Wanawake wa JF mnasemaje kuhusu hili?

Wanawake wa JF mnasemaje kuhusu hili?

mito

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2011
Posts
10,811
Reaction score
11,031
WANAWAKE WAUNGANA KUSUSIA BIDHAA NA MAONYESHO YA MWANAMUZIKI DIAMOND

Ni kwa Kumdhalilisha Bi. Wema Sepetu kwa kumrekodi katika simu na kusambaza mazungumzo nyeti!

Kitendo cha Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond,cha kurekodi mazungumzo yake na star wa Bongo Move Bi. Wema Sepetu, na kuyatuma mazungumzo yao ya mapenzi katika mitandao ni kitendo cha "Udhalilishaji wa Mwanamke."

Kwa kuwa wanamuziki na wasanii wote wanatakiwa wawe ni mfamo na kioo cha jamii katika kielekeza jamii kuishi kwa kufuata na kuheshimu mahadili, lakini mwanamuziki Diamond ameonekana kuwa ni kiongozi wa "Udhalilishaji wa Mwanamke" kufuatia kitendo chake cha

kurekodi na kusambaza mazungumzo yao ya simu ya kimapaenzi kati yake na Bi.Wema Sepetu na mpenzi wake wa sasa Bi. Penny, kitendo hiki ni cha "kuwadhalilisha wanawake wa kitanzania."

Tunaowaomba akinamama na kinadada na wanawake wote kwa ujumla kususia kununua video, vcd, cd pia kugomea kuhudhuria onyesho lolote lile litakalofanya na mwamuziki.

Nasibu Abdul Juma aka Diamond hadi pale atakapo waomba radhi wanawake wote wa kitanzania popote pale walipo.

Wanawake wote wanatakiwa kugomea maonyesho ya mwanamuziki huyo na na kutonunua bidhaa za mwanamuziki huyo Diamond ili kukomesha kabisa tabia hizi chafu za "Udhalilishaji wa Mwanamke."
 
Mie nilishamsusa kitambo toka aonyeshe tabia ya kubadili k kama boxer zake
 
okay ..

Wote wanamakosa.

Wema anamuomba amrudie jamaa na jaamaa
tayari ana bi dada mwingine.

Diamond na ye ameonyesha jinsi alivyo na akili za kijinga
kupita kiasi.

samahani wanawake mimi siwaungi mkono kabisa.
Ntazidi kusikiliza nyimbo zake na kuona show zake.

Life goes on................
 
Na tatizo lipo hapo kwa red! Ni kama ule msemo wa kichaa akikukuta ziwani unaoga halafu akakimbia na nguo zako, na wewe ukatoka majini uchi unamkimbiza, nani ataonekana kituko zaidi????
 
Diamond kajionyesha kuwa hana ustaarabu

Wema nae kajionyesha hana busara kwenye maamuzi yake
 
Na tatizo lipo hapo kwa red! Ni kama ule msemo wa kichaa akikukuta ziwani unaoga halafu akakimbia na nguo zako, na wewe ukatoka majini uchi unamkimbiza, nani ataonekana kituko zaidi????
Ndo hapo sasa..

lakini usema ukweli napenda nyimbo zake.
na ntazidi kuzisikiliza.

Mengine ulimwengu utamfunza..
 
Ndo hapo sasa..

lakini usema ukweli napenda nyimbo zake.
na ntazidi kuzisikiliza.

Mengine ulimwengu utamfunza..

Huyu hajui kukoma nae

Kama kudhalilishwa ile ya kwenye show ya Diamond ilikuwa zaidi ya kutosha

Sasa anatafuta nini zaidi

Wote wawili wapo katika kufunzwa na ulimwengu sawa na sie wengine tulobakia
 
Diamond kamdhalilisha mwenzake kupeleka maongenzi yao kwenye vyombo vya habari,ni mbaya sana hii
 
Diamond kamdhalilisha mwenzake kupeleka maongenzi yao kwenye vyombo vya habari,ni mbaya sana hii

Huyo msichana kajitakia.

Kajitakia kwa sababu tayari alishaadhirishwa hadharani na huyo huyo jamaa.

Kwangu hiyo ingekuwa tosha kabisa kuacha hata kuwaza kumuongelesha.

Sasa mtu aliyekufanya kituko mbele ya hadhira unampigia simu sijui kumbembeleza aje kwako...what kinda foolishness is that?

Na kama hiyo haitoshi, tayari inajulikana kuwa jamaa yuko kwenye mahusiano na mtu mwingine.

Nini tena unachokitaka kutoka kwake ambacho huwezi kukipata kwa mwingine?

SMFH!!
 
Ndo kosa la kujidai unamwaga mtu kumbe bado unampenda,angejua angeendelea kuwa na diamond,sio akamwacha na at the same time hayuko tayari kutokua nae
 
Hao raia wasiwaumize vichwa, nahisi wameamua kufanya maigizo tu ili wapata "attention" kwa watu.
Na hata kama ni kweli kwa mtu kama Wema anavyopenda "publicity" nadhani atakuwa amefurahi kwa sasa kuwa "talk of the town" manake alikuwa amepumzishwa kidogo na media za bongo.
 
No such thing as bad publicity huh...maana sasa hivi kaweza kukusanya huruma toka kwa watu wengi.
 
Huyo msichana kajitakia.

Kajitakia kwa sababu tayari alishaadhirishwa hadharani na huyo huyo jamaa.

Kwangu hiyo ingekuwa tosha kabisa kuacha hata kuwaza kumuongelesha.

Sasa mtu aliyekufanya kituko mbele ya hadhira unampigia simu sijui kumbembeleza aje kwako...what kinda foolishness is that?

Na kama hiyo haitoshi, tayari inajulikana kuwa jamaa yuko kwenye mahusiano na mtu mwingine.

Nini tena unachokitaka kutoka kwake ambacho huwezi kukipata kwa mwingine?

SMFH!!

Nyani Ngabu unamaanisha (hapo kwa red) alichofanya diamond ni sahihi? yaani kupeleka mazungumzo yao ya faragha kwenye media...
 
Nyani Ngabu unamaanisha (hapo kwa red) alichofanya diamond ni sahihi? yaani kupeleka mazungumzo yao ya faragha kwenye media...

Hapana, hata yeye huyo dogo naye hakufanya vyema.

Licha hivyo, mimi simuonei huruma huyo msichana maana inaonekana kama vile hana busara wala akili za kawaida.

Nimeshangaa sana kwa nini hata aliamua kumpigia simu huyo dogo na kumbembeleza aende kwake.

Mpaka kitokee nini ndiyo ajue kwamba jamaa hamtaki? Mpaka kitokee nini?

Will this be the last straw before she comes to her senses?
 
Huyu hajui kukoma nae

Kama kudhalilishwa ile ya kwenye show ya Diamond ilikuwa zaidi ya kutosha

Sasa anatafuta nini zaidi

Wote wawili wapo katika kufunzwa na ulimwengu sawa na sie wengine tulobakia
Gaijin kuna wanawake wanamoyo kweli..

Wema kumbembeleza vile huyu jamaa inaonesha jinsi alivyo "desperate"
Na Diamond naye anaonyesha jinsi alivyo " immature"

watajiju bana.
mi umbea kama huu kwanza naupenda.
wameamua kuaibishana ku act kama watu ambao hajabaleehe .
kwa raha zao.
 
Pesa jamani pesa......loh!!!! inasababisha mtu apoteze thamani yake!
 
Back
Top Bottom