANGANYE MUNGU HUKU UKIISHI
MAISHA MACHAFU MTAANI, USIUFANYE
MWILI WAKO KITUO CHA UTALII KWANI
HILO NI HEKALU LA ROHO
MTAKATIFUUU!! USIMDHARAU MTU KWA
NAMNA YOYOTE LEO WEWE HUJUI KESHO
YA HUYO MTU...., YULE KIJANA
NILIMKATAA SASA NI TAJIRI ANA VITU
VYOTE NILIVYOKUWA NATAKA BUT NOW
IT'S TOO LATE KWANI NALITAMANI VITU
NISIVYOVITOLEA JASHO. KUBALI MTU SI
KWA VILE ALIVYO TU BALI PIA
ATAKAVYOKUWA BAADAE, KUBALI
KUANZA SIFURI NAYE MUINUKE PAMOJA,
LIENI NA KUCHEKA PAMOJA..,
MTABARIKIWA. NAPIGANA VITA NAMI
HAPA NIKIAMINI MUNGU AMENISAMEHE
NA SIKU MOJA TUONANE MBINGUNI.

Mhhhhh pole sana. Hi simulizi imenikumbusha mbali sana
 
huwa nafurahi tu nikisoma michango yako yenye mafundisho. Inakuwa kama vile umeniibia diary yangu niliyohifadhi data zangu.

hahaaa mi napendaga tukigongana hum ndani.......

i just love your presence in here
 
jamani for a single out will you marry me YEEES!!!!!!!!!!! LOOO!!!!!!!!!!
haya tunashukuru kwa ushauri tutaufanyia kazi.
 
Inafundisha saana kiukweli..., hata sisi wanaume a.k.a wazee wa ku point maana unaweza kumwacha Mtu mhimu kwako ukaangukia kwa mrembo mwenye elimu kumbe unawah makazi mapya.. Tuwe makin saana kwa ujumla,tunapo bebwa tusipengee mgongoni kamasi... I luv u wife.... Mwuaaaaaah

Kweli kabisa
hii post ni kwa wanaume pia,kuna wengine hawapendewi pesa wala elimu lakini matatizo matupu ndo maana wanawake wengine hutafuta kimoja as unaeza kosa vyote
 
I was in that kind o ship mm mda sasa umepita na nmeshamove on nlimzidi elimu kama hvyo bt alichokuja kunifanyia cna hamu nae so it depends bt 2sidharau watu coz mapenz hayaangali pesa,uzuri na elimu

kweli mdau mapenzi hayaangalii pesa kabisa nakubali. Mimi pia ni muathirika wa hilo, nilimpenda na kumthamini mno bila kujali kwamba hakubahatika kusoma hata secondary na wala pesa hana, nikampenda na nikampenda sana nikampa moyo wangu wooote wala sikubakiza aisee, nilimpenda nahisi mpaka yesu mwenyewe alishangaa,,, duuu alichonitendaaaaa!! akaniona takataka akasahau tulipotoka nikavumilia na nikavumilia saaana kiasi akaamini hata anifanye nini sina cha kufanya juu yake. siku ya siku ilivyofika (usiombe mwanamke achoke aisee) nikabwaga manyanga akabaki analia, sikuwa na la kufanya ni mapenzi tu ndio yaliyo tuunganisha, so yaliisha na isingewezekana tuwe pamoja tena. Moral of my story, mapenzi hayana formular fuata moyo wako tu. si umasikini wala utajiri mapenzi ya kweli hayahusiano na hivyo vitu.
 
umeona eeeh sipendi tajiri lakini sitompenda mtu kwa kumuonea huruma kisa maskini oooh atatoka kesho...kwanini usitoke leo?
mwanaume hatabiriki...wala hana shukrani..
kweli mdau mapenzi hayaangalii pesa kabisa nakubali. Mimi pia ni muathirika wa hilo, nilimpenda na kumthamini mno bila kujali kwamba hakubahatika kusoma hata secondary na wala pesa hana, nikampenda na nikampenda sana nikampa moyo wangu wooote wala sikubakiza aisee, nilimpenda nahisi mpaka yesu mwenyewe alishangaa,,, duuu alichonitendaaaaa!! akaniona takataka akasahau tulipotoka nikavumilia na nikavumilia saaana kiasi akaamini hata anifanye nini sina cha kufanya juu yake. siku ya siku ilivyofika (usiombe mwanamke achoke aisee) nikabwaga manyanga akabaki analia, sikuwa na la kufanya ni mapenzi tu ndio yaliyo tuunganisha, so yaliisha na isingewezekana tuwe pamoja tena. Moral of my story, mapenzi hayana formular fuata moyo wako tu. si umasikini wala utajiri mapenzi ya kweli hayahusiano na hivyo vitu.
 
kama ni kweli fundisho kubwa sana hasa kwa ulimwengu huu wa digitali
 
hebu nipisheni huko......huna pesa kaa kushoto....maisha yenyewe haya mara moja.....kufa ni kufa tu....kwa ajali......ngoma.......hata ghafla....mwisho wa siku wote tutadedi.......cha muhimu......funja mifupa wakati bado meno ipo.......huyo dada nae kashoboka....mtu akutoe out siku moja....akwambie.....will you marry me.....hushtuki.....huyo kajitakia mwenyewe.......analo hilooooo.......
Eti Preta, Yaani muanze na sifuri kisa unaogopa kufa kwani unajua salio lako au uliahidiwa utaishi milele hapa duniani? mnaanza na sifuri ikifika milioni anatafuta wengine aah wapi? nani kasema ukiwa nashda hautakufa? kifo ni kifo tu, na ukimwi hauchagua Masikini wala tajiri hata huyo masikini inawezeka na yeye anao anaishi kwa matumaini.
 
Back
Top Bottom