Wanawake wa kibongo na maisha ya mteremko

Wanawake wa kibongo na maisha ya mteremko

Ngoja wanakuja, wapo kwa Gwajima bado
 
Bado tupo pale pale yaani ukioa mke akiwa ananjua unapesa na gari zuri,ujue kabisa mkeo anapenda hela na siku bahati mbaya umeanguka iwe magonjwa kuyumba ki uchumi,kufukuzwa kazi au kuzidiwa na majukumu hawa wanawake hawatoagi msaada wowote kwenye family,Zaidi ya kubadilika tabia na maana ujue kabisa alikuwa anataka mtu mwenye uwezo wa kimaisha yaani ye ni kama zigo hamuwezi kishare chake na siku akitoa ujue ataandika na status kwenye watsapp
 
Wote wana shida si WANAUME si WANAWAKE.......kwahy msilaumiane hapa
 
Mwenyezi mungu hajakataza kuomba unachotaka wana haki yakuomba hata kuolewa Tajiri yoyote Duniani,ila mda ukiwa unaenda na demand zinapungua, mpaka mwisho watasema yoyote tuu niondoe nuksi...
 
Baadhi ya kina dada wanakoseaga sana kumfanyia mtu tathmini kwa muonekano wake..Dada kweli ameenda kwenye maombi anataka mume mwenye pesa siku 1 amekaa kwenye hotel akaja bwana 1 alievalia simple tu, Akamsalimia yule dada, dada akaitika kwa shida tu wakaendelea kukaa pale jamaa akawa anachezea simu yake tochi akahudumiwa akamwambia dada ongeza kinywaji yule dada akamwangalia toka chini hadi juu..akafyonza..Jamaa hakuchoka akamwambia dada samahi unaitwa nani...Dada kawa mkali mno jamaa akaamua kuachana nae...Kidogo simu yajamaa ikaita akaanza kuongea...''Safi tu niko TZ sasa nimetua jana nitakaa kidogo hapa TZ siunakumbuka nilikuambia nataka nioe TZ wasichana wa Kimarekani siwawezi kwa hiyo nitahakikisha napata mke hapa TZ ndo nije nae huko Amerika..Lakin nataka nisimamie na ile nyumba yangu imaliziwe kule masaki kwa hivyo ndo mchakato niko nao...Jamaa ile kakata simu..Yule dada akawa kama ndo amemwona jamaa kwa mara ya kwanza eti akamwambia jamaa ''Shkamoo kaka ...Mimi naitwa Nancy..Samahani eti ulikuwa unasemaje tena?
 
Hujambo Exec....?
Mie sipendi mteremko ila kuolewa na mtu nimtoe chini haiwezekani aisee.Akifika juu anaanza kuwa juu ya michepuko.Mwanaume tabia yako inajulikana ukiwa na vihela kidogo.Wako wengi wamewatoa wanaume wao chini na sasa wanajuta.Wanaume waliotolewa chini ni majanga kwenye ndoa nyingi.
 
Mtihani wa Mahusiano umezidi kuwa Mkubwa sana kwa Vijana wanaotaka wenza,
Kila nikitazama vijana wa kike ni wachache sana wenye uwezo wa kuwa na familia kwa maana ya kwamba ana uwezo wa kubeba familia( Baba, mama, wadogo), Hivi kweli sisi tukizeeka tutajisikiaje kama watoto wetu watatutelekeza kisa mwanamke wake hakutaki.....hivi ni kweli msichana wa kibongo kwa sasa ni nadra sana kumwuguza mama mkwe wake???
Nikitazama sisi Vijana wa kiume, Roho yangu inauma, Moyo unabubujika damu, Me Sielewi kabisa tunakoelekea, Yani hali si shwari.........Sasa tunatembea na Mama Zetu wa Kutuzaa, Kibaya Zaidi najisikia vibaya sana ninapoona vijana wa kiume wanapaka poda arghhhhh! Kila nikiwaza natamani kuhama Dsm nikakae kijijini, Hivi wewe unayetembea na Mama wa kukuzaa au unapaka poda unaweza kuja kuwa baba mwajibikaji kweli???
Mungu tunusuru.
 
HESHIMA KWA WAKULIMA ITARUDI......NA HAPO NDIO NDOA NYINGI ZITATULIA
 
Kila Siku wanashinda kwenye nyumba za ibada, wakifunga na kuomba ili wapate wanaume wa kuwaoa.

Unadhani kuna mwanaume mjinga aliyetafuta pesa Kwa shida hadi akafanikiwa eti akuchukue tu wewe ule bata, Thubutuuuu... na kama akikuchukua basi ujue mpo wengi na si peke yako.

Wanapenda sana mteremko, hawajui maana ya ndoa, kwao ndoa ni starehe na kula bata, kila mara wanabaki kupeana moyo eti ipo Siku na wao watakuwa Kama flani aliyeolewa na tajiri flani, nyooooo... hilo zali huwa linatokea mara moja baada ya miaka 50.
Halafu wakiambiwa ukweli ni wakali Kama pilipili.

Waoaji wapo wengi sana ila tatizo nyie mnachagua sana, shauri yenu na muda si rafiki, yetu macho.
@Ciprofloxacin: kwa hii "post" umebugi (lugha ya mitaani). Nimeweka nukuu chache tu za maneno yako ambayo ukiyasoma kwa kina utaamini kwamba:

1) aliyeandika hakuzaliwa na mwanamke, hana dada, hana binti na kwa ujumla anaishi dunia ya wanaume tu.

2) wanawake wanapenda kuolewa zaidi kuliko wanaume.

3) wanawake hutegemea wanaume kuendesha maisha yao.

4) hutegemea ndoa kuonekana katika jamii.

Jifikirie kwanza tangu ulipozaliwa hadi ulipo kwa sasa (kiasi cha kuandika hayo):

1) ulipitia mikono ya nani!

2) Familia yako inaishije?

3) unamsaidiaje mama, shangazi na dada yako anayeshinda kanisani/msikitini.

Maneno uliyoandika ni kashfa nzito kwa ustawi wa familia kwa kuwa mwanamke ndiyo nguzo kuu. Kwenda kanisani/kuomba si kwa sababu ulizozioanisha hapa. Matendo maovu kwenye familia ndiyo huwasukuma akina mama kwenda kwenye maombi. Wanawake ndiyo wafariji wakuu kunapokuwa na matatizo.

NANI KAMA MAMA
 
Baadhi ya kina dada wanakoseaga sana kumfanyia mtu tathmini kwa muonekano wake..Dada kweli ameenda kwenye maombi anataka mume mwenye pesa siku 1 amekaa kwenye hotel akaja bwana 1 alievalia simple tu, Akamsalimia yule dada, dada akaitika kwa shida tu wakaendelea kukaa pale jamaa akawa anachezea simu yake tochi akahudumiwa akamwambia dada ongeza kinywaji yule dada akamwangalia toka chini hadi juu..akafyonza..Jamaa hakuchoka akamwambia dada samahi unaitwa nani...Dada kawa mkali mno jamaa akaamua kuachana nae...Kidogo simu yajamaa ikaita akaanza kuongea...''Safi tu niko TZ sasa nimetua jana nitakaa kidogo hapa TZ siunakumbuka nilikuambia nataka nioe TZ wasichana wa Kimarekani siwawezi kwa hiyo nitahakikisha napata mke hapa TZ ndo nije nae huko Amerika..Lakin nataka nisimamie na ile nyumba yangu imaliziwe kule masaki kwa hivyo ndo mchakato niko nao...Jamaa ile kakata simu..Yule dada akawa kama ndo amemwona jamaa kwa mara ya kwanza eti akamwambia jamaa ''Shkamoo kaka ...Mimi naitwa Nancy..Samahani eti ulikuwa unasemaje tena?

hahahahahahahahaha JF oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Daily Dream of Ready Made men -Kuna wanawake wengi wamefia hapa na kubaki ndani ya mijumba mikubwa na magari ya kutosha lakini love hakuna ,wanakuwa watumwa wa wanaume matajiri.Hii Tabia ni mbaya sana badilikeni tafuta mtu muanze naye from Zero and you will never regret.
 
wanaume wa dar ndivo walivo! ivi nikuulize, mnapomtongoza bint kwani mnaanza kuuliza una kazi gani?? akikwambia mam ntilie unapotea mazima why?? Kuna wale wanaotafta virgn kisa kahangaika kusaka mali wakati ye kageuzwageu
zwa na wadada km 50 hiv,. je huyo virgn ni size yako??? unazani hana wake??? Au kisa mali ndo mnazan mmepangiwa kuwaoa la hasha msijidanganye nao hao wana wakwao waliotoka nao mbali na wanawatunzia watu wao nyie kazana kutafta mali kwaajil ya kuwa ridhisha walio kwisha bikiriwa ndio kazi mliyopangiwa kama hamjui hawa wana wa kwao wanaoendna nao,. so dont judge 1 side of a coIn,.
Aisee mbona hasira hivyo.taratibu basi atakuelewa tu.
 
Kila Siku wanashinda kwenye nyumba za ibada, wakifunga na kuomba ili wapate wanaume wa kuwaoa.

Hilo ni jambo jema sana, maana sisi sote kimbilio letu ni MUNGU tu.
Pamoja na yote hayo, hebu jaribu kuwadodosa mawazo yao hao wanaomlilia Mungu ili awapate waume wa kuwaoa, utachoka na kuishiwa pozi kabisa,kila mmoja wao anawaza aolewe na mwanaume mwenyewe gari zuri, nyumba nzuri, kazi nzuri au biashara kubwa, wanamwomba Mungu halafu tena wanampangia na aina ya mume wanayetaka, hii ni sawa na mtu ana njaa, anakuomba chakula tena masharti na mkwara juu, kwamba ni kweli ana njaa, ila hataki ugali dagaa, anataka umpatie chakula chenye gharama Kubwa.
Na ndo maana Mungu hajibu maombi yao, miaka inaenda, rudi, hadi sura zao zinaanza kuchuma kunde, mwisho wanakata tamaa na kuwa ma senior spinsters.

Unadhani kuna mwanaume mjinga aliyetafuta pesa Kwa shida hadi akafanikiwa eti akuchukue tu wewe ule bata, Thubutuuuu... na kama akikuchukua basi ujue mpo wengi na si peke yako.
Wanapenda sana mteremko, hawajui maana ya ndoa, kwao ndoa ni starehe na kula bata, kila mara wanabaki kupeana moyo eti ipo Siku na wao watakuwa Kama flani aliyeolewa na tajiri flani, nyooooo... hilo zali huwa linatokea mara moja baada ya miaka 50.

Halafu wakiambiwa ukweli ni wakali Kama pilipili.
Bure ina tabu yake, jengeni tabia ya kuishi na wanaume toka wakiwa maskini hadi wanafanikiwa, Kwa maana ya kwamba mtafute wote mali, na siyo tabia yenu ya kudandia magari Kwa mbele, ndo maana yanawagonga na hamwishi kulia kila siku.

Kwa tabia zenu za kuwaza kuolewa na waliofanikiwa tayari mtasubiri sana, matokeo yake mnaanza kuchukia wanaume bila Sababu .
Waoaji wapo wengi sana ila tatizo nyie mnachagua sana, shauri yenu na muda si rafiki, yetu macho.
Naona umesahau kuzungumzia wanaume wanaopenda wanawake wenye kazi na mali. Haya ni mabadiliko ktk jamii. Mbona sikuizi amuoi wanawake kutoka vijijini kwenu, kama nyie watafutaji kweli?
 
Back
Top Bottom