Wanawake wanadanganya jamanii

kwamtoro

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
4,922
Reaction score
3,245
Jumapili nilienda kiwanja cha mbali na mazingira ninayoishi kujirusha.

Nilipofika mda fulani hivi bila ya kutarajia nikamuona mpenzi wa rafiki yangu na mwanaume mwingine wakiwa kwenye romance.

Nikastuka hivi, aliponiona nikamuona kajisikia hana amani nikahisi atakuwa labda alimdanganya rafiki yangu. Akaninulia kinywaji nikakireject.

Kijana aliyekuwa naye akawa ananiangalia sana huku akiwa confused.

Kwa masikio yangu nikamsikia shemu akimwambia kwamba mimi ni kaka yake mkubwa.

Jana asubuhi shemu akanipigia simu na kujichekelesha. Ohh yule ni binamu yangu, please usimwambie jamaa coz ataniua kwa vile nilimdanganya nipo kwa shangazi sitokuwa nyumbani. kwamtoro please I love your friend so deeply yaani.

Nilichoka!

Na hasa nikikumbuka uwongo mwingine wa wanawake, nikaamini kweli wanawake waongo sana.
 
Ukitaka ufurahi zaidi fanya udadisi ili ujue alimuagaje rafiki yako siku hiyo, hapo ndipo utajua kuwa wanawake ni noma!!
 
ila jitahid bana, usimwambie rafik yako teh teh
 
ha!ha!haaa!uwongo tabia ya mtu haijalish mwanamke ama mwanaume!!!
Na kilichokuja kuongeza zaidi uongo ni hii teknolojia ya simu za mkononi. Mtu anakuwa Kibaha anabanjua amri ya sita ukimpigia anakwambia wana kikao cha ukoo kwa baba mdogo kinondoni!!
 
Shetani kauteka ulimwengu kila nyanja.

Lakini hii ni wote tu maana hata huyo jamaa atakuwa ana ki date chake amekidanganya..

Inauma kuibiwa aisee..
 
Na kilichokuja kuongeza zaidi uongo ni hii teknolojia ya simu za mkononi. Mtu anakuwa Kibaha anabanjua amri ya sita ukimpigia anakwambia wana kikao cha ukoo kwa baba mdogo kinondoni!!
ha!ha!haaa!mkuu na mi nimeongopa hvyo hvyo leo umeniona nini?
 
Ili usijiingize kwenye hilo kundi la waongo vunja ukimya liwalo na liwe
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…