Simplicity.
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 2,636
- 1,664
- Thread starter
- #21
Umeongelea kwa ujumla sana, nahisi hujakutana na wanawake wazuri, binafsi naamini ulikuwa unawaongelea warembo. Maana warembo ndio wengi wanakimbiwa kwa sababu ya kuwa artificial sana, na ukamtolea mfano wemaaa, huyo kwa mtazamo wangu ni mrembo na siyo mzuri.
Hata kama kuna wazuri (maana halisi niijuayo mimi), siyo wote huwa ni wagumu wakitongozwa, kama ulivyowachambua hao wabaya (kwa mujibu wa wewe).
Umejisahaulisha ya kuwa, tabia ya kuwa na wanaume ama wanawake wengi (umalaya), ni tabia ya mtu binafsi, sasa inaweza kuwa ni ya kurithi, kuiga toka akiwa shule / Chuo, kuinua kipato chake binafsi, ama tu kuambukiza magonjwa makubwa wengine ama Roho chafu wengine - na hili linafanyika siku hizi kama kisasi, labda naye aliambukizwa Roho hizo chafu ama magonjwa yasiyotibika.
Wapo wanawake walio wabaya (kwa mujibu wa wewe na wengi humu), ambao ni malaya ama siyo malaya, vivyo hivyo kwa walio wazuri / warembo (kwa mujibu wa wengi humu).
Uzuri na ubaya wa binadamu, anaujua Mungu, pekee na yeye anayo makusudi ya kuumba hivyo, ni sawa na waliozaliwa vilema, huwezi kumkosoa Mungu, katika hilo.
Tabia yake na Mwenendo wake Mtu, ndiyo inathibitisha ubaya na uzuri wake na siyo mengine tunayoyaongezea kibinadamu. Maana wapo hata hao unaowaita wazuri hawatongozwi (na hili husababishwa na vitu vingi), na pia hawajiamini.
Ahsante!
Nakubaliana na wewe kuhusu uzuri na ubaya anayejua ni Mungu, mimi nimeelezea kwa mjibu wa mitazmo ya watu. Lakini trend ya wanaume wengi wa kibongo sasa imekuwa ni kukimbia wanawake warembo, wakiamini hawajatulia. Tena hawaishii hapo, mwanamke akiwa mrembo, msomi au ana mali, wanaume wa kibongo ni mbio.