cutelove
JF-Expert Member
- Oct 3, 2017
- 3,317
- 7,509
Mwanamke umebahatika kupata mwanaume wako wa ndoa,mnaishi vizuri tu,lakini kwa nini sisi wanawake tunakuwa tunawategea wanaume na huku unajua fika hali ya mmeo? Na huku tuna ingiza vipato vyetu wenyewe
Kuna mkaka nimemuonea hadi huruma
Huyu kaka ni mfanyakazi wa serikali na mke wake pia
Siku za hivi karibuni amemaliza chuo,ila gharama za chuo alikuwa anajigharamikia kwa kiasi kikubwa na kulingana na maisha ya chuo na gharama ,aliweza kukopa kwenye Benki moja hivyo kwa wastani kwa makato ya mshahara wake ,mshahara ukawa mdogo sana,na ulivyotoka wa mwezi uliopita alilipa kodi ya nyumba na nyingine kwenye shughuli za kilimo,akawa hana kitu
Na bahati nzuri mke wake anajua hali yake ya uchumi na kila kitu
Sasa leo mke wake kasafiri kwenda nyumbani kwao,na kwa vile mke wake anajua hali ya mme wake,mwanaume akafikiri mwanamke angefanya shopping ya mahitaji ya ndani kabla hajaondoka ili watoto wao watatu na mmewe wasipate shida
Lakini mwanamke hakununua mahitaji ya ndani ameondoka kwenda kwao akisema wazazi wake wamemuita kwa dharura
Mwanaume alivyojaribu kumuuliza "Mbona umetuacha bila kitu ndani?
Majibu ya mwanamke" Hivi wewe si ndo mwanaume, yaani unadiriki kuniambia jambo kama hilo,kwani mimi ndo mwanaume wa familia,wewe fanya mpango mle na wanao lakini sio kuniambia mambo ya ajabu"
Loh! Kaka wa watu mpaka nimemhurumia,
Jamani na sisi wanawake tuwe na utu,familia ni ya wote, na kama mwanaume hali si nzuri,ajibika asilimia 100,lakini si kwa roho mbaya hiyo