Wanawake wa kiafrika wa siku hizi wavivu sana (Ma lazy)

Mi huwa najiuliza, kama washing machine ipo, kwanini mtu ajisumbue kufua? Kama trekta lipo, jembe la mkono unalitumia ili iweje? kwanini utwange mahindi kwa kinu, wakati mashine za kusaga zipo?

Na kama wanaume tupo, kwanini wanawake watwange mahindi.

Wanawake wanaonewa sana asee. Tena mnaonewa zaidi na wavulana. Mwanaume wa kweli hamtesi mkewe, bali anamtunza.

Wanawake wote semeni Amina.

well said! yaani wanaona mwanamke akitwanga wkt yeye yupo na hana shighuli, ndio inaonyesha ukidume ndani ya nyumba.
kweli sie wengine tuna bahati kupata wenza walio tayari kutusaidia (especially) kazi za kutumia nguvu bila hata kuwaomba msaada.

kuna siku nilisema wanaume muwafundishe wavulana jinsi ya kuishi na wapenzi wao. maana hawakawii kwenda kusema kwa mama

.
 
Hao wenye uwezo wa kununua majenereta kwa kipato cha kazi zao halali bado wanaitwa wavivu?

wavivu kwa kazi za kike, waafrika tuna kazi za kike na kazi za kiume, tusisahau mira na desturi zetu. watu mkipata wageni toka kijijini mkikumbushia za kijijini mnalazimika kula ugali wa unga wa kutwanga kwa mkono, mama lazima awe tayari kwa hilo.
 
makazini tuende kama nyie, tukirudi home tukoboe mahindi na mpunga kwenye kinu. unaishi dunia hii ya leo au? halafu nawaza hiyo sugu ya kwenye mikono kwa ajili ya kutwanga, kama fundi makenika vile!

Asprin na The Boss, nimeipenda sana michango yenu kwa hii thread.
 
Last edited by a moderator:
wavivu kwa kazi za kike, waafrika tuna kazi za kike na kazi za kiume, tusisahau mira na desturi zetu. watu mkipata wageni toka kijijini mkikumbushia za kijijini mnalazimika kula ugali wa unga wa kutwanga kwa mkono, mama lazima awe tayari kwa hilo.

hao wageni wa kijijini kama ni lazima wale wa kutwangwa, nitawatafutia kinu watwange wenyewe kwa kweli, maana mi nitaenda mashine
 
Mi huwa najiuliza, kama washing machine ipo, kwanini mtu ajisumbue kufua? Kama trekta lipo, jembe la mkono unalitumia ili iweje? kwanini utwange mahindi kwa kinu, wakati mashine za kusaga zipo?

Na kama wanaume tupo, kwanini wanawake watwange mahindi.

Wanawake wanaonewa sana asee. Tena mnaonewa zaidi na wavulana. Mwanaume wa kweli hamtesi mkewe, bali anamtunza.

Wanawake wote semeni Amina.

Sikioni kitufe cha like. Pokea like like like
 
Hehehhe mlioni CC haya am here,
mweeh em acheni zenu
MBONA NYIE HAMUENDI KUWINDA NA KUKATA KUNI???inahusuuu.....mtuwache jmnn...
Km dishwasher ipo nioshe vyombo ili iwejeee
tunavohangaika kusoma,tafuta pesa huwa ni kwa lengo ganiii KAMA SIO KUSIMPLIFY MAISHA??
Beki tatu muhimuuuu unless niwe na vitendea kazi digitali,majiko ya gesi,oven,vacuum cleaner,washing machine nk...:MPO HAPOOOOO.....
 
Wanaume wa kileo mnauweza mziki wa KUUA SIMBA NYIE??KAMA MORANI?acheni zenu,na mnavokula chipsi kuku na mabia hehe,....
Au mnapenda tu kazi nyepesi tuu,wengine ht gym hakuna,wala zoezi ht kibarazani au mpira ligi za mbuzi hamtaki tena...
Iwe iwavyo,mzungu kasha'simplify mengi,so ts js getting money na kununua,nitwange blender zimeisha??mashineni si kupo?dona hata shoprite si linauzwa...semeni kingine
 
tena wanawake wa siku hizi wengi ndio wachapa kazi wanafanya kazi maofisini na kwenye vibarua huko ilimradi apate cha kulisha familia yake ila wanaume wengi ndo wamekuwa wavivu kazi hawafanyi.
 
mnataka aharibu kucha zake from american nails!!!weeeeeee thubutuuu
 
Well kiaina flani nawatetea wanawake wa cku hizi ya kuwa wachakalikaji wanasaka mshiko na kuokoa jahazi inapobidi ila basi wasipitilize wala kusahau majukumu ya nyumani maana imekuwa taabu sana nowdays kwa kuwa NDOA UREMBO MAJUKUMU YA NYUMBANI HOUSE GIRL.
 
Amina.

Nikute hapa kaunta ya wazee wa mujini.

Mi huwa najiuliza, kama washing machine ipo, kwanini mtu ajisumbue kufua? Kama trekta lipo, jembe la mkono unalitumia ili iweje? kwanini utwange mahindi kwa kinu, wakati mashine za kusaga zipo?

Na kama wanaume tupo, kwanini wanawake watwange mahindi.

Wanawake wanaonewa sana asee. Tena mnaonewa zaidi na wavulana. Mwanaume wa kweli hamtesi mkewe, bali anamtunza.

Wanawake wote semeni Amina.
 
Bora mtuone wavivu tu,nina washng mashine nifue niharibu kucha inahuuuu,mshine zimejaa nitwange kwa kinu haihuuu kwanza chaguo la mama inarahisisha!hg lazima niwe nae kwa shughuli baadhi,kupika na kufua kufuli za mr ndio nafanya mie!twaenda na wakti bana
 
He he he, ukute na kipato anazidiwa, bajeti anapanga yeye, bado nitwange? Tufyakwa!

Tufanye kwa mfano mkeo ni mfanyakazi. Mnadamka wote kwenda kibaruani. Na wote mnarudi late hours. Afu bahati nzuri kipato chake kiwe sawa na chako. Bado utamwita mvivu kwakuwa anafuga kucha na hatwangi mahindi ya makande?
 
Back
Top Bottom