Wanawake wa kisasa na tatizo la "Double standard"

Wanawake wa kisasa na tatizo la "Double standard"

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,093
Reaction score
22,806
Hivi wanawake kwa ujumla wenu mna udhaifu gani kwenye ile sehemu ya kichwa inayohusika na kufanya maamuzi sahihi.......?!

Nauliza hivi kwasababu mamsap ananionyesha elementi ambazo hata nashindwa kuzielewa.

Ipo hivi - few months ago alikuwa ameomba kazi TRA na alifanikiwa kupata mualiko wa usahili.

Kama mwanaume responsible nilijitahidi kadili ya utashi wangu uwezavyo kumnoa ili afanikiwe katika usahili wake wa kwanza katika taasisi ya serikali.

Alifanya na kufanikiwa kupita katika usahili na hivi navyoongea yupo mzigoni. Sasa few days ago baada ya kupokea pay mara kadhaa simuelewi haiba yake maana si niliyoizoea.

Kwanza tumeanza kubishana kuhusu mawasiliano na wafanya kazi wenzake wa kiume.Huwa anaendekeza mawasiliano hata yasiyo na uhusiano na kazi just mazoea ambayo mimi siaprove.Mfano ni siku nilikuta ujumbe umeandikwa "Mambo bi dada,missing you swty" na "yeye alijibu hii text"poa niaje my"!

Zingine ni chat kati ya yeye na rafiki zake kujadili mbwembwe za wafanyakazi wenzao wa kiume ikiwemo yeye kuthubutu kusema " G ni handsome akikutaka unakataaje".!

Text ni jingi kwakweli ambazo nikiziweka hapa zitajaza thread nzima ila maudhui yake yanaashiria kuwa kuna mambo siyo yanaendelea huko kazini kwao.

Pili ni hii tabia ya jeuri ya kuwasiliana ameanza,ananiambia huwa anakuwa tight na kazi tokea anapoingia mzigoni hadi anavyotoka huwa anakuwa free muda tu wanapumzika saa saba hadi saa nane lakini cha ajabu wapendwa ni kuwa hakuna siku anathubutu nitext kusema chochote kile ndani ya huo muda yaani labda nianze mimi ila cha ajabu nikicheki kwenye simu yake huwa kuna conversation zinaonyesha alikuwa anachat muda huo anadai anakuwa busy na hata ule wa mapumziko.

Sasa hili la juzi kati ndio limenikata stim hadi nimeamua kufanya ninachofanya now.Tulipokuwa faragha yakamtoka maneno ya kunikera sijawahi msikia kasema.Akasema kuwa muda mwingi huwa hajisikii kufanya mapenzi yaani hisia zinagoma kabisa.Nikamuuliza kwanini anasema hivyo akadai basi tu inamtokea huwa anajisikia mara chache sana pengine nikiwa nimesafiri ndio huwa inakuja lakini nikiwa around ni mara chache sana stim zinakuja.

Nikaona huyu pepo la umapepe linaanza kumshika kichwa so nikampiga swali hivi.''Kwa hiyo stim za kutupiana zimekata baada ya kuanza kazi sio,maana hata text siku hizi utadhani nakutongoza unavyojivunga kureply.

Haya nikamwambie anitolee ufafanuzi kuhusu text zote zile za kipuuzi nilizohack kweny inbox yake.Majibu yake sikuridhishwa nayo maana ni aidha nilipewa nusu ukweli au niliambiwa ukweli lakini sio kwakuwa alikuwa anaconfess ila tu ni kwasababu nimemfuma.!

Basi mimi nikalala zangu nikamuacha ameduwaa pale maana akavuta picha na kujionea kuwa amebadilika kweli na amenikosea heshima sana mume wake. Basi akajifanya kulia pale kinafiki na samahani mara elfu mimi wala nikakausha maana hawa watoto wa kike wa siku hizi sijui nani ni kunga wao.

Asubuhi ikafika akajiandaa akapanda kitandani tena kunisihi nimsamehe na atajirekebisha mimi nikamwambia wewe zingua hapo uchelewe job.Basi alipoona simpi ushirikiano akaondoka kwa huzuni.

Nilikisikia vibaya maana hata sikumsindikiza kama ninavyofanyaga siku zote.


Aliposepa nikaamka nikapanga baadhi ya nguo zangu nikaenda kwa mshikaji wangu maana yeye anaujua inshu nzima.Nikaenda kukaa kwake kwa zaidi ya wiki mbili naamkia huko kwenda kazini.

Muda wote huu mamsap alipata wehu wa kutosha maana aliponitafuta kwa mara ya kwanza kwenye simu baada ya kujua nimehama maskani nilimjibu kuwa "AM GIVING YOU A CHANCE TO CHOOSE BETWEEN MY PRESENCE OR MY ABSENCE IN YOUR LIFE"....text ambayo ilimfanya apige zaidi ya mara mia bila mimi kupokea na kunitext hadi inbox ikawa overloaded na conversation yake, kuwatafuta rafiki zangu wote. Mwisho wa siku alifanikiwa kwa kumwambia auntie yangu ma dada yake ambao walinisihi kumsikiliza na kumsamehe hakuthubutu kwenda kwa B mkubwa maana anajua angejichafua CV.

Nikarejea kambini,anajitahidi kuwa yule ninayemjua nyodo zimepungua.Ananitext hata ule muda wa kazi na sometimes ananiomba nimpitie job wakati wa lunch tukale sote.

Sasa hapa ndipo ninapojiuliza hivi kumbe wanawake huwa mnapenda kufanya mizaha ili wanaume tukichukua hatua mseme wanaume ni wakorofi!! Na haya ni matokeo ya kujipa double standard.Mnapokosea ninyi ionekane ni mwanamke anayepambana na mfumo dume na nimeshamwambia atakapoomba likizo tukaonane na wanapsychology wa mahusiano kama dk. Chriss Mauki ili wampe maneno kuntu na ufahamu wa maisha ya ndoa wakati wa ujana.

Wanawake hebu acheni michezo ya kitoto kwenye uhusiano!! If the guy is fair kwako treat him nice show some love n care kwa uwezo wako wote usipende ishu za tit for tut au ishu za mazoea in the end of the day hao marafiki na vijamaa unavyo flirt navyo ni hallucinations tu na zina expire date.

Sasa before haujampoteza life time companion wako just to satisfy the demands of that silly brated section of your brain hebu jaribu kugrow up na kuwa serious na life.

==========
Kwa wale wasiojua maana ya neno double standards tafsiri yake ni kuwa ni tabia ya kujipa thamani mara mbili zaidi ya stahili.Mfano mwanaume anapocheat ionekane ni okay but anapocheat mwanamke not okay.

Sasa kama unataka kujua ishu za double standards refer vituko vyote vinavyofanywa na wanawake now days kwa excuse ya payback kumbe ni utoto tu.

Hujachokozwa unarudishia.
 
Unajua kususa kijana, una muda gani kwenye ndoa? Mna mtoto?
Ndoa bhana!
 
Unajua kususa kijana, una muda gani kwenye ndoa? Mna mtoto?
Ndoa bhana!



Hapana bado hatujatafuta mtoto tunavuta muda kidogo tuwe na kwetu kabisa two to three years from now.........mtoto acheze kwenye sebule yao sio ya kwa watu.........ndio inakwenda mwaka wa tatu now.......but we r together tokea 2007........
 
Mwanaume unafunga virago na kuacha mji wako???

Anyway hapo kuu imeunganisha wanawake woooote sio wote wanafanana tabia na mkeo Mkuu
 
Shida ya wanawake wengi ni kuwa akishapata Nguvu za kiuchumi tu tayari anadhani yeye na wewe mnalingana katika kuongoza familia, anasahau kuwa mwanaume ni mwanaume tu na ndiyo kichwa cha familia (kwa mujibu wa maandiko matakatifu) hivyo huyo mkeo alianza kuzuzuka baada ya kupata Kazi huko TRA na kuanza kulamba mpunga.Shame on her! NB: Mchango wangu huu nimeutoa nikiamini kuwa ulichoandika ni ukweli vinginevyo ningepaswa kwanza kumsikia na mkeo anasema nini kuhusu hiyo issue.
 
Ni tabia ya baadhi ya binadamu, kujisahau majukumu yao na kwenda na kile kilichopo, hao ndo tunawaita bendera fuata upepo,
 
ur genius bro ume solve ipasavyo.....wanawake ni hamnazo tatizo wametuzaa tu .tungekua tunatoka kwenye MITI au MATRANSFOMER mbona wangeelewa KAZI
 
Banaee, hao watu karibu wote wanafanana, Ila next time usikimbie nyumba, mwanaume hakimbii nyumba, Komaa naee..
 
Mkuu mie naona ulichokifanya ni kurudisha heshima iliyokuwepo mwanzo hapo nyumbani ila bado kuna suala la kujiheshimu yeye kama yeye,maana bila ya hivyo unaweza ukaheshimiwa ila yeye akawa hajiheshimu.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom