Wanawake wa kibongo na maisha ya mteremko

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,697
Kila Siku wanashinda kwenye nyumba za ibada, wakifunga na kuomba ili wapate wanaume wa kuwaoa.

Hilo ni jambo jema sana, maana sisi sote kimbilio letu ni MUNGU tu.
Pamoja na yote hayo, hebu jaribu kuwadodosa mawazo yao hao wanaomlilia Mungu ili awapate waume wa kuwaoa, utachoka na kuishiwa pozi kabisa,kila mmoja wao anawaza aolewe na mwanaume mwenyewe gari zuri, nyumba nzuri, kazi nzuri au biashara kubwa, wanamwomba Mungu halafu tena wanampangia na aina ya mume wanayetaka, hii ni sawa na mtu ana njaa, anakuomba chakula tena masharti na mkwara juu, kwamba ni kweli ana njaa, ila hataki ugali dagaa, anataka umpatie chakula chenye gharama Kubwa.
Na ndo maana Mungu hajibu maombi yao, miaka inaenda, rudi, hadi sura zao zinaanza kuchuma kunde, mwisho wanakata tamaa na kuwa ma senior spinsters.

Unadhani kuna mwanaume mjinga aliyetafuta pesa Kwa shida hadi akafanikiwa eti akuchukue tu wewe ule bata, Thubutuuuu... na kama akikuchukua basi ujue mpo wengi na si peke yako.
Wanapenda sana mteremko, hawajui maana ya ndoa, kwao ndoa ni starehe na kula bata, kila mara wanabaki kupeana moyo eti ipo Siku na wao watakuwa Kama flani aliyeolewa na tajiri flani, nyooooo... hilo zali huwa linatokea mara moja baada ya miaka 50.

Halafu wakiambiwa ukweli ni wakali Kama pilipili.
Bure ina tabu yake, jengeni tabia ya kuishi na wanaume toka wakiwa maskini hadi wanafanikiwa, Kwa maana ya kwamba mtafute wote mali, na siyo tabia yenu ya kudandia magari Kwa mbele, ndo maana yanawagonga na hamwishi kulia kila siku.

Kwa tabia zenu za kuwaza kuolewa na waliofanikiwa tayari mtasubiri sana, matokeo yake mnaanza kuchukia wanaume bila Sababu .
Waoaji wapo wengi sana ila tatizo nyie mnachagua sana, shauri yenu na muda si rafiki, yetu macho.
 
Wewe waache wadada wa watu,
Nadhan mtu anaomba what her heart desire most,
And binadamu wote we selfish in nature

Hata wewe ukisali unaomba unachotaka sio masharti unampa Mungu,
Eg; Ukiumwa unaomba upone kwa nn husiombe kufa, Ukifanya mitihan unaomba kufaulu kwa nn husiombe kufeli
 
kuna mengi ya kiuchambuzi lakini naona hili limekuja baada ya maisha kuanza kubana namengi sana yatakuja humu hata yale ya kuombwa vocha etc
Hahahaah ya kuombwa vocha mbona kila siku yanaletwa humu??
 
harafu cha ajabu huyo anayekupa hayo masharti ukimuangalia haendani hata na anachokiwekea masharti. Unakuta mashavu yashaanza kushuka harafu bado anajiita mrembo
 
wanaume wa dar ndivo walivo! ivi nikuulize, mnapomtongoza bint kwani mnaanza kuuliza una kazi gani?? akikwambia mam ntilie unapotea mazima why?? Kuna wale wanaotafta virgn kisa kahangaika kusaka mali wakati ye kageuzwageu
zwa na wadada km 50 hiv,. je huyo virgn ni size yako??? unazani hana wake??? Au kisa mali ndo mnazan mmepangiwa kuwaoa la hasha msijidanganye nao hao wana wakwao waliotoka nao mbali na wanawatunzia watu wao nyie kazana kutafta mali kwaajil ya kuwa ridhisha walio kwisha bikiriwa ndio kazi mliyopangiwa kama hamjui hawa wana wa kwao wanaoendna nao,. so dont judge 1 side of a coIn,.
 
tehe tehe tehe tehet tehe kuachwa kuachwa kuachwa ni shughuli ndefu aaahh mbaya zaidi kwa yule uliyempenda..............just singing
 
kuna mengi ya kiuchambuzi lakini naona hili limekuja baada ya maisha kuanza kubana namengi sana yatakuja humu hata yale ya kuombwa vocha etc
yote haya kayataka Magufuli kubana mianya yote. Siku za nyuma hatukuwasikia hapa sasa hivi wamegundua kumbe mishahara pekee haitoshelezi kukidhi na kina 'bebi' wa nje wanajifanya kuwapaka.
 
Mtu ana wanawake zaidi ya wawili na wote wanahitaji matunzo unategemea nini.. Kaa tulia na wako uone kama utapiga kelele humu jf. Tatizo kuendekeza tamaa na mwanamme kulia lia kushindwa kumtunza mwanamke wake ni udhaifu sasa kwa hali hiyo kuna kuoa hapo. Halafu ukifika wakati wa kuoa mnataka muoe waliosoma why?? Si wanasema mapenzi hayachagui right??. Acha kulalamika piga kazi...
 
wanaume wa dar ndivo walivo! ivi nikuulize, mnapomtongoza bint kwani mnaanza kuuliza una kazi gani?? akikwambia mam ntilie unapotea mazima why?? Kuna wale wanaotafta virgn kisa kahangaika kusaka mali wakati ye kageuzwageu
zwa na wadada km 50 hiv,. je huyo virgn ni size yako??? unazani hana wake??? Au kisa mali ndo mnazan mmepangiwa kuwaoa la hasha msijidanganye nao hao wana wakwao waliotoka nao mbali na wanawatunzia watu wao nyie kazana kutafta mali kwaajil ya kuwa ridhisha walio kwisha bikiriwa ndio kazi mliyopangiwa kama hamjui hawa wana wa kwao wanaoendna nao,. so dont judge 1 side of a coIn,.
Mbona povu linakutokaa
 
Mie sipendi mteremko ila kuolewa na mtu nimtoe chini haiwezekani aisee.Akifika juu anaanza kuwa juu ya michepuko.Mwanaume tabia yako inajulikana ukiwa na vihela kidogo.Wako wengi wamewatoa wanaume wao chini na sasa wanajuta.Wanaume waliotolewa chini ni majanga kwenye ndoa nyingi.
 
Ukimpata wa kufanana nae lazima unajua na hutabanduka kwake no matter what, wakufanana nae atakuja tu keep praying!
 
Aiiiiiiiiiiii ujinga gani huu! Mkuki kwa nguruwe! jamani nyie ndo mnashinda kulalama mda wa kuoa umefika una hata wa kusingiziwa vigezo vingi kama mkopo wa nmb.

Mara utaskia nataka wife awe na zigo nyuma, mrefu wakati wewe kifupiii!, mweupe mwenye heshima, awe na kazi, sifa kibao kama mganga wa kienyeji!

Anyway you have a right not to remain silent!
 
Back
Top Bottom