Simplicity.
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 2,636
- 1,661
Nimeona uzi mmoja, jamaa ameleta unaodai kuwa kwa nini wanaume wengi huoa wanawake wabaya? Nitatumia uzuri na ubaya kwa muktadha wenu.
Nataka tu kufundisha kidogo. Mwanaume anayeona mwanamke akampenda, lakini akasita kumuoa kwa sababu ni mzuri, kwamba atakuwa anatongozwa, HAJIAMINI, na ataishi maisha ya kitumwa mpaka anakufa.
Wengi wanadhani wanawake wazuri, wana tabia mbaya, mfano Wema Sepetu, Lulu nk. Hao kitabia ni exceptional na wameamua kuishi maisha yanayowapa picha mbaya kwenye jamii ili wazidi kuwa gumzo na hivyo kupata umaarufu.
Mimi nimewahi kuulizwa na wanawake, ambao watu wengi huwaona ni wa wastani au sio wazuri, maswali kama haya:
Hivi kaka, kwa nini sitongozwi? Au sura yangu haiwavutii wanaume? Yaani naweza kukaa hata miezi sita bila mwanaume kunitania!
Hivi unanionaje, mbona wanaume wakiwa na mimi hawanichangamkii kama wanavyochangamkia akina dada wengine?
Hivi wanaume huwa mnapenda wanawake weupe eehhh? (Akidhani uzuri ni weupe).
Ngoja niwape somo kidogo:
1. Kuna kitu kinaitwa status, hiki huwa hakitengenezwi. Ukiwa katika jamii kutegemea na status yako, unajikuta automatically huwazi wala hutegemei kuoa wanawake wa level fulani au wenye maisha fulani fulani, kwa sababu unaona mwendokasi wa level yao ya maisha huwezi kuendana nao, watakukimbiza. Sio kwa sababu watataka makuu, bali maisha yao ndivyo yalivyo, pindi utakapotaka waishi tofauti na walivyozoea, mtahitilafiana. Na mwanaume kwa kutojiamini na kuchukulia kuwa hiyo ni changamoto, atajijengea kuwa wanawake wazuri ni wasumbufu, malaya (utaanza kuhisi analeta usumbufu kwa sababu ya uzuri wake, au labda ana wanaume, lakini kumbe sio), wanaringa, nk. Sasa zingatia hili, wanawake wengi wanakuwa wazuri kwa sababu wana maisha mazuri. Wana vipodozi, wanakula vizuri, wanalala pazuri na vizuri, wana mahitaji karibu yote wanayotaka ambayo yanawafanya wajisikie vizuri hata kisaikolojia. Wapo wanawake wengi wazuri kiasili, lakini kwa sababu hawawezi kujiweka vizuri kutokana na uzembe wao au kutokuwa na mahitaji muhimu na ya msingi, utaona hata idadi ya wanaume wanaowaona wazuri ni ndogo. Chukulia mfano, Wema angekuwa anachunga ng'ombe kwao kijijini, ungemsikia popote? Ungejua kuna mwanamke anaitwa hivyo na ni mzuri? Wakati mwingine saikolojia inawahamisha watu kutoka kumwona mwanamke maarufu hadi kuona ni mzuri kwa sababu ya aina ya maisha yake, kampani, status, vitu anavyomiliki, nk.
2. Wanawake wazuri wanajiamini (ujasiri wa mwanamke upo kwenye uzuri wake, kama ulikuwa hujui, jiongeze). Sasa mwanamke wa hivyo, hasa ukikuta ana akili pia, mara nyingi wanajiamini na watakukosoa positively bila woga ikiwezekana kukuchallenge. Kwa sababu umezoea akina Mwajuma na Zaituni ambao ukiwaambia mguu pande, mguu sawa bila sababu ya msingi wanakutii, lazima utawaona wakorofi, mbaya zaidi usijikute una madhaifu na wewe, utakuwa unalia kuwa unaonewa au mwanamke anakuringia.
3. Wanawake wazuri sio malaya kama watu wanavyochukulia, kinachotokea mara nyingi ni kuonekana kama vile kuna wanaume wengi wanawafutilia au wanawataka na mara nyingi ni kabla ya kuolewa. Pamoja na wanaume wengi kuwatamani, huwa wanatolewa nduki, hawawapati kirahisi, kwa sababu wanawake wazuri mara nyingi huangalia vigezo vya mwanaume wanayemtaka, sio kila mwanaume. Jambo hilo hufanywa tofauti na wanawake wabaya. Wanawake wazuri wakiolewa, huwa kama vile wanaishi kwenye ngome ya mfalme, kwanza interaction na watu ovyoovyo hawana na hujijengea security nzuri sana wanapopata mtu sahihi, na wanaume wakwere mpaka wapate mwanya wa kuwatongoza tu, hupoteza sana muda na rasilimali nyingi, na mara nyingi hawafikii lengo. Kwanza wanaweza kukushushua mpaka ukimbie: "Hivi wewe unajiona ni hadhi yangu?", Unaumwa? etc., pindi unapojaribu kuwatongoza, utaishia kusema samahani sista. Hata inapotokea wamechepuka hufanya kwa staha na tahadhari kubwa mno kiasi kwamba mme wala watu wengine hawatahisi. Sio kama akina Pili au Swaumu, unamwinamisha tu hata uchochoroni. Ndio maana sio rahisi kuona kuna kundi linajiandaa au kupanga kwenda kufumania mtu akiwa na mwanamke mzuri hata kama ni wa mtu, hali ni tofauti na akina Undulile ambao kila leo wanafumaniwa!
4. Bottom line: Rejea maswali yangu niliyoulizwa na wanawake ambao nyie mnawaita wabaya. Sijawahi kuona katika maisha yangu wanawake wasiojiamini kama hao wabaya (kwa mjibu wako). Ikitokea mtu akamtongoza, huwa ni kama surprise kwao na kukataa ni kama kutupa bahati. Huwa wanajishangaa na kujiuliza, huyu ananitongoza kweli au ananitania? Mbaya zaidi anayemtongoza asije kuwa ni mwanaume mwenye status yake ya maana (na labda ni handsome - kwa mjibu wako)! Wanawake hawa wakati mwingine wako tayari kumnunua mwanaume. Ili kucompensate uzuri wao, hujitahidi sana kuwa wachapakazi na kusoma kwa bidii ili na wao wawe na kitu fulani kinachowatambulisha maishani, maana kama uzuri hawana watajivunia nini sasa? Ndio maana kwenye social media wanaoongoza kupost picha za ajabu, ambazo kwa akili zao wanadhani zitasaidia kuvuta hisia za wanaume! Wakuipost nawe ukacomment umependeza, watarudi tena na tena kuangalia hiyo comment, na kuona kama kuna zingine za aina hiyo, usiku watalala wakiota, na ikitokea ukajichanganya kutongoza, ndio hao ambao huwa hawahitaji hata utumie condom, lakini uwezekano wa wewe kumkana mbeleni ni mkubwa!
Note: Mwanamke mbaya frequency ya kutongozwa ni ndogo lakini hana stamina ya kuhimili au kukataa kwa sababu kwake ni kama "zali". Mwanamke mzuri mnawaweza kutongoza 50, mmoja ndio akabahatika baada ya muda mrefu, kwa nini msiwaone wanaringa? Ili uone kuwa wanawake wazuri ni expensive, je, wewe sio shahidi hata kukaribiana nao au kupata tu mawasiliano yao ni kazi? Wakati akina mwanahamisi unawapotezea na namba zao unazifuta kila siku? Tena wanakung'ang'ania? Mnawapa mimba mnawakimbia, kwa nini?
Go ahead and make your choice.