Wengi wachangiaji wa maada hii wamesema wajawazito wengine hizi fujo wanazoleta wanaigiza aisee mimi nakataa kabsa,Mimba ni noma kwanza hata akufanyie fuju kiasi gani huwez kumpiga km unabusara lkn,Ila ni muda mzuri sana wa kumliwaza wife kwa kuwa hichi kipind ni kigum sana na inahtaj moyo wa uvumilivu hapo ndio muda wake yy mke kudeka na kuona kama kweli unampenda na kumjali.....hii ndio fursa ingawa tunafukuzwa ndani kwamba Tunanuka ,wanatuchukia ,anakufokea yaani aaah mradi siku ziende tu....Nakumbuka mwaka juzi wife akiwa mjamzito yye alikuwa hatak kbsa kuongea na mimi,nikiwa hom anakula buyu,ila toka hatua moja simu hiyo eeh umeshaenda kwa Malaya zako wakat amekutuma kitu dukani, Ukiwahi kurud unasikia muda wote unashinda ndani siuende nje ukakae na wenzako haya ukienda dk2 simu hiyo utasikia na ulale huko huko. Usiku ndio kazi sasa yaani nikutafuna mchele mbichi na kutafuna barafu....jaman eeehh...Nashukuru nilimvumilia bahat nzuri kaniletea matwins mapenz yamerud km wachumba vile
Hahahahahahahah lol! Na wewe kwanini ulikuwa ukitumwa dukani unachelewa kwa kupitia kwa Malaya zako? Dah! hiki kipindi Wanaume inaidi kuwa na uvumilivu na uelewa wa hali ya juu ili kuepusha tafrani za aina yoyote na hivyo kusaidia katika ujauzito kuendelea salama salmini mpaka kujifungua pia kuwe salama. Kuna waume wenye bahati zao mimba miezi tisa haya yote huwa hawakutani nayo. Hongereni kwa mapacha.
Nakumbuka kipindi shemeji yangu (mke wa kaka) kapata mimba, alikuwa hataki kukaa na mumuwe akaja home, kipindi hiko nipo field trainning, yeye kila kitu mimi, nikienda sehemu anataka aende nami.
Nikipigiwa simu au kuongea na msichana njiani huyo binti atanuniwa, mimi nabaki kucheka. Nilikuw nina habit ya kufanya evening walk sasa mother kasem nenda naye afanye zoezi maana anakufata, pigisha route ndefu lakini hakomi kesho nafatwa tena.
Kimbembe asubuhi naamshwa niangalie nae CD za majuto 6am. Nisipo kuwepo hataki kula ( kama mimi ndo mumewe)
Nikarudi chuo akawa anatafuta excuse ya kuj, mara aseme home Hataki nile magengenu daily anapika ndizi au maandazi analeta nile anashinda room, Ikabidi niende na kurudi home kuepuka kumtesa na mim fulu kujishtukia
Ilikuwa kama movie mengi sana, ila after kupata bby boy akawa fulu aibu anasema kanisumbua sana.
Dah na kweli huyu imempendeza haswa,
Pole sana mpendwa! Unapita shida nyingiii mwisho wa siku unabaki mikono mitupu! Naelewa maumivu yako yalishanikuta pia!