Wanawake wanahitaji mwanaume anayewapa uhuru. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake wanahitaji mwanaume anayewapa uhuru.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by DASA, Nov 4, 2011.

 1. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wanawake wanapenda sana kuwa huru na hii inafanya baadhi ya wanaume wasijisikie vizuri. Kutokana na mabadiliko ya maisha ya ,wanawake wanafanya kila ambacho kipo kwenye akili zao kwa ajili ya kuendeleza na kuimarisha familia, wanafanya kazi, wanafanya business, wanasafiri na pia wanafanya miradi yenye lengo la kuimarisha uwezo wa familia kiuchumi.


  Wapo wanaume huona haiwezekana mwanamke kufanya kazi za ofisini eti atakuwa huru mno kiasi kwamba atachukuliwa na wanaume wengine. Hayo ni mawazo ya kizamani na hayana nafasi kwa karne ya leo. Unamzuia mke hata kwenda shule eti atachukuliwa na wanaume wengine.


  Mimi naamini ni vizuri kumtia moyo kwanza awe anajiamini na kwamba anaweza kufanya jambo lolote akitaka kwani uwezo anao. Asipotiwa moyo na mume ni nani ataweza kumtia moyo ili ajiamini na kufanya mambo makubwa kwa ajili ya familia. Maisha ya sasa hivi yanahitaji wana ndoa ambao wanachakarika kwelikweli hivyo ni suala la kumpa mke wako uhuru ili muweze kusaidiana kuendeleza familia na maisha kwa ujumla.

  https://www.jamiiforums.com/newthread.php?do=newthread&f=62
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Umeongea points tupu ingawa kuna wanawake wengine wakipewa uhuru wanautumia vibaya.
   
 3. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Husninyo we hupendi kupewa uhuru!!!
   
 4. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tafiti kwanza kuhusu wanawake ndo uje na conclusion. Kwa kifupi wanawake wanamatatizo yao mengi tu. Wengi wanaona pale walipo tu. Kwa hiyo uwe makini na uhuru unaompa kwani kama mazingira yatakuwa yakumvutia kubadilika, usishangae siku unampigia simu anakuuliza 'Wewe nani? Unasemaje?'
   
 5. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Dah,mkuu kwa mara ya kwanza siku nzima ya leo nasoma sred yenye maneno matamu kwa mwanamke mungu akubariki sana.
  Hakika uliyosema ni ukweli mtupu kwan siku zote asilimia kubwa ya wanawake tukipewa uhuru na kuaminiwa hasa ktk mambo ya kuongeza kipato huwa hatufanyi makosa,na mafanikio huonekana.
  Tatizo hili la mwanaume kumzuia mkewe kujishuhulisha kwa kisingizio cha kuwa atachukuliwa na wanume wengine ni ulimbuken tu,
  Na wanaume wa aina hii huwa ndio wenye tabia za kutoka nje ya ndoa na hapo wanakuwa wanahisi watafanyiwa km wafanyavyo wao.
  Nakushukuru sana na ubarikiwe sana,na wikiend njema.
  Kumbuka kuvuta sigara ni hatari kwa afya yako(avatara yako)
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  napenda sana. We hupendi kutoa uhuru?
   
 7. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Aaah! Inategemea uhuru gani!! Loh!.

  Nampa uhuru mkubwa tu!! cha msingi ajiheshimu!!
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  basi vizuri. Nitarudi b'dae kuchakachua.
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180  thank you....
   
 10. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  AshaDii, vipi wewe huko uliko, kuna uhuru unakosa!!
   
 11. Wabogojo

  Wabogojo JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 355
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuna mzee jirani yangu aliwahi toa huo uhuru kwa maiwife wake kwenda kusoma mkoa wa jirani yaliyo mkuta baadaye ilikuwa siri ya wanandoa hao, lakini sasa si siri tena kwani hakuna tena ndoa kwa wawili hao japo wako pamoja baada ya mzee kubaini kuwa mama ana lipedeshee anatesa nalo.
   
 12. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Lakini na wanaume wanahitaji uhuru!!
   
 13. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Ishu ni huo uhuru wadada wanautumiaje? Ktk hii miaka ya karibuni nafikiri wadada wengi wamepewa uhuru ktk kuamua na kufanya wakipendacho.
   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  hatukatai kuwapeni uhuru...................tunachelea kuponzwa na maamuzi hafifu yanoyotokana na kutotambua nini maana ya uhuru tuliowapa...........nyie wanawake!
   
 15. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​ni kujiamini tu na kuacha wivu wa kipuuzi na usio na msingi
   
 16. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  eeh asante kwa kuliona hilo
   
 17. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Mimi huwa kila kitu akisema/akitaka kufanya wala simpingi,basi sasa anasema simpendi eti kwa nini hata sihoji!....na hapo ndio nashindwa kuelewa kabisaaaaaaaaaa.
   
 18. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  You think? Fanya analysis ya wanafunzi wanavyuo walio kwenye ndoa!
   
 19. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  juu ya mada hii naomba nitoe ushuhuda::

  ni mwezi sasa tangu nirude hapa tz....ndugu yangu wa karibu sana na na tuko nae idara moja yeye alimwamini sana mkewe tena na huyu ndugu yangu tuko nae mkoani huku tunafanya kazi huko dar ndiko amejenga na ambako mkewe anaishi lakini pia mkewe huyu alikuwa anasoma master na ile juzi ndo ametunukiwa siku ile ambayo na jk alipewa phd ya sheria ....

  kisa kilkuwa hivi ..mama yake na mke wa jamaa huyu alikuwa mgonjwa huko moshi..basi ndugu yangu huyu akamwambia mkewe aende moshi kumuona mama yake lakini pia apeleke mahitaji...mama akaenda moshi akakaa siku tatu..kwa kadri walivyokuwa wameongea na mumewe mke alipaswa kurudi nyumbani siku ya jumapili ....lakini mke huyu kumbe alikwenda kwao akalala usiku mmoja tu nakesho yake mama akarudi dar.... siku ya jumamosi kuanzia mida ya mchana simu ya mkewe ikawa hiko hewani...kwakuwa jamaa alikuwana imana kubwa na mkewe hakuna na shida.....usiku wa jumamosi ndugu yangu huyu alikuja kwangu tukala chakula cha usiku na tukawa tunaongea juu ya safari yanguna moja ya vitu tulivyokuwa tunaongea ni juu ya laptop yangu niliyoipata toka kampuni ya aple ilivyo na software za ukweli ambazo unaweza kulocate namba ya mtu na mahali alipo kikubwa kuwe na network....na nilimuonyesha kwa kwa baadhi ya namba za ndugu...usiku ule hakunieleza lolote juu ya habari ya mkewe kutopatikana hewani..nikamsindikiza akaenda kwake kulala...

  jumapili ya tareh 20 ambayo mkewe alitauwa kuwa njia mume wake alimpigia simu asubuhi sana ili kumuansaha awahi usafiri simu ikapatikana na wakajuliana hali vizuri na mke akamshukuru mumewe kwa kumuamsha.....kwa mujibu wa ndugu yangu huyu mke alipiga tena simu na kumwambi mumew sasa ndio tunaondoka moshi...mume akamtakia safari njema...

  mchana wa jumapili hiyo mimi na ndugu huyu tulikutana baada ya kutoka kanisani tukaa kwangu hapo badae akapiga simu ili kujua wapi mke wake amefika ..simu haikupatikkana..mimi nikamwabia ''mahali alipo hakuna network ndo maanaa hapatikanni....baadae mimi nikachukua laptop yangu nkawasha maana nilitaka kuchek news na mails....huyu bwana kuona hivyo akasema '' nami ngoja nikachukue yangu bwana ili niche mails na pia habari za mpira (ni mnazi wa aseno)

  aliporudi kutoka kwake akiwa na hiyo laptop yake akaiwasha mara gafla akaona mke wake yuko online kwenye skype...nikamsikia anaguna akanambia kaka namuona mke wangu yuko online hapa ina maana ameshafika dar tayari? mara gafla ile skyp ya mkewe ikawa offline.....jamaa akapiga simu ..simu haipatikani..mi nikakwambia kama alikwenda na laptop basi atakuwa ameweka moderm na sasa yuko eneo amabalo hallina net ndio maana amekuwa offline tena....ndugu yangu huyu alichezwa machale akasema..akaniuliza hivi hivi mtandao wa ttcl unashika tanzania nzima maana mke wangu ana moderm ya ttcl..mi nikamjibu kwa kweli sijui ....

  baadae akawa kama amestuka hivi akanambi kaka si laptop yako ina uwezo ku trace mahali alipo? nikasema inawezekana ila mpaka simu iwe hewani kama simu haiko hewani huwezi kujua.....baadae jamaa akapiga simu tena ikawa haipatikani baada kama ya dakika 10 hivi simu ikawa hewani lakini haipokelewi....ndipo hapo sasa ikabidi tuchukue ile namba na kuifeed kwenye laptop yangu...kwa kutumia gps na google earh latop ikaonyesha kuwa namba ya mtu huyi iko morogoro kwenye benk ya nmb karibu na kilipo kituo cha daladala... jamaa hakuamini....akapiga simu kwa mke wake simu haikupokelewa tena....alipopiga mata ya pili mke akapoke akasema..''baba devy nipigie badae kidogo ndo tunafika ubungi hapa ninashuka na akakata simu....baada ya kama robo saa hvi kwenye laptop huku tunaona simu ipo moro main road .....mi nikamwambia mkeo yuko morogoro na si dar...

  baada ya kauli yangu hiyo jamaa akapiga simu tena wakati huo kwenye laptop anaonekana yuko msamvu..mume alipopiga simu mke akapoke akasema sasa ndio naeleka nyumbani nimechukua tax hapa ndo tunatoka getini ubungo..kwa kuwa jamaa alikwa ameweka lod speker nami nisikie nilisikia..ndipo mume akamuuliza hivi'' na hapo morogoro musamvu unafanya nini?'' mke akakata simu na ilizimwa kabisa....

  ndugu yangu huyu alitokwa na jasho sana ikabidi nimtulize pale lakini haikusaidia...baada kama ya nusu saa alipotulia ilabidi sasa tufatilie nyendo za mkewe kwa kupitia simu ....ilinibidi nitumie simu yangu aina ya HTC smart phone ili niweze kudivert number ya yule mama laini pia inipe access ya kuingia kwenye inbox zake....badae nikaunganisha simu kweny laptop yangu na tukaziforwad meseji zote kwenye laptop na baada ya hapo tukaziprint.....hapo ndipo nilijua mwanamke mpe uhuru lakini sio asilimi 100.....yule mama ana hawara huko dar....ni muhni ile mbaya...ndugu yangu huyu alisoma sms 3 na moja iliyokuwa mbaya zaidi ilimata apate presha....mimi na jirani mwingine tukamkimbiza hosp amabo alipimzishwa kwa mda.....alipotoka hosptali na kurudi nyumbani na baadaya ushauri wa watu mbali mbali...ilibidi amuite mkewe aje huku mkoan na alipofika akapokelewa vizuri....na kesho uake mume wake akachukua zile sms alizoprint akampa mkewe asome..zilikuwa page 3 .....

  ndugu zangu bila talaka wala kuambiwa lolote na mume..mke alichukua uamzi wa kuondoka na kurudi kwao mpaka sasa yuko kwao


  je ni uhuru kiasi gani anapaswa kupewa mke???
   
 20. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135


  Loh! Hiyo software nitaipataje mjomba!! mana naona kama nataka kubadilisha mawazo! Loh!
   
Loading...