Wanawake tuwe makini na huu uamuzi

Nandinii

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2019
Posts
2,572
Reaction score
2,829
Habari zenu wakuu, wengi wa wanawake nimeweza kuwashuhudia pale wanapoona kuwa wenza wao hawana dalili ya kuwaoa basi uamua kubeba mimba kama ticket ya kuolewa. Anaona kwamba kama nikiamua kubeba mimba atanioa au lah kama nikibeba mimba basi wazazi wataweza niruhusu niende kwa yule mwanaume nikaishi nae.

Binafsi hili jambo huwa sioni kama ndiyo suluhisho sahihi kwa wadada ili wapate kuolewa mapema. Nimeweza kushuhudia zaidi ya mara 2 wanawake kubeba mimba ili waolewe lakini matokeo yake ndoa imekuwa yenye karaha na vituko kila kukicha, kiasi kwamba nikiwaangalia nawaonea huruma sana. Ingawa sio wanaume wote ambao watakutesa kwasbb umelazimishia mimba.

Ni bora hata iingie kwa bahati mbaya lakini sio uibebe kwa makusudi , huwa ni jambo baya sana wadada wenzangu, mana muda mwingine unakuwa umejifunga kitanzi mwenyewe bila kushurutishwa na mtu. Kama imeingia bahati mbaya basi mshukuru Mungu na ilee mimba yako lakini sio kubeba mimba ili uweze kuolewa mapema sababu tu mwanaume hana uelekeo wa kukuoa au umekaa na Pete ya uchumba kwa muda mrefu, huwa si jambo jema.

Naongea ili jambo kwa uchungu sana na lenye kuniumiza, sababu ya watu wa karibu ninaowafahamu kupitia tabu sababu ya kulazimishia mimba ili wapate kuolewa. Siyo wote ambao wataharibikiwa pale wanapobeba mimba kwa makusudi ili waolewe, mana wapo wanaume waelewa ,atakuoa na mtaishi vizuri tu lkn wapo wengine ambao atakuongezea machungu na maumivu ya moyo usiyoyatarajia.

Wadada wenzangu tuwe makini katika hili swala na tusipende kuchukua maamuzi ya ghafla bila kufikiria, kwa sbb tu huyu mwanaume hana dalili ya kunioa basi komesha yake ni mimba tu. Wazazi hawataki kuniruhusu niolewe na mwanaume hana uwezo wa mahali basi komesha yake ni mimba tu ili niende. Si jambo zuri hili, km anakupenda atakuoa kwa wakati sahihi na mtaishi kwa amani, utazaa kwenye ndoa lkn si kubeba kwa makusudi maana matokeo yake ni makubwa.
 
Nanyi wanaume sio kwasababu mwanamke kakusakizia mtoto ukiwa huna nia hio basi ndio unatelekeza mtoto na mama.
Tufanye ujinga wote ila kamwe tusitekeleze damu zetu nyuma..mateso yao yanabeba laana maishani mwenu
 
Kila mtu na bahati yake ..wangu me nilitegesha na ngoma ikaclick now tuna watoto wawili na ndoa yenye amani n furaha.
Sasa ndugu zangu wale wenye damu za kunguni chukueni tahadhari hawa kina Shabani siku hizi hawaeleweki
 
Kila mtu na bahati yake ..wangu me nilitegesha na ngoma ikaclick now tuna watoto wawili na ndoa yenye amani n furaha.
Sasa ndugu zangu wale wenye damu za kunguni chukueni tahadhari hawa kina Shabani siku hizi hawaeleweki
Ebu njoo pm tuyajenge mama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani acha tu, ni jambo ambalo linaniuma sana. Kulazimishia mimba ili uolewe ni kosa kubwa. Matokeo yake unaambiwa umemuharibia mtu maisha yake na hakuhudumii kwa chochote kwa lolote, ww ndiyo unakua baba ,unakua mama pia. Kisa tu ulibeba mimba kwa makusudi.
 
Ahahah apo ss ni bahati sn. Unaweza tegesha na ukaolewa vzr tu na ndoa ikawa na amani. Ila kuna mtu nimemshuhudia kategesha na kaolewa, lkn huwezi amini mwanaume hataki kufanya chochote kile. Kakaa tu nymbn, lkn mwanamke ndy ss amekuwa baba na amekuwa mama. Fikiria ss tabu anayoipata apo ni ya kiasi gani.
Kila mtu na bahati yake ..wangu me nilitegesha na ngoma ikaclick now tuna watoto wawili na ndoa yenye amani n furaha.
Sasa ndugu zangu wale wenye damu za kunguni chukueni tahadhari hawa kina Shabani siku hizi hawaeleweki
 
Bikra feki za kutengenezwa kupitia ndimu na body plastic sugery ni nzuri au mnajisahaulishaga mlichoongea tu na shetani bustanini kuhusu kujifanya kondoo nnje ya miili lakini ndani ya miili yenu ni mmbwa mwitu?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! Kuna mmoja nilimtokea tukaelewana vizuri kabisa ila hata kabla ya tarehe ya mechi yetu wana Uvinza FC, akanambia habari za kunizalia mtoto!!!!!

Nikaona hapa kuna kitu kinaitwa "kuoa kimasihara" au kubambikiziwa mimba!. Nikawa namzuga tu wala sikutokea uwanjani kabisa.
Mpaka alipohamishwa kikazi nikapumzika na kelele zake. Dah!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…